• ePaper
Tuesday, September 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 24, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

WAKATI Simba ikipiga vyema hesabu zake kuvuna pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji kesho, Yanga imepania kuendeleza kasi ya ushindi katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutetea taji hilo.

Timu hizo zimetoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti juzi baada ya kila moja kuvuna pointi tatu.

Simba inayonolewa na Steven Barker ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati Yanga ikishinda 1-0 dhidi ya Namungo katika Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Kila moja ikicheza mechi tisa msimu huu, Simba imeibuka na ushindi mara saba, sare moja na kupoteza mechi moja wakati Yanga ikishinda mechi nane na kutoka sare mara moja.

Kesho, Wekundu hao wa Msimbazi watachuana na Dodoma Jiji katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati Yanga ikivaana na JKT Tanzania katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Kocha wa Simba, Barker, alisema hivi sasa wameelekeza nguvu na akili katika mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji.

Barker alisema ataiandaa vyema timu yake kwa mchezo huo kuendelea kuvuna alama tatu.

“Tumeshamaliza mchezo na Tanzania Prisons, hivi sasa tunajipanga kwa mechi na Dodoma Jiji, tunarudi uwanja wa mazoezi kufanya mazoezi kuhakikisha tunakuwa bora,” alisema.

Barker raia wa Afrika Kusini, alifurahia kikosi chake kuonyesha kiwango bora katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

“Ninawapongeza mashabiki kwa kujitokeza uwanjani na kusapoti timu yao kwani ujio wao umewapa nguvu wachezaji kupambana hadi kufanya vizuri na kuondoka na pointi tatu,” alisema.

Naye nyota wa Yanga, Dickson Job, alisema kila mchezaji anajua umuhimu wa kutetea taji hivyo watapambana katika kila mechi kuhakikisha wanatimiza adhma hiyo.

“Sisi kama wachezaji tunaahidi tutapambana katika michezo iliyobaki kwani tunahitaji kutetea ubingwa, kikubwa mashabiki waendelee kutusapoti,” alisema.

Job aliwashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani hatua ambayo imekuwa ikiipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri.

Job alidai kuwa, hivi sasa akili na nguvu zao wamezielekeza katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Previous Post

KIHONGOSI AWAPA SALAMU WATAKAOHUJUMU MIRADI

Next Post

SHULE YA BILIONI 1.23/- YAMKOSHA MWIGULU

Next Post
SHULE YA BILIONI 1.23/- YAMKOSHA MWIGULU

SHULE YA BILIONI 1.23/- YAMKOSHA MWIGULU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

TUSHEREHEKEE EID KWA UTULIVU, AMANI

6 months ago
KUVUMILIANA MUHIMU

KUVUMILIANA MUHIMU

5 months ago

Popular News

  • SIMBA HII GUSA UNASE CAFCL

    SIMBA HII GUSA UNASE CAFCL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UNDANI UGONJWA WA FIGO NA MATIBABU YAKE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?