• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

MOROGORO YA DK. SAMIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 30, 2025
in Habari, Siasa, Uchaguzi
0
MOROGORO YA DK. SAMIA
0
SHARES
18
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Morogoro

WANANCHI mkoani Morogoro wamethibitisha kwa vitendo kiu yao kuendeleza rekodi ya kuongoza kitaifa kwa kura za Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, baada ya kumhakikishia mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kumpigia kura za kishindo.

Hilo limethibitika katika mkutano wa kampeni za Urais uliofanyika leo (Agosti 29 mwka huu) viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro ambapo maelfu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo maarufu kwa shughuli za kilimo kujitokeza kumuunga mkono Dk. Samia alipokuwa akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambapo ameahidi kuurejesha mkoa huo kuwa wa viwanda.

Msafara wa Rais Dk. Samia uliwasili katika viwanja hivyo saa 14:42 mchana, ukisindikizwa na msafara wa matarumbeta, pikipiki huku nyimbo maalum ya kumpokea ikipigwa na bendi ya Tanzania One Theatre (TOT).

Akihutubia mkutano huo, Dk. Samia alisema CCM imejipanga vyema kuleta mageuzi makubwa katika mkoa huo.
Alisema katika miaka mitano ijayo, serikali itawekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya 28 na zahanati 97 huku Manispaa ya Morogoro vitajengwa vituo viwili vya afya na zahanati 11.

Pia, alisema serikali itakamilisha maabara, jengo la upasuaji na Kituo cha Afya Tungi pamoja na wodi ya mama na mtoto eneo la Mafiga.


“Tuawekeza katika elimu kwa kujenga madarasa 190 kwa shule za sekondari, ujenzi wa shule mpya ya wenye mahitaji maalum na kuendeleza sera ya elimu bila ada.

“Tutafikisha umeme vitongoji vyote na kuhamasisha uunganishaji umeme kwenye kaya. Tutajenga soko la kisasa Morogoro mjini kwa ajili ya wajasiriamali na wamachinga ili kuboresha mazingira yao.

Aliongea: “Tutajenga masoko mengine wilaya za Kilosa na Malinyi, kuwekeza kwenye mbolea ya ruzuku na mbegu bora. Tutajenga maghala matano wilayani Kilosa katika ushoroba wa reli ya SGR kurahisha usafirishaji mazao.”

Kadhalika, alisema CCM kupitia ilani yake imepanga kujenga vituo vya kupoza umeme, Tungi, Msavu, Kilosa na Mvomero.
“Dhamira yetu ni kuufufua Mkoa wa Morogoro kuwa Mkoa wa viwanda, viwanda vipya vinakuja vikubwa na vidogo. Jitihada hizo zitasaidia kuvutia uwekezaji na hivyo kuongeza fursa za ajira,” alieleza.

Previous Post

CCM IMEJIPANGA KUFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU – BALOZI DK. MIGIRO

Next Post

TANZANIA IPO SALAMA MIKONONI MWA CCM – PETER MSIGWA  

Next Post
TANZANIA IPO SALAMA MIKONONI MWA CCM – PETER MSIGWA  

TANZANIA IPO SALAMA MIKONONI MWA CCM – PETER MSIGWA  

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUBAKI HISTORIA

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUBAKI HISTORIA

2 months ago
KISHINDO CHA DK. NCHIMBI RUVUMA

KISHINDO CHA DK. NCHIMBI RUVUMA

4 weeks ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.