• ePaper
Tuesday, October 13, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU, Dodoma

NAIBU Katibu Mtendaji wa Menejimenti ya Utendaji na Tathmini Tume ya Taifa ya Mipango, Sosthenes Kewe, amesema ni umuhimu kwa miradi ya umwagiliaji kuwa na matokeo yanayoonekana kwa jamii na kuzingatia vipaumbele vya taifa.

Kewe alisema hayo katika kikao baina ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na Tume ya Taifa ya Mipango.

Kikao hicho kililenga kujadili namna bora ya kuoanisha mipango, miradi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa nia ya kuongeza tija kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Alieleza ni muhimu taasisi zote kuhakikisha miradi yao inaendana na mipango ya maendeleo ya muda mfupi na mrefu, huku ikionesha uwajibikaji na kuinua uchumi wa wananchi

“Tunapaswa kuzingatia miradi yenye matokeo zaidi kwa jamii, inayotanguliza vipaumbele vya taifa na kuonesha matokeo halisi yanayoboresha maisha ya Watanzania,” alisisitiza.

Alisema, sekta ya umwagiliaji ni kubwa kufikia malengo ya maendeleo ya kitaifa hivyo ni muhimu kazi zinazotekelezwa na NIRC na uwekezaji unaoenelea uendane na mipango ya nchi kwa kuzingatia malengo ya kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na uratibu madhubuti kati ya taasisi hizo ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta matokeo chanya.

“Ni muhimu tuanze pamoja ili kuhakikisha yale tunayoyafanya yanaendana na mipango ya nchi. Pale tunapokwenda vizuri tuendelee, lakini pia turekebishane mapema ili kuepuka upotevu wa rasilimali za serikali na kuongeza ufanisi katika utekelezaji,” alisema.

Kikao hicho pia kililenga kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa mipango ya maendeleo, ikiwemo uingizaji wa miradi kwenye mifumo rasmi ya ufuatiliaji na tathmini, kuongeza ubora wa taarifa za utekelezaji na kuhakikisha upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazosaidia kuvutia uwekezaji na kuonesha mchango wa sekta ya umwagiliaji katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Aidha, majadiliano hayo yanathibitisha dhamira ya serikali ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi zake, kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi zaidi kuleta matokeo chanya, ya kudumu kwa jamii na kukuza uchumi wa nchi.

Previous Post

MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

Next Post

NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

Next Post
NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

HAPATOSHI ‘KNOCKOUT YA MAMA’ KIJITONYAMA

HAPATOSHI ‘KNOCKOUT YA MAMA’ KIJITONYAMA

10 months ago
4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

4 ZAONGOZA KWA UKAME WA MABAO LIGI KUU BARA

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

    RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HATIMAYE IMELIPA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA NJIA NYEUPE MISS GRAND 2026

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, YANGA ZAPIGWA ‘STOP’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?