• ePaper
Saturday, September 12, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 11, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO
0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Dodoma

NA WAANDISHI WETU

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuandika sura mpya ya maendeleo nchini, huku utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta mbalimbali ukibadili maisha ya wananchi na kuongeza fursa za kiuchumi.

Katika kipindi cha uongozi wake, Serikali imeelekeza nguvu katika sekta za maji, nishati, afya, elimu, kilimo, miundombinu, uwekezaji, viwanda, ajira na teknolojia, huku ikisisitiza kuwa maendeleo ya taifa yanapaswa kuonekana katika maisha halisi ya wananchi.

Hatua hiyo imeenda sambamba na uwekezaji mkubwa katika miradi ya maendeleo, maboresho ya huduma za kijamii na kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali.

MAJI YAWAFIKIA WANANCHI

Katika sekta ya maji, takwimu zinaonesha kuwa upatikanaji wa maji safi na salama vijijini umeongezeka kutoka asilimia 72.3 mwaka 2020 hadi asilimia 85.3 mwaka 2025.

Ongezeko hilo limeendelea kupunguza changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta maji, huku likitoa fursa zaidi kwa wanawake na watoto kutumia muda wao katika shughuli nyingine za uzalishaji na maendeleo.

Hatua hiyo pia imekuwa sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wengi zaidi, hususan katika maeneo ya vijijini.

UMEME WAFIKIA WANANCHI ZAIDI

Katika sekta ya nishati, Serikali imeongeza kasi ya usambazaji wa umeme ambapo upatikanaji wa huduma hiyo umefikia asilimia 86.2.

Aidha, uwezo wa Taifa kuzalisha umeme umeongezeka zaidi ya mara mbili, hatua inayolenga kuweka msingi imara wa uchumi unaotegemea uzalishaji, viwanda, biashara na matumizi ya teknolojia.

Kwa wananchi, kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme kumefungua fursa za biashara, uzalishaji na matumizi ya teknolojia katika maeneo mbalimbali.

Mustapha Hoza, mkazi wa Majengo jijini Dodoma, alisema umeme umebadili shughuli zao za kila siku na kuwa nyenzo muhimu ya uzalishaji mali.

“Umeme unapopatikana, siyo mwanga pekee unaopatikana, bali unaongeza nafasi ya kufanya biashara, kusoma, kutumia teknolojia na kuongeza kipato,” alisema.

USAFIRI, MIUNDOMBINU

Katika miundombinu, Serikali imeendelea kuwekeza katika barabara, madaraja, reli, viwanja vya ndege na miradi mingine ya kimkakati inayolenga kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa.

Moja ya viashiria vya hatua hiyo ni ongezeko la idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa treni ya SGR, kutoka takribani milioni 1.2 hadi milioni 4.1.

Ukuaji huo unaonesha kuongezeka kwa matumizi ya usafiri wa reli na umuhimu wake katika kurahisisha safari za wananchi, usafirishaji wa bidhaa na kuchochea shughuli za kiuchumi.

Kwa wakulima na wafanyabiashara, miundombinu bora ina maana ya kupunguza gharama za usafirishaji na kurahisisha upatikanaji wa masoko.

Ahmady Bulyo, mkulima katika Kijiji cha Kazura Mimba mkoani Kigoma, alisema barabara bora na usafiri wa uhakika vinaongeza uwezekano wa mazao kufika sokoni kwa wakati kama ilivyo sasa kwa mkoa wa Kigoma.

AFYA KARIBU NA WANANCHI

Sekta ya afya nayo imeendelea kupewa msukumo kupitia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya, ununuzi wa vifaa tiba na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Takwimu za mpango wa Taifa zinaonesha kuwa hatua zilizochukuliwa katika sekta hiyo zimechangia kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi, huku vifo vya uzazi vikifikia 104 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2022, chini ya lengo la 180 lililowekwa kwa mwaka 2025/26.

Kwa familia, maboresho hayo yana maana ya kupata huduma kwa wakati, hasa kwa wajawazito, watoto na wananchi wenye mahitaji mbalimbali ya matibabu.

Neema Songo, mkazi wa Chanika, alisema kusogezwa kwa huduma za afya karibu na wananchi kumepunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.

“Huduma ya afya inapokuwa karibu, mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata msaada mapema. Hili ni jambo linalogusa maisha ya watu moja kwa moja,” alisema.

ELIMU, UJUZI KWA VIJANA

Katika elimu, Serikali imeendelea kuongeza nafasi na miundombinu ya kujifunzia pamoja na kusisitiza elimu inayomwandaa kijana kushiriki katika uchumi wa Taifa.

Msisitizo katika elimu ya ufundi na mafunzo ya ujuzi unalenga kuwawezesha vijana kupata maarifa na stadi zitakazowawezesha kujiajiri na kuajiriwa.

Mwelekeo huo unakwenda sambamba na hitaji la Taifa la kuwa na nguvu kazi yenye ujuzi inayoweza kushiriki katika uzalishaji na kukabiliana na mahitaji ya uchumi wa kisasa.

KILIMO KINAPATA NGUVU

Kilimo kimeendelea kuwa nguzo muhimu ya uchumi wa Taifa, kikichangia asilimia 24.3 ya Pato la Taifa mwaka 2025 na kuwa chanzo cha ajira kwa zaidi ya nusu ya Watanzania.

Serikali imeendelea kuwekeza katika uzalishaji, umwagiliaji, pembejeo, masoko na kuongeza tija kwa wakulima ili sekta hiyo iwe chanzo kikubwa zaidi cha kipato na ajira.

Kwa wananchi wa vijijini, maendeleo ya kilimo yana maana pana kwa sababu yanaathiri moja kwa moja kipato cha familia, upatikanaji wa chakula, elimu ya watoto na uwezo wa kaya kumudu gharama za maisha.

Batenga Shaaban, mkazi wa Namanyere mkoani Rukwa, alisema uwekezaji katika kilimo na upatikanaji wa pembejeo, ikiwemo mbolea za ruzuku, umeongeza matumaini kwa wakulima.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Katika eneo la nishati safi ya kupikia, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi ambazo zimekuwa na athari kwa afya za wananchi na mazingira.

Takwimu zinaonesha kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yameongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 28.6 mwaka 2025.

Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kupunguza athari za kiafya na kimazingira zinazotokana na matumizi ya nishati zisizo safi, huku ikilenga kuwafikia wananchi wengi zaidi.

UCHUMI WAENDELEA KUKUA

Katika uchumi, Tanzania imeendelea kuonesha ukuaji licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia.

Uchumi wa Taifa ulikua kwa asilimia 5.9 mwaka 2025 na unatarajiwa kufikia asilimia 6.3 mwaka 2026.

Aidha, wastani wa Pato la Taifa kwa kila Mtanzania uliongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia Sh3,544,124 mwaka 2025 kutoka Sh3,299,637 mwaka 2024.

Ukuaji huo umeendelea kuambatana na ongezeko la shughuli za biashara, uwekezaji, ujenzi na sekta nyingine zinazochangia katika uchumi wa Taifa.

WASOMI WATOA TATHMINI

Mwanazuoni wa Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk. Conrad Masabo, ameeleza kuwa kipindi cha uongozi wa Rais Samia kimeibua matumaini miongoni mwa wananchi, akitaja pia hatua katika masuala ya uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, mwanazuoni wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Aurelia Kamuzora, ameeleza kuwa kipindi cha uongozi wa Rais Samia kimekuwa na mazingira mazuri ya kiuchumi, yakichochea biashara, mikopo na uwekezaji.

“Hatujawahi kupata Rais ambaye anasimamia vyema uchumi katika kipindi cha miaka minne kama huyu tuliye naye sasa,” alisema Profesa Kamuzora.

UWEKEZAJI, VIWANDA

Serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na uzalishaji kwa lengo la kuongeza shughuli za viwanda, biashara na huduma.

Sekta ya ujenzi ilichangia asilimia 11.9 ya Pato la Taifa mwaka 2025, huku uchimbaji madini na mawe ukichangia asilimia 10.3.

Hatua hiyo inaonesha nafasi ya sekta hizo katika kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza fursa za ajira na kuibua biashara kwa Watanzania.

TEKNOLOJIA YACHOCHEA UCHUMI

Mageuzi ya kidijitali nayo yamekuwa sehemu ya mwelekeo wa Serikali katika kurahisisha huduma na kuifanya Tanzania iendane na mahitaji ya uchumi wa kisasa.

Kuongezeka kwa matumizi ya intaneti na mifumo ya kidijitali kunatoa nafasi kwa wananchi kupata huduma, kufanya biashara na kuwasiliana kwa urahisi zaidi.

Wataalamu wameendelea kusisitiza umuhimu wa Tanzania kuwekeza katika teknolojia, utafiti, ubunifu na kuongeza ujuzi wa kidijitali kwa vijana ili waweze kunufaika na fursa zinazotokana na uchumi wa kidijitali.

WANANCHI WAZUNGUMZA

Kwa wananchi wengi, kipimo cha maendeleo siyo takwimu pekee, bali ni mabadiliko wanayoyaona katika maisha yao ya kila siku.

Mtafiti wa uchumi, Dk. Juma Mohammed, alisema maendeleo yanapaswa kupimwa kwa kuangalia namna huduma na fursa zinavyobadilisha maisha ya wananchi.

“Tunapozungumzia maendeleo, mwananchi anaangalia kama maji yanapatikana, kama mtoto anapata elimu, kama kuna huduma ya afya na kama anaweza kufanya biashara kwa urahisi,” alisema.

Alisema kasi ya utekelezaji wa miradi inapaswa kuendelea huku Serikali ikihakikisha miradi inayotekelezwa inakamilika kwa wakati na inakuwa na manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

“Tunatambua yaliyofanyika, lakini wananchi tunahitaji kasi hii iendelee ili fursa ziongezeke zaidi,” alisema.

DIRA 2050, HATUA MPYA

Mbali na mafanikio yaliyopatikana, Serikali imeanza hatua mpya ya kuweka msingi wa maendeleo ya muda mrefu kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Dira hiyo inalenga kubadili muundo wa uchumi na kuongeza kasi ya maendeleo huku ikisisitiza ukuaji jumuishi na endelevu.

Katika utekelezaji wake, Serikali imeweka mkazo katika uchumi imara na shindani, maendeleo ya watu, utawala bora, mazingira pamoja na vichocheo vya mageuzi kama nishati, miundombinu ya usafiri, utafiti na maendeleo na mageuzi ya kidijitali.

Katika taarifa ya Juni 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais–Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisema utekelezaji wa Dira ya 2050 unahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

“Utekelezaji wa Dira ya 2050 unahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi,” alisema Profesa Mkumbo.

SAMIA, KIONGOZI WA MATOKEO

Safari ya Serikali ya Awamu ya Sita imejikita katika utekelezaji wa miradi na programu zinazolenga kuleta matokeo yanayoweza kuonekana na kupimika katika maisha ya wananchi.

Maji yanapofika kijijini, mtoto anapokwenda shule, mama anapopata huduma ya afya karibu na nyumbani, mfanyabiashara anapopata umeme, mkulima anapofikisha mazao sokoni na msafiri anapotumia treni au barabara bora, hayo ndiyo matokeo yanayotoa maana halisi ya maendeleo.

Mbunge wa Kisarawe, Dk. Selemani Jafo, alisema maendeleo nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kutokana na juhudi zinazofanywa na Rais Samia katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Alisema kasi hiyo ni chachu ya kuhakikisha maendeleo yanakuwa sehemu ya maisha ya wananchi na kuwa ushahidi wa hatua zinazochukuliwa na Serikali.

Dk. Jafo alisema licha ya kumalizika kwa uchaguzi, Serikali haijasita kuendelea na utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali, jambo alilosema linaonesha dhamira ya Rais Samia ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi hadi mwaka 2030.

“Kwa hiyo kubwa tunamshukuru na tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa hii kazi kubwa na spidi kubwa tunaondoka nayo,” alisema Dk. Jafo.

Aidha, Dk. Jafo alisisitiza kuwa amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya Taifa, akiwataka Watanzania kwa pamoja kuilinda na kuidumisha ili kuwezesha nchi kufikia malengo yake ya maendeleo.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Neema Majule, alisema hatua ya Serikali ya kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwamo Mji wa Serikali Mtumba na Bwawa la Mwalimu Nyerere, ni ushahidi wa dhamira ya kuendeleza mipango iliyowekwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Majule alisema miradi hiyo ni alama ya maendeleo ambayo inaweka kihistoria kwa Tanzania.

Vilevile alisema uamuzi wa kuendelea na miradi iliyoanzishwa na viongozi waliotangulia unaonesha kuwa Serikali haijaweka pembeni mipango ya maendeleo, bali imeendelea kuijenga na kuikamilisha kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

“Ni jambo la kishujaa linaenda kufanyika na Rais Dk. Samia anaenda kutimiza lengo la watangulizi wake la kuifanya kuwa makao makuu ya nchi na Serikali,” alisema Majule.

Kwa upande wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Majule amesema kukamilishwa kwa miradi ya kimkakati ya aina hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha msingi wa maendeleo ya Taifa, hususan katika sekta zinazohitaji uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu.

Hivyo, a                    lisema juhudi hizo zinapaswa kuendelea kuungwa mkono na Watanzania kwa kuwa miradi mikubwa kama Mji wa Serikali Mtumba na Bwawa la Mwalimu Nyerere inaweka msingi wa maendeleo ya muda mrefu na kuacha alama itakayokumbukwa na vizazi vijavyo.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAMPENI ZA KUMNADI EMMANUELA ZINAVYOPAMBA MOTO ISMANI

KAMPENI ZA KUMNADI EMMANUELA ZINAVYOPAMBA MOTO ISMANI

4 months ago
JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

JKT YATAKATA LIGI KUU BARA

10 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

    RAIS DK. SAMIA NI KIONGOZI WA MATOKEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?