• ePaper
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AIPAISHA TANZANIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 10, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AIPAISHA TANZANIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amezidi kuipaisha Tanzania, kwa  kuifanya  kivutio cha kimataifa cha uwekezaji katika sekta ya madini, baada ya kuorodheshwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza barani Afrika, kwa mujibu wa ripoti ya Fraser Institute (Annual Survey of Mining Companies 2025).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Tanzania imeshika  nafasi ya 34 kati ya maeneo 68 duniani yaliyotathminiwa katika Investment Attractiveness Index (IAI), kielelezo kinachotumiwa na wawekezaji na kampuni za utafiti wa madini kuamua wapi waelekeze mitaji ya utafiti na maendeleo ya miradi. 

Katika muktadha wa Afrika, Tanzania imeendelea kushika nafasi ya juu kwa kuwa ya nne barani Afrika katika IAI, ikifuatiwa na Botswana, Morocco na Zambia, hatua inayothibitisha ushindani wa Tanzania katika kuvutia mitaji ya kimataifa ya utafiti na uwekezaji wa madini. 

Ripoti hiyo inaonesha pia mwenendo chanya wa kupanda kwa alama za Tanzania, ambapo alama ya IAI imefikia 68.04 mwaka 2025, ikilinganishwa na 62.75 mwaka 2024 na 46.38 mwaka 2023 mwenendo unaoashiria kuongezeka kwa uaminifu na mvuto wa Tanzania kwa wawekezaji wa sekta ya madini. 

Kwa maelezo ya ripoti, IAI hujengwa kwa kuzingatia vipengele viwili vikuu vinavyoongoza maamuzi ya uwekezaji: uwezo wa kijiolojia wa rasilimali (mineral potential) na mazingira ya jumla ya kufanya biashara kwenye sekta husika.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa katika hesabu yake, asilimia 60 ya uzito huenda katima madini ya kimkakati  na asilimia 40 huenda katika mifumo ya kisera,  kutoa taswira ya mvuto wa eneo husika kwa uwekezaji wa utafiti na uchimbaji.

Katika kipengele cha Best Practices Mineral Potential Index, kinachoangalia mvuto wa kijiolojia kama eneo lingekuwa na kanuni bora zaidi duniani; Tanzania imeorodheshwa nafasi ya 15 duniani kwa alama 75.00, jambo linaloonesha kwa uwazi ukubwa wa fursa na uwezo wa rasilimali madini zilizopo nchini. 

Utafiti huo wa Fraser Institute ni miongoni mwa rejea muhimu zinazotumiwa kimataifa na sekta binafsi, taasisi za utafiti na wadau mbalimbali kutathmini mwenendo wa masoko ya uwekezaji wa madini.

Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti, dodoso lilipelekwa kwa viongozi na wataalam 2,304 wa kampuni za utafiti na uchimbaji, na waliotoa majibu waliripoti matumizi ya pamoja ya takribani Dola za Marekani bilioni 4.2 katika shughuli za utafiti wa madini mwaka 2025. 

Kwa Tanzania, nafasi hiyo inaongeza msukumo katika  jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha sekta ya madini kama nguzo muhimu ya uchumi, ikiwemo kuongeza utafiti, kuvutia mitaji mikubwa ya uendelezaji wa miradi, na kukuza ushiriki wa Watanzania katika mnyororo mzima wa thamani wa madini. 

Wataalamu wa uchumi na wadau wa sekta ya madini nchini wamempongeza Rais Dk. Samia kwa kuvutia uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini nchini, huku wengi wakibashiri  sekta hiyo kuwa nguzo kuu ya uchumi wa Tanzania kwa miaka michache ijayo.

Previous Post

WAZIRI MKUU AWAPA ‘TANO’ WANAOCHAPAKAZI SERIKALINI

Next Post

SERIKALI KUHARAKISHA MABADILIKO KIDIJITALI

Next Post
SERIKALI KUHARAKISHA MABADILIKO KIDIJITALI

SERIKALI KUHARAKISHA MABADILIKO KIDIJITALI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI MATUMAINI KIBAO AFCON

SERIKALI MATUMAINI KIBAO AFCON

4 months ago
DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

2 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?