• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 3, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi

0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Maswa

MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amesema Mgombea Urais wa Chama, Dk. Samia Suluhu Hassan, iwapo atapewa ridhaa ya kuongoza nchi, ndani ya siku 100 za kwanza, ataanzisha Tume ya Maridhiano, Watanzania wote wawe kitu kimoja, wasikilizwe na watoe mawazo yao.

Amesema atafanya hivyo, Watanzania waendeleze umoja, mshikamano na upendo kwa nchi.

Dk. Nchimbi, amesema hayo katika Kata ya Lalago, wilayani Maswa, mkoani Simiyu, wakati wa mkutano wa hadhara wa kunadi sera za Chama na kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025.

Aidha, kuitangaza Ilani mpya ya Chama ya mwaka 2025-2030 na kumwombea kura Rais Dk. Samia, wabunge na madiwani wawachague Oktoba 29, mwaka huu kwa kishindo.

Amesema hakuna faida yoyote ya kuwa na taifa ambalo lina watu wanaovurugana, wasiosikiliza, wasioheshimiana, hivyo lazima huko watoke.

“Tunakwenda kutoka huko kwa kuanzisha Tume ya Maridhiano itakayotufanya Watanzania wote tuwe kitu kimoja,” amesema.

Balozi Dk. Nchimbi ameongeza serikali ya chini ya uongozi wa Dk. Samia itakapopata ridhaa ya kuongoza nchi itaanzisha mfumo mpya wa mawasiliano kati ya wananchi na serikali.

Mgombea Mwenza wa Urais huyo amesema mfumo huo unaopimika kila mwananchi atawasiliana na mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa na ofisi ya Rais moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Balozi Dk. Nchimbi, rais atapima sehemu ya kushughulikia matatizo ya wananchi kwa haraka mahali watakapoanzia.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA WILAYANI MASWA

Dk. Nchimbi, ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dk. Samia, ni kuimarika kwa huduma za afya kutoka vituo vitatu miaka mitano iliyopita hadi kufika vinane.

Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa zahanati kutoka 34 hadi 44, huku katika kuboresha Hospitali ya Wilaya ya Maswa, zimejengwa maabara mpya, jengo jipya la mionzi, matibabu ya dharura na kupanuliwa kwa wodi.

Kuhusu sekta ya elimu, Balozi Dk. Nchimbi, amesema shule za msingi zimeongezeka kutoka 125 hadi kufikia 135, shule za sekondari kutoka 36 hadi  47.

Akizungumzia madarasa, Dk. Nchimbi, amesema yaliyokuwepo awali yalikuwa 1,513, ambapo 504 yamejengwa, hivyo kufanya idadi yake kufikia 2,017 na kiwango cha upatikanaji maji, nacho kimeongezeka, ambapo watu 73 kati ya 100, wanapata maji safi na salama.

ILANI 2025- 2030

Balozi Dk. Nchimbi, amesema katika miaka mitano ijayo, wamedhamiria kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vipya sita, zahanati 10.

Amebainisha katika shule za msingi wamekusudia kujenga madarasa mapya 100, shule za sekondari mpya 200, vyumba vya maabara 75 na kuimarisha mtandao wa maji safi na salama kutoka maeneo ya Budekwa, Kiloleni na Mwabayanda.

Balozi Dk. Nchimbi amesema mtandao wa mabomba ya maji unatarajiwa kuimarishwa zaidi, wananchi wapate maji safi na salama.

AKIWA KISHAPU

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Nchimbi, amemwahidi Mgombea Urais, Dk. Samia, kuwa atamsaidia kusukuma gurudumu la kuwaletea maendeleo Watanzania, pindi wakipata ridhaa ya kuongoza nchi.

Ahadi hiyo, ameitoa wakati akiwa Kata ya Mhunze, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, jana, baada ya kusimikwa rasmi kuwa Chifu Msaidizi wa Chifu Hangaya, ambaye ni Dk. Samia.

Hayo yalijiri katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na kuwanadi wagombea ubunge na udiwani huku akieleza sera za CCM na utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2020-2025 na kuinadi ilani mpya.

Dk. Nchimbi, alisimikwa na watemi wa kabila la Kisukuma, lengo likiwa ni kumsaidia Dk. Samia, alivishwa shuka la rangi nyeusi kama ishara ya mawingu mazito ya mvua ambayo ni neema kwa Watanzania wote.

Aidha, Balozi Dk. Nchimbi, alivishwa shuka nyeusi nayo ikiwa ni ishara ya kulinda amani na utulivu kwa nchi, alikabidhiwa mkuki ikiwa na maana ya kukumbushwa kuwa mlinzi wa mila na desturi nchini.

Pia, alivishwa mkufu wa simbi na alikabidhiwa usinga kama ishara ya kuwatuliza wananchi na kuwapa baraka atakapokuwa anawapungia, kuashiria amani na utulivu.

Pia, watemi hao, walisema kuanzia hivi sasa, ataitwa mfungua njia zote, asiwepo wa kumzuia na kwamba, kazi hiyo, itakuwa ni kufungua njia kwa Chifu Hangaya.

Baada ya kukabidhi zana hizo, Dk. Nchimbi, alimshukuru kiongozi wa watemi kwa heshima kubwa waliyompa ya kumsimika kuwa chifu msaidizi wa Chifu Hangaya

“Nataka niwahakikishie kwamba, kwa heshima kubwa, heshima hii naithamini, nawahakikishia nitamsaidia Chifu Hangaya kwa uwezo wangu wote.

“Kwa akili zangu zote na kwa juhudi zangu zote na kwamba, nitatimiza  azma yake ya kuwaletea maendeleo Watanzania,”amesema

Previous Post

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

Next Post

WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

Next Post
WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA ATANGAZA HATUA ZA MWISHO UTEKELEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

DK. SAMIA ATANGAZA HATUA ZA MWISHO UTEKELEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

2 weeks ago
MOROCCO ATAJA KILICHOIPONZA STARS

MOROCCO ATAJA KILICHOIPONZA STARS

5 days ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.