• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 3, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,
SONGWE

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kufanya makubwa zaidi katika sekta za elimu, afya, maji, umeme na miundombinu huku akitangaza mpango wa uboreshaji wa barabara ya TANZAM na reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), lengo likiwa kumaliza msongamano wa maroli yanayokwenda Zambia kupitia mpaka wa Tunduma.


Amesema barabara hiyo, imeanza kujengwa kwa njia nne kutoka Igawa hadi Tunduma, yenye urefu wa kilometa 75 hatua ambayo itaimarisha shughuli za usafirishaji mizigo katika njia hiyo.


Akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma mkoani Songwe, Dk. Samia, alisema uboreshaji uliofanyika Bandari ya Dar es Salaam, umechochea ongezeko la mizigo kutoka tani milioni 15 hadi milioni 28 kwa mwaka.


“Natambua uboreshaji mkubwa uliofanyika Bandari ya Dar es Salaam, umeongeza mizigo inayotoka nchini kwenda nje ya nchi. Kabla ya uboreshaji, tani za mizigo zilikuwa zikiingia bandarini ni milioni 15.8 na baada ya uboreshaji, bandari inapokea tani milioni 28 za mizigo.


“Mzigo unaovuka mpaka wa Tunduma, umepanda kutoka tani milioni 3.7 hadi milioni tisa. Hali hiyo, inaleta msongamano wa maroli ya mizigo yanayoelekea kuvuka mpaka wa Tunduma, kwa maana hiyo, tumeanza ukarabati kwa kupanua barabara kuu ya TANZAM, inayounganisha Tanzania na Zambia.

Kazi inaendelea na tutaendelea nayo hadi itakapokamilika,”amesema.


Dk. Samia, amesema ukarabati huo, umeanza kwa njia nne kutoka Igawa hadi Tunduma kwa urefu wa kilometa 75, huku mazungumzo ya kukarabati na kuimarisha reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) yakiendelea.


Amesema reli hiyo ya muda mrefu, imechoka na kusababisha kubeba kiwango kidogo cha mizigo wakati huu ambao idadi ya mizigo ikiongezeka katika Bandari ya Dar es Salaam.


“Tutakamilisha ujenzi wa Bandari kavu eneo la ekari 1,800, Katenjele, Kata ya Mpemba ili maroli yasiegeshwe barabarani, tutaongeza barabara mbadala itakayoanzia Mwakabanga, tutajenga maegesho ya kisasa, kuongeza mizani, kuharakisha uchakataji nyaraka kabla ya magari kufika mpakani.

“Pia, serikali tumeanza kuzungumza na mamlaka za ukusanyaji mapato Zambia, ifanye kazi saa 24 kama ilivyo kwa Tanzania,” alisisitiza,”amesema.


Amesema serikali imejipanga kutekeleza mradi wa umeme kutoka Iringa – Njombe hadi Tunduma wenye msongo wa kilovoti 730, kati ya hizo, kilovoti 400, zitatumika Tunduma na Rukwa, huku kilovoti 330, zitauzwa Zambia.


“Tumekamilisha mazungumzo, tumeanza mchakato kujenga njia hii umeme ufike uhakika. Hii inakwenda pamoja na uhamasishaji matumizi ya nishati safi kwa sababu, umeme na gesi ni nishati safi,” ameeleza.


Ameongeza: “Nataka kuwathibitishia na kuwaahidi, nitaendelea kufanya makubwa katika sekta ya elimu, afya, maji na umeme.

“Tunakwenda kutoa huduma kwa wananchi, tutaendelea kuongeza shule, elimu bila ada, mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na VETA, kujenga vyuo vya VETA ili kuwawezesha vijana wapate ujuzi na kujiajiri.


“Tutaendelea kujenga vituo vya afya na zahanati, tunakwenda kumaliza miradi ya maji lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania apate maji safi na salama kwa asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini.

“Baadhi ya maeneo, tumefikia, lakini baadhi miradi inaendelea. Umeme tumemaliza vijiji vyote, tupo nusu ya vitongoji na tunakwenda kuunga umeme kila mwananchi afaidike,”amesema.


Vilevile, amesema alipotoa ahadi ya mambo atakayoyatekeleza ndani ya siku 100 endapo atakapochaguliwa, amesema mpango wa bima ya afya kwa wote utakaoanza kwa majaribio, wagonjwa watakaopata msamaha wa vipimo vya matibabu ni wale wanaotoka kaya masikini.


Mgombea huyo wa Urais kupitia CCM ametumia fursa hiyo, kuomba kura kwa wananchi ifikapo Oktoba 29 mwaka huu, wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa CCM kuanzia Rais, wabunge na madiwani.


“Kubwa zaidi CCM tunaweza, tunafanyakazi, kujali utu wa mtu na ndiyo maana tunasema ‘Kazi na Utu’ kuanzia huduma za afya, maji ni kujali utu wa mtu, tunapoongeza uzalishaji chakula ni kujali utu wa mtu.

lakini la pili tunajiamini, uwezo tunao na nyezo za kufanyiakazi tunazo. Pigeni kura kwa CCM kama kawaida yetu ni mafiga matatu, Rais, wabunge na madiwani,” ameeleza.


AKIWA VWAWA


Akiwa katika mkutano wake uliofanyika viwanja vya TACRI eneo la Vwawa, Dk. Samia, alisema serikali imeitendea haki Songwe, kwani wabunge wanajivunia maendeleo yaliyofanyikiwa.


“Maendeleo ni tele kwa tele, kuhusu ujenzi wa barabara Mlowo – Kasamba inakwenda kujengwa.

Kuhusu mbolea Nilikuwa nazungumza na Waziri wa kilimo, mbolea ya kupandia tumbaku imeshaingia bado kusambazwa, mbolea ya kupandia mazao imeshaingia bado kusambazwa.

Niwahakikishie wakulima kwamba, mbolea imeingia bado kusambazwa,” amebainisha.


KATIBU MKUU WA CCM


Naye, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Asha – Rose Migiro, amesema mambo mengi yamefanyika chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia, ikiwa ni utekelezaji ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025.


“Wananchi wa Songwe wana matumaini makubwa, tutakapopata ridhaa katika kipindi kifupi kijacho, mengi yatakamilishwa na katika ilani ya uchaguzi 2025 – 2030, makubwa yatafanyika,” amesisitiza.


CHONGOLO AFUNGUKA


Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Daniel Chongolo, alisema hakuna sababu ya kubishana na wale ambao wanaendeleza maneno ya uongo, kwani ndiyo kazi ambayo wameichagua.


“Mgombea wetu anafanyakazi ya ‘katapila’ wapo mabingwa wa kupiga porojo, tuwaachie hiyo ndiyo kazi waliyoichagua.

“Tunapoteza muda na watu waliotimiza wajibu wao, sisi tuna wajibu wa kujenga nchi. Hapa wapo watumishi wa umma kwa kipindi kifupi, Rais wetu ameruhusu watumishi wote wenye sifa kupandishwa madaraja,” ameeleza.


KOMREDI MOHAMMED KAWAIDA


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM), Mohammed Kawaida, amemshukuru Rais Dk. Samia kwa kutoa ajira kwa vijana, mikopo ya elimu ya juu, vyuo vya kati na mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu.


MGOMBEA UBUNGE VWAWA
Kwa upande wake, mgombea Ubunge Jimbo la Vwawa, Japhet Hasunga, amesema ruzuku ya pembejeo iliyotolewa na serikali, imeongeza uzalishaji wa chakula, hali ambayo imechangia kuongeza kipato cha wananchi hivyo kuwaepusha na njaa.


Pia, amesema zaidi ya sh. bilioni tatu zimetengwa kujenga soko la kimataifa katika eneo hilo huku sh. bilioni 12.9 zilitolewa kujenga Hospitali ya Rufaa Mkoa ambayo sasa wananchi wanaendelea kupatiwa matibabu.


Vilevile, alisema Rais Dk. Samia ametoa sh. bilioni 3.5 kujenga majengo ya halmashauri katika eneo la Old Vwawa ambako ujenzi unaendeleo.


MWENYEKITI CCM SONGWE


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Rodwell Mwampashi, amemshukuru mgombea urais na Kamati Kuu ya CCM kwa kuwarudisha wabunge waliofanyakazi vizuri katika kipindi kilichopita.


Amesema CCM ilisimamia vyema utekelezaji wa ilani, kuhakikisha Ilani ya Chama inatekelezwa kwa usahihi huku akitoa wito kwa wananchi na wanachama wa CCM kumpigia kura Dk. Samia  aendeleze kasi ya maendeleo mkoani hapa.


MGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU
Mgombea ubunge wa Viti Maalumu, Juliana Shonza, amempongeza Dk. Samia kwa kuunganisha mkoa huo katika gridi ya Taifa ya umeme hali ambayo imewafanya kupata nishati hiyo kwa uhakika.
Amesema vitongoji 800 vimeunganishwa na umeme ambapo vimebaki vitongoji 500 ambavyo tayari katika bajeti vitafikiwa.

Previous Post

FADLU AWAONGEZEA ‘DOZI’ MASTAA WAKE

Next Post

DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

Next Post
DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

DK. NCHIMBI : SIKU 100 TUME YA MARIDHIANO ITAANZISHWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WANASIASA WAELEZA IMANI YAO TUME YA JAJI CHANDE

WANASIASA WAELEZA IMANI YAO TUME YA JAJI CHANDE

2 weeks ago
YANGA YARIDHISHWA UUZAJI WA JEZI

YANGA YARIDHISHWA UUZAJI WA JEZI

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?