• ePaper
Tuesday, July 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU : SERIKALI KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 1, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU : SERIKALI KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeweka mkakati wa kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na miradi inakamilika kwa wakati.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sokoine, wilayani Serengeti, mkoani Mara, Waziri Mkuu amesema Serikali imeanza rasmi utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030, Bajeti ya Serikali ya mwaka 2026/2027 pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

 “Tunaanza utekelezaji wa Ilani leo, Ilani ya 2025–2030. Tunaanza utekelezaji wa Bajeti leo ya mwaka 2026/2027, na tunaanza utekelezaji wa Dira mpya ya 2050 leo.”

Waziri Mkuu amesema baadhi ya miradi ya maendeleo ilichelewa kuanza au kupungua kasi ya utekelezaji kutokana na uamuzi wa kimkakati wa Serikali wa kuelekeza rasilimali katika kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, Daraja la JPM na Reli ya Kisasa (SGR), ambayo sasa imeanza kuwanufaisha Watanzania.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya barabara, Waziri Mkuu alsema Serikali imeweka utaratibu mpya utakaohakikisha fedha za Mfuko wa Barabara zinawafikia watekelezaji moja kwa moja ili kuondoa ucheleweshaji wa miradi.

 “Kuanzia leo tarehe moja, fedha zitakazokusanywa zinazotakiwa kwenda kwenye ujenzi wa barabara, zikishakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, hazitapelekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Zitakwenda moja kwa moja kwenye Mfuko wa Barabara ili kasi ya ujenzi wa barabara isiende kwa kusuasua.”

Alisema hatua hiyo itawawezesha wakandarasi waliokuwa wamesimama kurejea katika maeneo ya kazi na kuharakisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Mkoa wa Mara.

 “Nimewaelekeza wakandarasi ambao walishatoka site warudi site, kwa sababu kuanzia leo tarehe moja Mfuko wetu wa Barabara… fedha zitakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ili wananchi wapate maendeleo yanayochochewa na miundombinu hiyo wezeshi.”

Aidha, Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa ahadi zote zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 “Yale ambayo Mheshimiwa Rais aliwaahidi, amenituma niwahakikishie kuwa yatatekelezwa. Na mimi, kama wajibu niliopewa na Katiba, nitasimamia kuhakikisha maelekezo hayo ya Mheshimiwa Rais yanatekelezwa.”

Previous Post

MAFANIKIO TRA USIPIME KABISA

Next Post

TUTUMIE AFCON KAMA FURSA YA KUJITANGAZA KIMATAIFA – DK. YONAZI

Next Post
TUTUMIE AFCON KAMA FURSA YA KUJITANGAZA KIMATAIFA – DK. YONAZI

TUTUMIE AFCON KAMA FURSA YA KUJITANGAZA KIMATAIFA - DK. YONAZI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

HESHIMA KUBWA KWA TANZANIA

1 month ago
RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA WABUNGE

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA WABUNGE

3 months ago

Popular News

  • CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

    CHINA YAZIDI KUSISITIZA USHIRIKIANO KWA AFRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, SINGIDA BS MACHO ‘KAGAME CUP’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI : TAMKO LA PAMOJA CCM NA ACT-WAZALENDO LAFUNGUA NJIA YA UTEKELEZAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BIL.8/- KUISUKA AZAM FC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WADAU WAMGOMEA SAMATTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?