• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SHULE YA BILIONI 1.23/- YAMKOSHA MWIGULU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 24, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SHULE YA BILIONI 1.23/- YAMKOSHA MWIGULU
0
SHARES
14
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, amesema ameridishwa na ujenzi wa shule mpya ya bweni, Sekondari ya Sinya.

Shule hiyo iliyojengwa katika Kijiji cha Leremeta, wilayani Longido, Mkoa wa Arusha, imegharimu sh. bilioni 1.23.

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Sinya na viongozi mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Dk. Mwigulu, alielekeza ujenzi wa uzio wa shule, ufanyiwe kazi haraka kutokana uwepo wa wanyama wakali.

“Nimeridhishwa na ujenzi wa hii shule; taarifa nilizonazo zinaonesha ujenzi wake, umezingatia thamani halisi ya fedha kwa ubora. 

“Ombi la kuwekwa uzio hapa shuleni ni jambo la maana kwa sababu, kuna wanyama wakali. “Mkurugenzi angalia ndani ya mapato ya halmashauri, mnaweza kupata kiasi gani ili kazi hiyo ifanywe haraka. Mkuu wa Mkoa (Amos Makalla), simamia jambo hili, liwe moja ya kipaumbele.

“Nyumba za walimu kama alivyoomba mkuu wa shule, Naibu Waziri wa TAMISEMI, kaa nao muangalie uwezekano. Na mabweni yaliyoombwa ni muhimu yajengwe,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Awali, akitoa taarifa ya ujenzi, Mkuu wa Shule hiyo, Andrew Emmanuel, alisema shule hiyo ina wanafunzi 387 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu na walimu 12, ambao kati yao, tisa wanaume na watatu wanawake.

Alisema bweni la wanafunzi wa kike limekamilika, linatumika na aliomba mabweni zaidi na nyumba za walimu kwa kuwa iliyopo ni moja inayoweza kutumika kwa familia mbili. Alisema nguvu ya wananchi sh. milioni 34, ilitumika kununua meza 140 na vitanda 80.

Katika hatua nyingine, Mwigulu alikagua ujenzi wa mradi wa majisafi wa Sinya–Namanga ambao pia unatekelezwa katika Kijiji cha Sinya, wilayani Longido, mkoani Arusha kwa gharama ya sh. bilioni 13.5.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisema kupatikana maji katika eneo hilo, kulitokana na uwepo wa mitambo ya kupimia maji chini ya ardhi, iliyonunuliwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambayo iligawanywa katika kanda tofauti.

“Wananchi wa huku walikuwa wanategemea chanzo cha Mto Simba ambacho hakitoshelezi, lakini utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) ulibaini eneo la Ildonyo (Sinya) linafaa kuwa na kisima chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.4 kwa siku,” alisema.

Waziri huyo, alisema uzalishaji wa sasa ni wastani wa lita milioni 1.7 kwa siku, wakati mahitaji ni lita milioni 3.8 na mradi ukikamilika utaongeza uzalishaji hadi lita milioni 4.1 kwa siku, hivyo kuboresha huduma ya maji safi kwa wananchi na mifugo.

Previous Post

SIMBA HESABU KALI, YANGA NI USHINDI TU

Next Post

SEKTA MADINI KUWA INJINI – MAVUNDE

Next Post
SEKTA MADINI KUWA INJINI – MAVUNDE

SEKTA MADINI KUWA INJINI - MAVUNDE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

AMANI NGUZO KUU YA USTAWI – RAIS DK. SAMIA

6 months ago
‘MOSHI MWEUPE’ WAFUKA UWANJA NDEGE MSALATO

‘MOSHI MWEUPE’ WAFUKA UWANJA NDEGE MSALATO

5 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?