• ePaper
Wednesday, September 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 23, 2026
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kikiendelea na maandalizi ya mechi mbili za kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON 2027), wachezaji wa timu hiyo wameweka wazi kuwa wana morali ya kupambana mwanzo hadi mwisho kupata ushindi.

Taifa Stars itaanza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Guinea-Bissau utakaochezwa Septemba 25, mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan Complex, uliopo Zanzibar, kabla ya kuifuata Madagascar, Septemba 29, mwaka huu, mchezo utakaochezwa Casablanca nchini Morocco.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam, mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva, alisema wachezaji wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi.

Alisema timu yao haina sababu ya kutoa visingizio kwani inapaswa kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya AFCON 2027 kwani imesheheni wachezaji wenye uwezo mzuri.

Msuva alisema Taifa Stars imejengwa upya ikiwa na wachezaji vijana na imepata maandalizi muhimu, huku uzoefu walioupata nchini Morocco katika AFCON 2025 ni sehemu ya maandalizi makubwa kwao hatua inayofuata.

“Bado tuna nafasi ya kufanya makubwa katika mashindano haya yatakayofanyika mwaka Tanzania, Kenya na Uganda, hivyo tunapaswa kutumia nguvu na ubora wa kikosi chetu kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi ya awali,” alisema Msuva.

Hata hivyo, Msuva alisema pamoja na kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi za kufuzu AFCON 2027, alitamani mshambuliaji Mbwana Samatta aendelee kuitumikia Taifa Stars, lakini anaheshimu uamuzi wa nahodha huyo wa zamani wa timu hiyo kustaafu soka la kimataifa.

Msuva alisema Samatta tayari alikuwa amefanya uamuzi wake baada ya kushauriana na watu wake wa karibu, hivyo Watanzania wanapaswa kuuheshimu.

“Ninapenda siku moja Samatta apewe nafasi ya kueleza mwenyewe sababu zilizomfanya aamue kustaafu, nikiamini maelezo hayo yatakuwa muhimu kwa Watanzania kumwelewa zaidi,” alisema Msuva.

Kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, alisema anashukuru kwa kuitwa tena katika kikosi kwani ni heshima ambayo kila mchezaji anaitaka.

Fei Toto alisema timu yao ina nafasi ya kufanya vizuri katika AFCON 2027 kwa sababu itacheza nyumbani.

“Tunaendelea kufanya maandalizi kuelekea katika mechi zetu mbili, kwani maandalizi ya mapema ndiyo msingi wa mafanikio, hivyo anaamini uongozi pamoja na benchi la ufundi wataandaa timu vizuri,” alisema.

Fei Toto alisema katika kipindi hiki walikuwa wanamuhitaji Samatta,hata hivyo alisema wanaheshimu uamuzi wa nyota huyo.

“Bado tunamhitaji Samatta, katika kipindi hiki yeye ni mtu muhimu na sisi tunatamani kuendelea kuwa naye, ila maamuzi yake yaheshimiwe,”alisema Fei toto.

Mchezaji Nathaniel Chilambo, alisema wanaendelea vyema na maandalizi kuhakikisha wanakuwa fiti katika mechi zitakazofuata.

Chilambo alisema Taifa Stars ilijifunza mambo mengi kutokana na ushiriki wake katika AFCON 2025 nchini Morocco, akieleza kuwa uzoefu huo ni sehemu ya maendeleo ya timu.

“Tumejipanga vizuri kuhakikisha tunashinda katika mechi zetu mbili, tunaendelea vizuri na maandalizi kwani tunahitaji kufika mbali zaidi,” alisema.

Mshambuliaji Kibu Denis, alisema alipokea kwa furaha taarifa ya kuitwa kwake kwa mara nyingine katika kikosi cha Taifa Stars atahakikisha anapambana timu ifanye vizuri.

Katika michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika nchini Morocco Taifa Stars iliishia katika hatua ya 16 bora baada ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco uliochezwa Januari 4, mwaka huu.

Tanzania ilimaliza katika nafasi ya tatu katika Kundi C ya michuano hiyo ikiwa na alama mbili baada ya kupoteza dhidi ya Nigeria (2-1), kisha kutoka sare ya 1-1 na Tunisia hivyo ikafanikiwa kutinga hatua hiyo ya 16 bora kupitia moja ya timu zilizoshika nafasi ya tatu vizuri zaidi (“best loser”) na kuweka historia ya kutinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza.

Previous Post

YANGA, SIMBA, WADAU WAMLILIA FATMA KARUME

Next Post

TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

Next Post
TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

DK. NCHIMBI ATOA AGIZO KWA PROF. MKENDA

9 months ago
DK. SAMIA KUVALIA NJUGA SHIDA YA MAJI

DK. SAMIA KUVALIA NJUGA SHIDA YA MAJI

11 months ago

Popular News

  • TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

    TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA, WADAU WAMLILIA FATMA KARUME

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NGORONGORO HEROES YAFUZU AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MAMBO MOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?