• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI AWAPA SALAMU WATAKAOHUJUMU MIRADI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIHONGOSI AWAPA SALAMU WATAKAOHUJUMU MIRADI
0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesisitiza Chama hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mtumishi yeyote wa umma atakayehujumu au kuchezea miradi ya maendeleo.

Kauli hiyo aliitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Nsimbo, ambapo pia alisikiliza changamoto za wananchi na kuzitatua.

Alisema CCM ina wajibu wa kufuatilia utekelezaji wa miradi iliyomo katika Ilani ya Uchaguzi na kulifananisha jukumu hilo na mwenye duka anayekwenda kukagua biashara yake.

“Sisi ndiyo wenye serikali, lazima tufuatilie miradi yetu. Hatutacheka na yeyote. Mtumishi wa umma atakayejaribu kuchezea miradi ya wananchi tutamchukulia hatua,” alisema.

Akizungumzia miundombinu ya barabara, Kihongosi alisema Mkoa wa Kigoma umepiga hatua kubwa katika sekta ya miundombinu na kuutaja ujenzi wa barabara za lami zinazounganisha wilaya ni utekelezaji wa ahadi za CCM.

Alikumbusha zamani safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma kupitia Tabora ilikuwa ya vumbi na usumbufu mkubwa, sasa hali imebadilika kiasi kikubwa.

Kuhusu gridi ya taifa, Kihongosi alisema mwaka 2022 mkoa wa Kigoma, uliunganishwa rasmi katika gridi ya taifa chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, hatua aliyoondoa utegemezi wa majenereta na kupatikana umeme wa uhakika kwa wananchi na wawekezaji.

Aliongeza CCM itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo kuhakikisha wananchi wanapata thamani ya kodi zao na ahadi zilizotolewa zinatimizwa kwa vitendo.

Hata hivyo, alisema Chama kipo makini katika kusimamia rasilimali na maendeleo ya taifa.

Previous Post

KARDINALI PENGO AACHA SIMANZI

Next Post

SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

Next Post
SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UNDANI WA KUNDI LA STARS AFCON 2025

UNDANI WA KUNDI LA STARS AFCON 2025

7 months ago
YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

4 weeks ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?