• ePaper
Wednesday, July 29, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TULIENI NYUMBANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 8, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa
0
TULIENI NYUMBANI

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba

0
SHARES
33
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

>>Ni agizo la Waziri Mkuu Dk. Mwigulu

>>Simbachawene  asema maandamano ni haramu

Na IRENE MWASOMOLA

SERIKALI imewataka wananchi wasiokuwa na ulazima wa kutoka leo, watulie nyumbani.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, alipowasilisha salamu za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru, ambapo aliwatakia Watanzania kheri.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Waziri Mkuu alisema wananchi wasiokuwa na dharula washerehekee sikukuu hiyo nyumbani, isipokuwa ambao majukumu yao yanawataka kuwepo vituo vya kazi kama ambavyo wataelekezwa na viongozi wao.

Serikali imesema imejipanga kikamilifu na ipo imara, kudhibiti maandamano yaliyopangwa kufanyika leo katika mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, alisema Serikali haitambui maandamano hayo kwa kuwa hayana kibali rasmi.

Simbachawene alisema maandamano hayo yaliyohamasishwa mtandaoni, yana lengo la kuleta uvunjifu wa amani na kuchafua taswira ya nchi.

Hata hivyo, alisema vyombo vya ulinzi vimejipanga kikamilifu kudhibiti aina yoyote ya uhalifu, utakaofanyika kwa kisingizio cha maandamano hayo.
Simbachawene alisema kufuatia hali hiyo, aliwataka wananchi wasiokuwa na ulazima wa kutoka leo, kutulia nyumbani na alitoa tahadhari kwamba yeyote atakayeshiriki maandamano hayo atakumbana na vyombo vya ulinzi.

Aidha, waziri huyo aliwasisitiza wananchi kuepuka kuchungulia nje, badala yake wabaki ndani kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza endapo maandamano hayo yatafanyika.

“Maandamano hayo ni haramu hayaruhusiwi, hayana kibali na yako kinyume cha sheria. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimejipanga kuyadhibiti.

“Kama hakuna ulazima sana wa wewe (mwananchi) kutoka kesho (leo) jizuie, kama hakuna ulazima kufanya ‘movement’ jizuie uangalie hali halisi inakwendaje,”alisema.

Alisema wanaohamasisha maandamano hayo na kudai ni ya amani hawajulikani, haifahamiki wataanzia wapi na yanalenga nini ingawa wanaoratibu wanaeleza yatakuwa makubwa kuliko yaliyotokea Oktoba 29, mwaka huu.

“Niwaombe wananchi wasithubutu kujitokeza, Oktoba 29 kuna wengine walijitokeza bila kujua wanachokimbilia ni kitu gani, walijikuta wamejiingiza katika jambo ambalo hawakulijua.

Tunaambiwa maandamano hayo ni makubwa kuliko yale ya Oktoba 29. Maandamano hayo ndiyo tuliyoshuhudia vituo vya mafuta vikichomwa, mali za watu zikiharibiwa, yale siyo maandamano ni mapinduzi,”alisema Simbachawene.

Waziri huyo aliwasihi wananchi kuendelea kuitunza tunu yta amani ambayo imedumu muda mrefu, hivyo aliitaka jamii kuimarisha umoja na mshikamano.

Desemba 2, mwaka huu akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, Rais Dk. Samia alisema kilichofanyika Oktoba 29, hayakua maandamano badala yake yalikuwa na dhamira ya kupindua serikali.

Rais Dk. Samia alisema vurugu hizo siyo desturi au utamaduni wa taifa letu na kwamba vurugu zilizofanyika ni mradi mpana wenye ufadhili unaolenga kuchafua taswira ya nchi.

Wakati huo huo, akizungumza utaratibu wa ukamataji raia unaofanywa na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi, waziri huyo alisema amemwelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura, utumike utaratibu uliozoeleka usioleta hofu au vitisho kwa wananchi.

“Ukamataji ninaopenda ni ule wa kisheria, askari anaenda na sare anaripoti kwa mjumbe, yanini uende usiku umevaa ninja,”alisema.

Waziri Simbachawene alisema hakuna sababu ya ukamataji unaoleta hofu kwa wananchi, isipokuwa pale itakapobidi ufanyike kulingana na kosa.

Maandamano hayo yanaratibiwa mitandaoni zikiwa zimepita siku 42 tangu kutokea vurugu na uharibifu wa mali uliyofanywa Oktoba 29.

Previous Post

RC MTAKA AWAPA SOMO LA AMANI VIJANA WA NJOMBE

Next Post

RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI

Next Post
RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI

RAIS DK. SAMIA, BALOZI WA MAREKANI WAJADILI MIRADI YA KIMKAKATI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DRC WAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUTOA HIFADHI YA WAKIMBIZI

DRC WAISHUKURU SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUTOA HIFADHI YA WAKIMBIZI

7 months ago
DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA TANGA AKIPEWA RIDHAA YA KUONGOZA NCHINI

10 months ago

Popular News

  • MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAJA SIFA ZA MAWASILIANO SERIKALINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • 50 BORA ‘FORM SIX’ KUSOMA AI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2/- YAKAMATWA IKITOROSHWA DAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATAKA UADILIFU, USHIRIKIANO NA MATOKEO KWA VIONGOZI WAPYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?