• ePaper
Saturday, August 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 10, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW, Dodoma

BAADHI ya viongozi wa vyama vya ushirika nchini, wamesema wamefurahishwa na hatua ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuweka mkazo wa kuwatafutia wakulima masoko ya nje ya nchi na kuwawezesha kupata zana za kisasa za kilimo.

Wamepongeza juhudi hizo na kubainisha zitasaidia kuongeza uzalishaji, tija na kipato kwa wakulima.

Viongozi hao walisema hayo kwa nyakati tofauti jana kufuatia kauli ya Rais Dk. Samia aliyoitoa katika kilele cha Maonesho ya Nanenane, jijini Dodoma, kwamba serikali inaendelea kutafuta masoko ya ndani na nje, kuongeza uwekezaji na kutumia majukwaa ya kimataifa kukuza bidhaa za Tanzania.

Alisema serikali imeifungua nchi kibiashara na uwekezaji, huku ikiendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuongeza uzalishaji, thamani na mauzo ya bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi.

Rais Samia alisema kaulimbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu isemayo: “Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira 2050”, imeweka mkazo katika umuhimu wa wazalishaji kutambua soko la bidhaa zao kuongeza tija na kipato.

PENDOEL VALENTINE

Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Manyara, Pendoel Valentine, alisema upatikanaji wa masoko ni jambo la msingi kwa mkulima kwa kuwa humwezesha kuzalisha akiwa na uhakika wa mahali pakuuza mazao na kufaidi matunda ya jasho lake.

Alisema vyama vya ushirika vya kilimo na masoko vinaona hatua hiyo ni fursa kubwa kwa wakulima kwa sababu itaunganisha uzalishaji na masoko, jambo ambalo litachochea wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao yenye ubora na kukidhi mahitaji ya soko.

“Soko ndiyo kila kitu. Masoko yakipatikana, maana yake hata mkulima anapozalisha anajua atauza na tunaamini matokeo yatakuwa na tija,” alisema.

Meneja huyo alisema hali hiyo itawafanya wakulima kuanza kuzalisha kwa kuzingatia mahitaji ya soko badala ya kuzalisha bila kuwa na uhakika wa wanunuzi, akisisitiza mikakati hiyo ni muhimu katika kuimarisha sekta ya kilimo na uchumi wa wakulima.

“Hivi sasa mkulima atazalisha mazao yake akijua kabisa anakwenda kunufaika. Kwetu sisi ni fursa nzuri, tumefurahi na tunampongeza Rais Dk. Samia kwa kuliona hilo,” alisema.

Valentine alisema uwepo wa masoko ya uhakika utasaidia pia kuondoa hofu miongoni mwa wakulima wanaoshindwa kuongeza uzalishaji kutokana na kutokuwa na uhakika wa wanunuzi wa mazao yao baada ya mavuno.

“Tukipata masoko ya uhakika, tukiwa na wakulima walioungana katika vyama vya ushirika, tutakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzalisha na kuuza kwa pamoja,” alisema Valentine.

DAUDI ANDREW

Meneja Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Songwe, Daudi Andrew, alisema uamuzi wa serikali kuwezesha upatikanaji wa zana za kisasa za kilimo, hususan matrekta, utakuwa chachu ya kuongeza ufanisi na kupunguza muda unaotumika katika uzalishaji.

Alisema matumizi ya zana hizo ni muhimu kwa wakulima kwa kuwa baadhi bado wanatumia zana za kawaida ambazo huongeza muda na nguvu katika maandalizi ya mashamba, hali itakayopunguza ukubwa wa eneo linalolimwa na kiwango cha uzalishaji.

“Ukiwa na trekta inasaidia kupunguza muda unaotumia shambani kulima, kwa hiyo ni jambo zuri,” alisema.

Meneja huyo alisema vyama vya ushirika vimepokea kwa furaha mipango hiyo kwa kuwa itarahisisha utekelezaji wa kilimo na kuboresha maisha ya wakulima.

“Tunamshukuru na kumpomgeza Rais kwa kuliona hilo kupitia Wizara ya Kilimo kwa sababu itatusaidia sana kwa upande wetu vyama vya ushirika,” alisema.

Andrew alisema taarifa kuhusu hatua hiyo zilipokewa kwa furaha na wanachama wa vyama vya ushirika, akieleza mijadala katika makundi yao ya mawasiliano ilionesha namna wakulima na wadau wa ushirika walivyofurahishwa na serikali kuendelea kuitambua sekta hiyo.

“Vyama vingi vya wakulima baada ya kupata ile taarifa tulifurahi na tunaishukuru serikali kwa kutukumbuka kwamba ni sekta muhimu inayowakutanisha wakulima,” alisema.

Andrew alisema matumizi ya matrekta na zana nyingine za kisasa yatawezesha wakulima kulima maeneo makubwa kwa muda mfupi, hatua ambayo inaweza kuongeza kiwango cha uzalishaji na kupunguza utegemezi wa zana duni katika kilimo.

“Teknolojia inamsaidia mkulima kufanya kazi kwa muda mfupi na kupata matokeo makubwa. Hivyo tukimsaidia mkulima kupata zana, tunakuwa tumemsaidia kuongeza uzalishaji na hatimaye kuongeza kipato chake,” alisema Andrew.

Naye, Ofisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa Chama cha Ushirika cha Simiyu, Mussa Tule, alisema uamuzi wa serikali ya awamu ya sita wa kuwatafutia wakulima masoko ya nje pamoja na kuwawezesha kupata zana za kilimo, unapaswa kuungwa mkono kwa kuwa una nafasi ya kuongeza tija na kuboresha shughuli za kilimo.

Tule alisema upatikanaji wa masoko ya uhakika na zana bora za kilimo ni sehemu muhimu ya kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija zaidi, huku vyama vya ushirika vikiwa na nafasi ya kuwaunganisha wakulima na fursa hizo.

Previous Post

BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

Next Post

RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

Next Post
RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA KAULI UBORESHAJI WA MITAALA

DK. NCHIMBI ATOA KAULI UBORESHAJI WA MITAALA

5 months ago
DK. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA AFCON 2027

DK. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA AFCON 2027

6 months ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?