• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUBAKI HISTORIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 31, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUBAKI HISTORIA

MGOMBEA Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa Kilosa

0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH

KATIKA kuhakikisha migogoro baina ya wakulima na wafugaji inabaki historia, mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi serikali kuja na mpango kabambe kutokomeza kabisa migogoro hiyo nchini.

Amesema mara baada ya kuingia madarakani, Serikali ya CCM itapanua eneo la ufugaji kutoka ekari milioni 3.46 hadi kufikia ekari milioni sita hatua ambayo itapanua wigo wa maeneo ya wafugaji.

Akizungumza wilayani Kilosa (Agosti 30 mwaka huu) katika mwendelezo wa kampeni za Urais, Dk. Samia ameahidi kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika Jimbo la Kilosa kupitia mpango maalumu wa ‘Tutunzane’ ambao tayari umeonyesha mafanikio wilayani Mvomero.

“Serikali itapanua eneo la wafugaji kutoka ekari milioni 3.46 za sasa hadi kufikia ekari milioni sita, hatua ambayo inalenga kupunguza migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Dk. Samia amesisitiza: “Nafahamu zipo changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na wakulima ambayo tayari imeanza kufanyiwa kazi, lakini ahadi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuendeleza programu ya Tutunzane na kuongeza eneo la wafugaji ili kuepusha migogoro hiyo.”

Kuhusu dira ya taifa ya maendeleo 2050, Dk. Samia amesema Tanzania itakuwa nchi yenye neema itakayotekeleza miradi ya maendeleo pasipo kutegemea mikopo mikubwa huku wananchi wakipata huduma bora za afya, elimu, umeme wa uhakika.

Amesema safari hiyo ya mafanikio itafikiwa katika miaka mitano ijayo hivyo aliwaomba Watanzania kukipigia kura CCM kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu ili kufanikisha neema hiyo.

“Niwaombe tusimame pamoja kuiunga mkono CCM tuendelee na kasi kujenga Tanzania tunayoitaka. Tukifika mwaka 2050 (kwa mujibu wa dira ya maendeleo ya taifa 2050) tuwe tumeifika Tanzania yenye uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu. Hakuna Mtanzania atakayelia kukosa huduma za afya, elimu wala kukosa umeme.

Amesisitiza: “Tutakuwa na Tanzania ambayo uchumi wake utasimama kujitegemea, hatutaishi wala kufanya shughuli za maendeleo kwa mikopo mikubwa. Na hiyo safari tunaanza miaka mitano inayokuja.”

Dk. Samia amesema ili kufikia azma hiyo, ifikapo Oktoba 29 mwaka huu, wananchi wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupiga kura kukichagua Chama Cha Mapinduzi.

Previous Post

KIBAIGWA IMEFUNIKA, OKTOBA WANATIKI KWA DK. SAMIA

Next Post

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA ZAIDI GAIRO

Next Post
DK. SAMIA AAHIDI NEEMA ZAIDI GAIRO

DK. SAMIA AAHIDI NEEMA ZAIDI GAIRO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. MWINYI : HURUMA NA UADILIFU VIWE KIPAUMBELE MWEZI MTUKUFU

RAIS DK. MWINYI : HURUMA NA UADILIFU VIWE KIPAUMBELE MWEZI MTUKUFU

2 months ago
JAJI CHANDE AJIBU HOJA 8 NZITO TUME

JAJI CHANDE AJIBU HOJA 8 NZITO TUME

7 days ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?