• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 28, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KUTATUA CHANGAMOTO ZA WALIPAKODI
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

KATIKA kuendelea kusogeza karibu zaidi na wananchi huduma za kodi, Mkuu wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro Mhe. Dastan Kyoba amezindua Kliniki ya Kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupatiwa huduma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kwenye mji wa Ifakara amesema Kliniki hiyo inaendelea kutoa huduma kwenye ofisi za TRA wilaya ya Kilombero zilizopo Ifakara kwa kutoa huduma zote za kodi ikiwemo kuwasikiliza walipakodi na kutatua changamoto zao.

Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kujitokeza kupata huduma hiyo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika katika eneo hilo na imetokana na ziara ya Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alipotembelea wilayani hapo na kuwasikiliza walipakodi.

“Tumieni fursa hii inayotokana na maelekezo ya Kamishna Mkuu wa TRA ambaye alitutembelea na kuwasikiliza na kuagiza kuwekwa kambi maalum ya huduma za kodi ili changamoto mlizoziwasilisha kwake na nyingine mlizonazo zipatiwe majibu hivyo msipoteze hiyo fursa” amesema Kyoba.

Aidha amewasisitiza wananchi umuhimu wa kudai risiti kwa kila manunuzi wanayofanya ili wachangie maendeleo ya nchi kwani miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali inahitaji fedha za walipakodi.

Kwa upande wake  Meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro Bi. Husna Nyange amesema wameanza kwa kusikiliza changamoto za walipakodi na kuzitatua papo kwa hapo ambapo wapo wataalam wa sekta zote muhimu za kodi wanaotoa majibu kwa changamoto za walipakodi.

Amesema kila mwananchi atakayefika katika eneo hilo atapatiwa huduma anayoihitaji sambamba na elimu ya kodi.

Amesema TRA imekuwa ikifanya jitihada za kusogeza huduma za kodi karibu na wananchi na kuendelea kutoa huduma bora zinazorahisisha ulipaji kodi na kuwezesha biashara.

Previous Post

SERIKALI YAIMARISHA UWEZO WA TPDC KATIKA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Next Post

TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

Next Post
TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

SERIKALI YATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI NISHATI ZA DOLA BIL. 12.9

8 months ago
SERIKALI YAIPA TANO YANGA

SERIKALI YAIPA TANO YANGA

1 year ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?