• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 2, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
TANZANIA NA GHANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KIUCHUMI NA AJIRA KWA VIJANA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, leo amefanya mazungumzo ya pande mbili na Rais wa Jamhuri ya Ghana, John Dramani Mahama, Ikulu Ndogo Arusha.

Mazungumzo yao yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Ghana, hususan katika mageuzi ya kiuchumi, ajira kwa vijana na maendeleo ya uchumi wa kidijitali.

Viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuongeza thamani ya rasilimali za ndani badala ya kuendelea kuuza malighafi. Rais Mahama ameeleza hatua zinazochukuliwa na Ghana katika kuimarisha usimamizi wa sekta ya madini na kakao, kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani na kukuza uchakataji wa ndani.

Kwa upande wake, Rais Dk. Samia amesema Tanzania inaendelea kuharakisha mkakati wa uchumi wa viwanda, ikiwemo kuongeza thamani ya mazao ya kimkakati kama pamba na kuimarisha uchakataji wa madini, na kuongeza kuwa Tanzania ina nafasi muhimu ya kujifunza kutoka Ghana katika usimamizi wa rasilimali na sera za uchumi wa ndani.

Kuhusu suala la ajira kwa vijana, marais hao wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika maendeleo ya ujuzi, ubunifu na ujasiriamali, na kusisitiza umuhimu wa kuweka mazingira bora ya uwekezaji yatakayozalisha ajira endelevu kwa vijana wa pande zote mbili.

Katika eneo la uchumi, Rais Dk. Samia amesisitiza dhamira ya Tanzania ya kuimarisha mifumo ya fedha za kidijitali na usalama wa mitandao kama sehemu ya mkakati wa kujenga uchumi shindani na jumuishi.

Amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya TEHAMA na kukuza ubunifu wa vijana, huku akieleza kuwa uzoefu wa Ghana katika sekta ya teknolojia ya fedha na ulinzi wa miundombinu ya kimtandao ni eneo muhimu la kujifunza na kushirikiana ili kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na ufanisi wa huduma za kifedha nchini.

Halikadhalika, Viongozi hao wamepongeza hatua ya kuimarisha usafiri wa anga wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) kati ya Tanzania na Ghana, wakisema kuwa hatua hiyo itarahisisha biashara, utalii na mwingiliano wa watu kati ya nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa safari hizo za moja kwa moja zitachochea biashara sio tu ya Tanzania na Ghana, bali pia ndani ya Bara la Afrika.

Rais wa Ghana yupo chini kwa ziara ya kikazi ya siku moja. leo Machi 02, 2026 anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama, na Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, yenye makao yake makuu jijini Arusha.

Previous Post

GAMONDI MATUMAINI KIBAO AFCON 2027

Next Post

NHIF YATOA FARAJA KWA WAFUNGWA GEREZA LA ISANGA, DODOMA

Next Post
NHIF YATOA FARAJA KWA WAFUNGWA GEREZA LA ISANGA, DODOMA

NHIF YATOA FARAJA KWA WAFUNGWA GEREZA LA ISANGA, DODOMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU HAPOI

DK. MWIGULU HAPOI

3 months ago
RC MAKALLA  AKAGUA UJENZI UWANJA WA  AFCON ARUSHA

RC MAKALLA AKAGUA UJENZI UWANJA WA AFCON ARUSHA

6 months ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?