Na MWANDISHI WETU,
Babati
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema wanapomwombea kura Mgombea Urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, Watanzania ni mashahidi wa kazi kubwa alizofanya katika miaka minne na nusu ya uongozi wake.
Wasira amesema hayo, katika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi na wanachama wa CCM, wilayani Babati.
Ameleza tangu Rais Samia achukue uongozi kutoka kwa mtangulizi, Hayati Dk. John Magufuli, kuna mambo makubwa yamefanyika nchini.
“Wanataka kumwondoa, lakini sababu hawana na ukisema nao wapinzani pembeni, wanasema lakini nyie wakubwa, mmefanya mambo mengi.
“Nilikuwa mjumbe wa kamati iliyoandika Ilani mpya ya mwaka 2025 2030, akanipigia kiongozi mmoja wa chama cha upinzani, anasema nimeisoma Ilani yenu, mmeandika kila kitu, sasa sisi tutaandika nini?.
“Kwa sababu CCM, tulikuwa na Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020 imetekelezwa mpaka tumevuka na ushahidi wake hata hapa Babati upo katika sekta zinazohusu watu.