• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TPDC : TUNAPIMA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAFUTA NA GESI KWA MANUFAA YA WANANCHI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 26, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TPDC : TUNAPIMA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAFUTA NA GESI KWA MANUFAA YA WANANCHI
0
SHARES
29
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KAIMU Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mha. Pachali Njiko, amesema mafanikio katika miradi ya mafuta na gesi asilia hayapimwi kwa thamani ya rasilimali zinazozalishwa pekee, bali pia kwa mchango wa sekta hiyo katika kuboresha maisha ya wananchi na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii zinazozunguka miradi.

Mha. Njiko ameyasema hayo leo Oktoba 26, 2026 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Likong’o, mkoani Lindi, katika hafla ya uzinduzi  ambapo Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, akiwa mgeni rasmi.

Mha. Njiko, amesema sera ya urejeshaji kwa jamii inalenga kutekeleza miradi mikubwa inayozingatia mahitaji halisi ya wananchi, kwa kushirikiana nao ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua.

Ameeleza ushirikishwaji huo umewezesha kutambua na kushughulikia mahitaji muhimu ya jamii, ikiwemo elimu, upatikanaji wa maji, utawala bora na michezo.

Amesema ujenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Likong’o umefanikishwa kupitia ushirikiano kati ya TPDC, kampuni za Equinor na Shell pamoja na wadau wao, ukiwa na thamani ya jumla ya shilingi bilioni 1.278.

Katika mradi huo, TPDC imechangia asilimia 26.68 ya gharama, Shell asilimia 36.66 na Equinor asilimia 36.66.

Ameongeza kuwa uwekezaji huo unaonesha namna sekta ya nishati inavyoendelea kuwa kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kufungua fursa kwa vizazi vijavyo.

Amesema shule hiyo itawawezesha wanafunzi kupata mazingira bora ya kujifunzia, yatakayochangia kuboresha ubora wa elimu, kuongeza maarifa na kuwajengea msingi wa kutumia fursa zitakazopatikana katika maisha yao ya baadaye.

Akieleza kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mha. Njiko amesema ujenzi ulianza Julai 2025 na unahusisha madarasa saba ya shule ya msingi na madarasa mawili ya shule ya awali, vyoo vya matundu 18 kwa shule ya msingi na matundu saba kwa shule ya awali.

Miundombinu mingine iliyojengwa ni jengo moja la utawala, vyumba viwili vya stoo, kichomea taka kimoja, matanki 12 ya kuhifadhia maji, nyumba mbili za walimu pamoja na samani za shule, zikiwemo meza na madawati.

Amesisitiza kuwa TPDC itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi asilia unaleta manufaa yanayoonekana kwa wananchi na kuchochea maendeleo endelevu ya jamii.

Previous Post

WAZIRI MKUU AKEMEA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI

Next Post

PROF. MBARAWA AMPA ONYO  MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA- ISAKA 

Next Post
PROF. MBARAWA AMPA ONYO  MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA- ISAKA 

PROF. MBARAWA AMPA ONYO  MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA- ISAKA 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA : TUTATUMIA UHAMIAJI KUKUZA UCHUMI

RAIS DK. SAMIA : TUTATUMIA UHAMIAJI KUKUZA UCHUMI

3 months ago
SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI:NI MAENDELEO, UWAJIBIKAJI

SIKU 100 ZA RAIS DK. MWINYI:NI MAENDELEO, UWAJIBIKAJI

9 months ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?