• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SERIKALI YAFUNGUA MILANGO KWA WADAU AFCON 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 12, 2026
in Burudani, Habari, Kimataifa, Kitaifa, Michezo
0
SERIKALI YAFUNGUA MILANGO KWA WADAU AFCON 2027
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA 

SERIKALI imeendelea kuonesha dhamira yake ya dhati katika kuhakikisha mashindano ya AFCON 2027 yanafanyika kwa mafanikio makubwa, baada ya kueleza milango ipo wazi kupokea maoni.

Hatua hiyo, imekuja baada ya serikali kulipa ada ya ushiriki ya shilingi bilioni 76, hatua inayodhihirisha uzito wa maandalizi hayo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, katika mkutano na wadau wa michezo, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alisema wizara ipo tayari kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mashindano hayo yanaacha historia chanya na yenye mafanikio makubwa kwa nchi.

“Milango ipo wazi kwa kila mtu kutoa mawazo yake. Kila mmoja anapaswa kutumia nafasi aliyonayo kuchangia mafanikio ya AFCON 2027. Lengo letu ni kuona Tanzania ikiweka rekodi nzuri na kujivunia mafanikio haya,” alisema.

Katibu huyo alifafanua kuwa mashindano ya AFCON 2027 yanatarajiwa kuwa chachu ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo utalii, biashara na ajira.

“Hii ni fursa kwa Tanzania kuonesha utamaduni wake na ukarimu kwa wageni watakaokuja kutoka sehemu mbalimbali za dunia,”alisema Katibu huyo.

Msigwa aliwaomba Watanzania kuchangamkia fursa hiyo kwa ubunifu na uzalishaji wa bidhaa na huduma zitakazowapa furaha na kumbukumbu nzuri wageni watakaotembelea nchi wakati wa mashindano hayo.

“Tunawahimiza Watanzania kutumia nafasi hii vizuri kwa kubuni na kuandaa vitu vitakavyowavutia wageni wetu. Hii ni fursa ya kipekee kwa taifa kujitangaza kimataifa,” alisema.

Katibu huyo aliongeza kuwa serikali imeendelea kuonesha dhamira yake ya dhati katika kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa mafanikio makubwa.

“Baada ya kuwekeza fedha nyingi katika maandalizi ya tukio hilo kubwa la kimataifa, bado Watanzania wanatakiwa kuitumia vizuri kukuza uchumi wao na nchi kwa ujumla,” alisema.

Msigwa  alisema kuwa serikali tayari imelipa ada ya ushiriki ya shilingi bilioni 76, hatua inayodhihirisha uzito wa maandalizi hayo.

Alisema  kuwa uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati  kuhakikisha Tanzania inaandaa mashindano ya kiwango cha juu yatakayovutia wageni kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika na duniani kwa ujumla.

“Serikali imejipanga na imetoa fedha nyingi kuhakakikisha mashindano haya yanafanyika kwa kiwango kikubwa, pia imelipa ada ya ushiriki shilingi bilioni 76, “alisema.

Previous Post

UMUHIMU KUNYWA MAJI HUU HAPA

Next Post

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

Next Post
MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

MWIGULU ASHUSHA PRESHA SAKATA KUPAA BEI MAFUTA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

WASIRA AONYA WANAOTOLEA MACHO UMEYA

7 months ago
RAIS DK. SAMIA AFUNGUA UCHUMI WA KIDIJITALI

RAIS DK. SAMIA AFUNGUA UCHUMI WA KIDIJITALI

5 days ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?