• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KUTUMIA DINI KWA AJENDA ZA KISIASA NI KUFURU – PAPA LEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 20, 2025
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
KUTUMIA DINI KWA AJENDA ZA KISIASA NI KUFURU – PAPA LEO

Papa Leo, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani

0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

VATICAN CITY, Vatican

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, amewakemea viongozi wa kisiasa na wa dini wanaotumia imani za kidini kuhalalisha migogoro na vita, kwani kitendo hicho ni kufuru na dhambi kwa  Mungu.

Katika ujumbe wake uliotolewa juzi kuelekea Siku ya Amani Duniani ya Kanisa Katoliki, itakayoadhimishwa Januari mosi, 2026, Papa Leo ambaye ni papa wa kwanza kutoka nchini Marekani, hakumtaja kiongozi yeyote moja kwa moja, lakini alitoa wito kwa waumini wote kupinga matumizi mabaya ya dini katika siasa.

“Kwa bahati mbaya, imekuwa kawaida kuona lugha ya imani ikiburuzwa katika mapambano ya kisiasa, kubariki utaifa na kuhalalisha vurugu na mapambano ya silaha kwa jina la dini,” alisema Papa Leo.

Alisema wapo baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa wakiitumia kama daraja la kuchochea chuki kwa waumini, huku wao wakitafsiri matukio hayo kama uzalendo, jambo ambalo amelikemea.

Kutokana na hali hiyo, alisisitiza waumini wanapaswa kupinga mwenendo huo kwa vitendo na maisha yao ya kila siku.

“Waumini lazima wapinge kikamilifu, hasa kwa ushuhuda wa maisha yao, aina hizi za kufuru zinazolivunjia heshima jina takatifu la Mungu,” aliongeza.

Katika ujumbe huo wa kurasa nne unaotolewa kila mwaka, Papa Leo, pia alilalamikia ongezeko la matumizi ya kijeshi duniani, akinukuu takwimu za Taasisi ya Stockholm ya Utafiti wa Amani (SIPRI) zinazoonesha matumizi hayo yaliongezeka asilimia 9.4 mwaka 2024 na kufikia jumla ya dola za Marekani trilioni 2.7, sawa na asilimia 2.5 ya Pato la Taifa la Dunia (GDP).

Papa Leo aliyechaguliwa Mei, mwaka huu, baada ya Papa Francis kufariki dunia, aliendelea kuonya juu ya hatari za kutumia dini kama chombo cha kuhalalisha vurugu.

Katika safari yake ya kwanza nje ya nchi kama Papa, aliyoifanya nchini Uturuki mwezi uliopita, aliwaambia viongozi wa Kikristo Mashariki ya Kati lazima wakatae kwa nguvu matumizi ya dini kuhalalisha vita au aina yoyote ya misimamo mikali.

Previous Post

YANGA, MAYO USO KWA USO

Next Post

NEEMA LUKUKI BANDARI KILWA

Next Post
NEEMA LUKUKI BANDARI KILWA

NEEMA LUKUKI BANDARI KILWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MBAPPE AMFIKIA HENRY UFARANSA

MBAPPE AMFIKIA HENRY UFARANSA

11 months ago
WAZIRI MKUU : SERIKALI KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

WAZIRI MKUU : SERIKALI KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

4 weeks ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?