• ePaper
Monday, October 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

YAFUNGUA FURSA KWA KAYA MASKINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
YAFUNGUA FURSA KWA KAYA MASKINI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu, Ilemela

MRADI wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza, umeendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa kaya zenye kipato duni, kuwaongezea kipato walengwa na kuwasaidia kujikwamua dhidi ya umaskini.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Kaimu Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, David Macha, amesema umetokana na vikundi vya akinamama wanufaika wa mfuko huo waliobuni wazo la kufuga samaki kwa njia ya vizimba.

Macha amesema kinamama hao walitambua kuwa, kuishi karibu na Ziwa Victoria ni fursa muhimu inayoweza kutumika kuwaongezea kipato iwapo wanaitumia ipasavyo kupitia ufugaji samaki.

Amesema vikundi vya kinamama vilipatiwa mkopo kupitia TASAF; ambao katika awamu ya kwanza, vilikopeshwa sh. milioni 34, fedha ambazo zilitumika kutengeneza vizimba viwili, kununua vifaranga vya samaki na chakula kuendesha shughuli za ufugaji.

Macha amefafanua kuwa, baada ya kuanza ufugaji, vikundi hivyo vilivuna samaki na kupata sh. milioni 27, ambazo ziliwapa motisha ya kuendelea na mradi huo kujiongeza kipato na kuimarisha shughuli za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Macha, baada ya mavuno, wanachama waliamua kuendeleza uwekezaji huo kwa kutumia sehemu ya fedha zilizopatikana, huku kiasi kingine kikitumika kusaidia shughuli nyingine za wanachama, ikiwemo kukopeshana kukidhi mengine ya kijamii.

“Ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ni fursa inayoweza kusaidia kuongeza upatikanaji wa samaki, katika mazingira ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa samaki, huku ukiwawezesha walengwa kujenga msingi wa kujitegemea kiuchumi,” alisema.

MNUFAIKA

Mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF, Modesta Makonya, amesema mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba umemsaidia kuboresha maisha yake na familia, ikiwemo kipato na kujenga nyumba.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Modesta, amesema akiwa na kinamama wenzake walifikiria shughuli mbadala za kiuchumi; baada ya mwaka 2024 kuelekezwa kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini katika awamu waliyokuwa wananufaika nayo ungefikia mwisho.

Modesta amesema walikaa na kuanzisha kikundi cha wanawake, ambacho baadaye kilipata msaada wa serikali kupitia TASAF, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambao walipatiwa sh. milioni 34 zilizowawezesha kuanzisha mradi wa ufugaji samaki kwa njia ya vizimba.

“Baada ya kupata fedha hizo, tuliweka vizimba viwili, kila kimoja kikiwa na samaki 650. Tulifanya shughuli za ufugaji na tulipofikia wakati wa kuvuna, tulifanikiwa kupata takribani shilingi milioni 29, jambo lililotupa moyo wa kuendelea na mradi huo,” amesema.

AWAMU YA PILI

Amesema mafanikio ya mavuno ya kwanza yaliwafanya waendelee na awamu ya pili ya ufugaji, ambao walitumia sh. milioni 22.4, kwa mahitaji mbalimbali ya mradi huku wakiendelea na maandalizi ya kuongeza uzalishaji kupata mapato makubwa zaidi kwa mavuno yajayo.

Makonya amesema pamoja na mafanikio hayo, mradi huo unakabiliwa na changamoto za kimazingira, yakiwemo magugu maji yanayoathiri shughuli za ufugaji, hivyo aliiomba serikali na wadau wengine kuendelea kuwaunga mkono kuimarisha mradi huo uwe na tija zaidi.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA KUZINDUA RASMI MJI WA SERIKALI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

AHMED ALLY NA KAMWE WANENA

AHMED ALLY NA KAMWE WANENA

9 months ago
DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

DK. MWIGULU ATOA MAAGIZO AFCON 2027

8 months ago

Popular News

  • YAFUNGUA FURSA KWA KAYA MASKINI

    YAFUNGUA FURSA KWA KAYA MASKINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA KUZINDUA RASMI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATANZANIA WAHAMASISHWA KUPIMA SARATANI YA MATITI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TRC YAMKOSHA PROF. MBARAWA UBUNIFU  KIWANDA CHA MATARUMA YA ZEGE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. HOMERA AAGIZA UZINDUZI WA KAMPENI YA WASHA UMEME VITONGOJINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?