Na ABDURAHMAN JUMANNE,
Mara
MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amehutubia mamia ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Ubwere, Wilaya ya Rorya, mkoani Mara, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Katika mkutano huo, Dk. Nchimbi ambaye ni mgombea mwenza wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliwaombea kura wagombea wa CCM, akiwemo mgombea ubunge wa Jimbo la Rorya, Jafari Chege, sambamba na wagombea wengine wa ubunge na udiwani wa mkoa huo.
Amesema chama hicho kimejipanga kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini, iwapo kitapata ridhaa ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Dk. Nchimbi ataendelea na mikutano ya kampeni katika mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.