• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. NCHIMBI ATAJA FAIDA UKARABATI RELI TAZARA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 21, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
DK. NCHIMBI ATAJA FAIDA UKARABATI RELI TAZARA

MAKAMU wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU,
Lusaka

MAKAMU wa Rais, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema ukarabati wa Reli ya TAZARA, utachochea biashara kati Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Bara la Afrika kwa ujumla.

Pia, amesema kuwa, ukarabati huo, utaongeza mauzo ya bidhaa nje na ndani ya Zambia na Tanzania.

Dk. Nchimbi, alisema hayo alipomwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la uzinduzi wa ukarabati mkubwa wa Reli ya TAZARA, uliyofanyika, jijini Lusaka nchini Zambia.

Alieleza kuwa, ukarabati huo, utaongeza mauzo ya bidhaa nje na ndani ya Zambia na Tanzania, kukuza kilimo, madini, viwanda, utalii na kutengeneza ajira zaidi kwa wananchi wa ukanda huo.

Alilisisitiza kuwa, wakati Reli ya TAZARA ikizidi kuimarishwa, Tanzania inafanya uboreshaji mkubwa wa bandari, ikiwa ni pamoja na kutekeleza dhamira ya Rais Dk. Samia ya kuongeza ukubwa wa Bandari ya Dar es Salaam kwa magati mapya, kuboresha ufanisi na kuhakikisha muunganiko mzuri wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) na TAZARA.

Aliongeza kwamba, Tanzania itaendelea kuboresha bandari za Tanga, Mtwara na Bagamoyo kuhakikisha kunakuwa na ubora wa kimataifa wa usafirishaji kwa nchi za Zambia, SADC na Afrika kwa ujumla.

Aidha, Makamu wa Rais, alisema ukarabati huo, unafanyika wakati ambao China inaendelea kuwa mdau muhimu katika ukuaji wa uchumi wa kimataifa, chini ya mpango wake wa maendeleo wa 15 wa miaka mitano.

Alisema hatua hiyo, inaifanya China kuwa mshirika muhimu wa maendeleo kwa reli hiyo na nchi hizo kwa ujumla.

Makamu wa Rais, alisema historia inafundisha ukweli wenye nguvu kwamba, Tanzania, Zambia na China zinaposimama pamoja, hakuna changamoto kubwa.

Kwa mujibu wa Dk. Nchimbi, ikiwa waasisi wa nchi hizo, walifanikiwa kujenga Reli ya Uhuru, kwa sasa kwa kuzingatia uwezo wa nchi hizo, zitaweza kukarabati Reli ya TAZARA na kuifanya kuwa mfano wa ushirikiano wa karne ya 21.

Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), ni mojawapo ya alama muhimu za urafiki, ushirikiano na matarajio ya pamoja kati ya Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China.

Reli hiyo yenye urefu wa kilometa 1,860 ikiwa na kilometa 975 kwa Tanzania na kilometa 885 nchini Zambia, inaunganisha Bandari ya Dar es Salaam na Kapiri-Mposhi mpya, kwa kutumia mfumo wa Cape Gauge (milimita 1,067).

Uwekezaji katika ukarabati huo, utafanya uboreshaji mkubwa, ukiwemo wa njia ya reli, stesheni, mifumo ya mawasiliano na ununuzi wa treni 34, mabehewa 760, makochi 18 na treni mbili kwa huduma za abiria.

Ufufuaji huo, unalenga kuongeza usafirishaji wa mizigo hadi kufikia tani milioni 2.4 ifikapo mwaka wa tatu wa uendeshaji.

Ukarabati mkubwa wa Reli ya TAZARA, ni hatua muhimu katika historia ya miundombinu ya Reli ya Tanzania na Zambia.

Aidha, ukarabati huo, unatajwa kuwa fursa, ukiweka reli kama njia muhimu ya kikanda, ambayo itachochea uwekezaji, biashara, kupunguza gharama za usafirishaji na kukuza ushirikiano wa kikanda.

Mbali ya hayo, mradi huo ni msingi katika kuimarisha uhusiano kati ya China, Tanzania na Zambia, huku ukiimarisha uhusiano kati ya SADC na EAC.

Hafla hiyo, ilihudhuriwa na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Qiang.

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais Dk. Nchimbi, amliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Godius Kahyarara, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Salum na wataalamu mbalimbali serikalini.

Previous Post

WADAU WAMPA TANO RAIS SAMIA TUZO ZA CAF 2025

Next Post

NJOONI MUONE SHOO

Next Post
NJOONI MUONE SHOO

NJOONI MUONE SHOO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA UBABE UBABE

YANGA UBABE UBABE

2 days ago
KISHINDO CHA DK. NCHIMBI RUVUMA

KISHINDO CHA DK. NCHIMBI RUVUMA

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?