• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

MAELFU WAZIDI KUMIMINIKA KUMSIKILIZA MGOMBEA URAIS WA CCM DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 30, 2025
in Habari, Siasa, Uchaguzi
0
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Morogoro

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania itakuwa nchi yenye neema itakayotekeleza miradi ya maendeleo pasipo kutegemea mikopo mikubwa, huku wananchi wakipata huduma bora za afya, elimu, umeme wa uhakika.

Amesema safari hiyo ya mafanikio itafikiwa katika miaka mitano ijayo, hivyo amewaomba Watanzania kuipigia kura CCM katika Uchaguzi Utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu kufanikisha neema hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani Mvomero eneo la Dakawa, Morogoro ambao ulihuduriwa na ‘mafuriko’ ya watu, Dk. Samia, alisema CCM ina historia ya utekelezaji ilani kwa mafanikio makubwa.

“Niwaombe tusimame pamoja kuiunga mkono CCM, tuendelee na kasi kujenga Tanzania tunayoitaka. ukifika mwaka 2050 (kwa mujibu wa dira ya maendeleo ya taifa 2050), tuwe tumeifika anzania yenye uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu.

“Hakuna Mtanzania atakayelia kukosa huduma za afya, elimu wala kukosa umeme.

 “Tutakuwa na Tanzania ambayo uchumi wake utasimama kujitegemea, hatutaishi wala kufanya shughuli za maendeleo kwa mikopo mikubwa. Na hiyo safari tunaanza miaka mitano inayokuja,”amesema.

Dk. Samia amesema kufikia azma hiyo, ifikapo Oktoba 29, mwaka huu, wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupiga kura kukichagua Chama Cha Mapinduzi.

Pia, amewapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 394,354 hadi kufikia zaidi ya tani 400,000 huku mazao ya kibiashara yakiongezeka kutoka tani 400,000 hadi tani zaidi ya 500,000.

Amebainisha kuwa, ongezeko hilo, limetokana na upatikanaji pembejeo, mbegu bora na zana za kilimo. Kuhusu migogoro baina ya wakulima na wafugaji, Dk. Samia, alisema kupitia kampeni ya Tutunzane, imewezesha kuleta utulivu, kupendana na amani.

“Kwa wafugaji wetu, tumeendelea kushirikiana nao ambapo tumeongeza minada ya mifugo kutoka mitatu hadi mitano, tumejenga machinjio Matano, mashamba darasa yameongezeka kutoka shamba moja hadi 42. Hii ni hatua kubwa nzuri, wananchi ni mashahidi wa kazi zilizofanywa na serikali ya CCM,” ameeleza.

Dk. Samia ameahidi, serikali yake, itakamilisha ujenzi kituo cha afya Dawaka, zahanati, kutekeleza bima ya afya kwa wote, kujenga na kuboresha shule za sekondari ikiwemo kukamilisha vyumba 31 vya madarasa ya shule za msingi.

“Tutandeleza kuchimba visima virefu, kuboresha barabara na madaraja, tutajenga machinjio ya kisasa, tutajenga njia kubwa ya kusafirisha umeme yenye msongo wa kilovoti 230 kutoka Morogoro hadi Dumila ambayo umeme utapita Mvomero, hivyo utawanufaisha wananchi,”amesema.

KATIBU MKUU CCM

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Asha – Rose Migiro, amesema amepata fursa ya kuzunguka katika eneo hilo la mkutano na kuwa, idadi kubwa ya wananchi, wana imani na mgombea urais wa CCM.

MGOMBEA UBUNGE MVOMERO

Kwa upande wake, mgombea ubunge Jimbo la Mvomero, Sarah Msafiri, amemshukuru Dk. Samia kwa kumaliza migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji kupitia falsafa ya 4R.

“Tulikuwa na migogoro mingi ya ardhi, hadi kufikia kushindwa kuzikana na kuchimba mitaro ya kutenganishwa kati ya wakulima na wafugaji, lakini kupitia maono ya Rais Dk. Samia kwa kushirikiana na viongozi wa dini na kimila kupitia programu ya Tutunzane wameweza kuiimaliza,” ameeleza.

Kwa upande wa miradi, amesema miaka minne wakati Dk. Samia, anaingia madarakani, kulikuwa na miradi 13 ya umwagiliaji, lakini kwa sasa mipya ni 730 ikiwemo katika Jimbo la Mvomero.

Rais Dk. Samia, ameingia mkoani Dodoma kuendelea na mikutano ya kampeni. Akiwa Kibaigwa, alihutubia umati mkubwa wa watu waliojitokeza kumsikiliza.

Previous Post

TAIFA STARS HAKUNA KULALA

Next Post

WANANCHI MAGU WAELEZA KWA UFASAHA AHADI ZA DK. SAMIA

Next Post
MGOMBEA Mwenza wa Urais Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Magu

WANANCHI MAGU WAELEZA KWA UFASAHA AHADI ZA DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRA : TUSAHAU MCHAKATO WA UCHAGUZI, SASA TUUNGANE KUSAKA DOLA

WASIRA : TUSAHAU MCHAKATO WA UCHAGUZI, SASA TUUNGANE KUSAKA DOLA

1 month ago
ARAJIGA, KAYOKO HAOO CAFCL

ARAJIGA, KAYOKO HAOO CAFCL

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.