OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imetengua uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo.
Uamuzi huo umetokana na malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Monalisa Ndala, kuhusu uhalali wa Mpina kuwania nafasi hiyo.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amethibitisha kutenguliwa kwa Mpina na kueleza kuwa hatua hiyo inahusu uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
“Ni kweli tumewaandikia barua, ila tunaandaa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari,” amesema Nyahoza akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu.