• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Toleo Maalumu

ELIMU YA WATU WAZIMA KICHOCHEO CHA UJUZI KUKUZA UTSATAWI WA KIUCHUMI

admin by admin
August 26, 2025
in Toleo Maalumu
0
ELIMU YA WATU WAZIMA KICHOCHEO CHA UJUZI KUKUZA UTSATAWI WA KIUCHUMI
0
SHARES
34
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

ELIMU ya Watu Wazima ilianzishwa na Mwalimu Julius  Nyerere mwaka 1975, kwa lengo la kuondoa adui ujinga kati ya wale maadui watatu wakiwemo maradhi na umaskini.

Wakati huo, Taifa lilikuwa na watu wengi wasiojua kusoma na kuandika, hivyo lilianzishwa kwa lengo kuwajengea mfumo mzuri wa elimu wapate fursa hiyo ya kujua kusoma na kuandika. 

Miaka hiyo, elimu ya watu wazima ilikuwa ni maalumu kwa watu wazima tu, lakini kwasasa imeboreshwa kuwafaa watu wote wanaohitaji elimu ya kusoma na kuandika zaidi sana kupata ujuzi kupitia elimu ya amali kupitia maendeleo ya Teknolojia yaliyopo sasa.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesisitiza kuwa, serikali itahakikisha Uchaguzi Mkuu, unakuwa huru na haki, huku akiwasisitiza wananchi kujiandaa kutumia haki yao kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka Oktoba 29 mwaka huu.

Pia, amesema serikali imejipanga vyema kuimarisha ulinzi na usalama, kuhakikisha utulivu wa amani, vinatawala kipindi cha kampeni, wakati na baada ya kupiga kura.

Majaliwa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipofungua Kongamano la Maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu. 

“Unayohaki ya kidemokrasia, kikatiba na kikanuni ya kupiga kura kuchagua kiongozi atakayekuletea maendeleo katika eneo lako au ngazi mbalimbali. “Tunatambua tunazo ngazi ya urais, ubunge na udiwani, kila mmoja wetu aliyekamilisha utaratibu za kupiga kura, namsihi ajitokeze kupiga kura.

“Tunawashukuru viongozi wa dini kwa namna ambavyo wameendelea kuombea amani yetu katika kipindi hiki, jukumu letu viongozi wa serikali ni kuhakikisha kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na uwepo wa amani na usalama kwa kila atakayejitokeza kwenda kupiga kura.

“Amani na utulivu kwetu ni muhimu kuliko kitu chochote,watu wote hao wanaoingia katika uchaguzi, watapita kueleza sera zao,kasikilizeni kwa umakini viongozi wenye sera na mambo mazuri wachagueni, tuwapate viongozi watakao fanya taifa letu kuwa endelevu na amani yake, mshikamano na utulivu.

Alieleza kuwa, wananchi wanaelewa zaidi umuhimu wa amani, kwani hawajazoea masuala ya kukimbizana, inafanyika mikutano mbalimbali kwa amani na utulivu mwanzo hadi mwisho pasipokuwa na mashaka, hayo ndiyo yanayohitajika kuendelezwa.

Majaliwa, alisema ipo demokrasiana uhuru wa kila mwananchi kuchagua kiongozi anayemtaka, kila mwananchi akasikilize ajitokeze kipindi hiki cha kampeni kusikiliza sera na ikifika siku ya kupiga kura akawachague viongozi anaowataka wenye sera nzuri.

Alitoa rai kwa wananchi, kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu, huku akiwapongeza viongozi wote waliotia nia na kuwatakia kheri katika hatua wanaoendelea nayo ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Kuhusu maonesho hayo, Waziri Mkuu Majaliwa, aliipongeza taasisi hiyo ya Elimu ya Watu Wazima kwa kutimiza miaka 50 kwa mafanikio makubwa, ikiwa ni historia ya kujivunia kwani matarajio ni kupitia jukwa hilo watajadiliana na kupata maazimio mazuri yenye tija kwa maendeleo ya Taasisi hiyo kwa miaka mingine mbeleni.

Pia, alitoa maagizo mbalimbali kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na taasisi hiyo, ikiwemo kuendeleza na kuimarisha matunizi ya Teknolojia, Habari na Mawasilino (TEHAMA), ambayo ni nyenzo muhimu ya kuvuka vikwazo mbalimbali vya kuwafikishia wananchi elimu katika kipindi hiki cha zama za mabadiliko na maendeleo ya teknolojia.

Maagizo mengine aliyoyatoa Waziri Mkuu kwa wizara ya elimu, ni kuongeza wigo wa kuendeleza elimu ya watu wazima, kuyafikia makundi yote hasa yaliyoko pembezoni yenye changamoto ya kufikiwa, kukuza mafunzo ya amali na stadi za kazi kupitia vyuo vya veta na wadau wengi wananchi wapate ujuzi na kujenga uchumi.

“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, hakikisheni mnaendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia kujenga na kukarabati vituo na kushirikisha taasisi binafsi, kupata vifaa vya kisasa kurahisisha utoaji elimu na kujifunzia.

Pia, kuendelea kufanya tafiti za mara kwa mara kwa Watanzania, kubaini mahitaji yao, changamoto na suluhisho zake,”alisema.

Aliwataka kuwafikia vijana wabunifu nakutambua kazi zao za ubunifu kuwezesha kuwa na tija kwa wahusika na manufaa kwa umma.

Alisisitiza ushirikiano na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuwezesha kuongeza uzoefu, rasilimali watu, kusaidia taasisi hiyo kuendelea kuwa na tija kwa wananchi.

“Shauku yetu ni kuona kuwa taasisi hii inakua zaidi kuwa taasisi yenye ushindani wa kimataifa na kuwa chachu ya maendeleo ya jamii, kiuchumi na kiteknolojia nchini,”alisema.

Majaliwa alisema elimu ya watu wazima siyo tu elimu ya masomo ya kawaida, bali ni zana muhimu ya maendeleo endelevu, kwani inachangia kipato, ustawi wa kijamii, afya na ushiriki wa kiraia, huku akisema uzoefu duniani unaonesha kwamba elimu ya watu wazima ni chombo muhimu cha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na binafsi.

Alihimiza kuwa elimu inayotolewa na Taasisi ya watu wazima siyo maalumu kwa watu wenye umri mkubwa tu, bali mwananchi yeyote anayetamani kujiendeleza na kupata ujuzi wa fani yoyote. 

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda alisema Taasisi hiyo ilianzishwa kuondoa adui ujinga, ambapo Mwalimu Julius Nyerere alianzisha kampeni ya Elimu ya kuwapa wananchi elimu kuondosha kutojua kusoma na kuandika.

AlisemaTaasisi hiyo ilianzishwa 1995, kuratibu na kusimamia elimu ya watu wazima, huku mafanikio yakifikiwa kwa kusimamia mipango iliyowekwa na uwekezaji mkubwa wa miundombinu.

Alieleza kuwa kwa ushiriki wa Waziri Mkuu amewasaidia kutangaza sana elimu hiyo, huku wakiendesha mafunzo na tafiti mbalimbali, kuendeleza ujuzi wa kujiendeleza hususan masuala ya Akili Mnemba, kutekekeza agizo la Rais Dk.Samia la wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa shuleni hivyo kupitia Taasisi hiyo wanajiendeleza.

Alimshukuru na kumpongeza kwa kazi nzuri na kubwa aliyoifanya kwa taifa akimsaidia Rais Dk.Samia kuwasimamia mawaziri na viongozi mbalimbali wa Serikali kutekekeza majukumu ya Serikali.

Profesa Mkenda alisema kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imekuwa ikitekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati ukiwemo mradi wa SEQUIP (Secondary Education Quality Improvement Project), ambapo umefanikiwa kuwarejesha wasichana 13,272 katika mfumo wa elimu katika kipindi cha miaka mitano.

Alieleza kuwa mradi mwingine ni IPOSA (Integrated Programme for Out-of School Adolescents), ambao umewezesha kuwajengea uwezo vijana 10,000 walioko nje ya mfumo rasmi katika maeneo ya stadi za maisha, ujasiriamali na ufundi wa awali.

Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Philip Sanga, alisema wamefurahi kufikia maadhimisho ya miaka 50 wakitoa Elimu bila ubaguzi ikiwa ni jitihada za serikali za kuiimarisha kuwa nyenzo muhimu ya kisiasa na kiuchumi.

Alisema Taasisi hiyo ni kongwe lengo kuhakikisha elimu inawafikia watu wote, ambapo kwa sasa wanaprogramu mbalimbali ikiwemo shahada.

Alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wamefanya mambo mengi, kusaini hati ya makubaliano naVETA wamepeleka wanafunzi 100 katika Chuo Cha Mafunzo (VETA) ya Morogoro kupata mafunzo ya astashahada.

Alitaja mipango yaoni kukamilisha utaratibu wa maboresho ya sheria, kuweka mkazo katika uimarishaji wa programu ikijumuisha mafunzo ya amali. 

Alitaja changamoto yao ni eneo la kujenga ofisi Mkoa wa Dodoma ambalo wanaendelea kulifuatilia, lengo ni kuhakikisha kwa miaka ijayo wanakuwa taasisi bora Afrika huku Mataifa mengine yakivutika kujifunza mafanikio yao. 

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, alisema Mkoa wa Dar es Salaam uko salama na utaendelea kuwa na amani wakati wote hasa wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Akielezea mafanikio ya sekta ya elimu ya Mkoa wa Dar es Salaam alisema Rais Dk.Samia ametoa fedha nyingi za ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa, kuboresha maslai ya watumishi wakiwemo walimu.

Alisema Rais Dk.Samia ameiwezesha taasisi hiyo kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wajasiriamali kutimiza takwa la kusoma na kuandika ikiwa ni hatua ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Profesa Zacharia Mganila, alimshukuru Rais Dk. Samia kwa kumwamini na kumchagua kuwa mwenyekiti wa  baraza la taasisi hiyo huku akiahidi kutimiza malengo kusudiwa. 

Alisema taasisi hiyo imeendelea kutengeneza miongozo ya kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii kwa sasa katika suala la elimu na ujuzi, akiahidi kuendelea kusimamia mifumo iliyowekwa na serikali ikiwemo sera mpya ya elimu iliyoweka mkazo katika elimu ya amali.

Katika hatua nyingine, taasisi hiyo ilitoa tuzo mbalimbali kwa viongozi akiwemo Rais Dk. Samia kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza elimu ya watu wazima, huku tuzo zingine zikitolewa kwa viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo wakiwemo wastaafu waliofanya kazi kubwa kuifikisha ilipofika.

Previous Post

Uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa asilimia 6.8

Next Post

DK. MPANGO ATOA MAAGIZO6 MUHIMU TAASISI ZA UMMA

Next Post
DK. MPANGO ATOA MAAGIZO6 MUHIMU TAASISI ZA UMMA

DK. MPANGO ATOA MAAGIZO6 MUHIMU TAASISI ZA UMMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

5 days ago
DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

1 day ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.