• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Burudani

FADLU AWAONGEZEA ‘DOZI’ MASTAA WAKE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 3, 2025
in Burudani, Habari, Michezo
0
FADLU AWAONGEZEA ‘DOZI’ MASTAA WAKE
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WAKATI kikosi cha Simba kikiendelea na maandalizi ya tamasha la Simba Day na msimu mpya wa michuano mbalimbali, Kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids amesema kuwa amewaongezea ‘dozi’ wachezaji wake kuhakikisha anakuwa na kikosi bora zaidi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kocha Fadlu, amesema kuwa walipokuwa Misri katika kambi ya muda, alihakikisha anatoa mazoezi yakutosha kupata muunganiko mzuri wa wachezaji kitu alichofanikiwa.

Amesema wachezaji hasa wapya wamekuwa wakionyesha kiwango bora, hivyo amewaongezea dozi kuhakikisha wanakuwa fiti zaidi.

Amesema kuwa baada ya kurejea hapa nchini ameona awaongezee dozi wachezaji hao ili aweze kupata kikosi cha kwanza kilichokuwa bora na chenye uwezo wa kupambana na timu yoyote.

“Katika maandalizi yangu sijajiandaa tu na kucheza mechi kwa dakika 90, bali wingi wa mechi tutakazokwenda kucheza, tutacheza mechi kila baada ya siku tatu, tutasafiri umbali mrefu, ndiyo maana nimeona niwaongeze dozi wachezaji wangu.

“Tumefanya usajili mzuri na kila mchezaji anaonyesha ushirikiano wakutosha katika mazoezi tunayoendelea nayo wakiwemo wapya ambao wameshajiliwa mara ya kwanza kikosini.

“Ninaamini tutakuwa na kikosi cha ushindani chenye uwezo wa kupambana na timu yoyote msimu mpya,” alisema Kocha Fadlu.

Hata hivyo kocha huyo amekiri kuwa kuna baadhi ya wachezaji wapya hawatokuwepo Simba Day, Septemba 10, kutokana na kwenda kuzitumikia timu zao za Taifa.

Amesisitiza mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kuangalia kiwano cha kikosi chao katika mchezo huo dhidi ya Kenya, utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Kuna wachezaji wetu wapya, hatutokuwa nao katika mchezo dhidi ya Gor Mahia kwani watakwenda kuzitumikia timu za Taifa katika mechi za Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), hivyo tunaamini watakaobakia watatoa burudani murua kwa mashabiki zao.

“Baadhi ya wachezaji walikuwa katika timuya Taifa Stars katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024), lakini hivi sasa tayari walishajiunga na wenzao na wanaendelea vizuri na mazoezi,” amesema.

Amesema baada ya kumalizika kwa tamasha hilo watakuwa na siku chache kuelekea katika mechi za kimataifa, hivyo itakuwa ngumu lazima wawe na kikosi chenye ubora kwa ajili ya kushindana.

Naye Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, aliwataka mashabiki na wapenzi wa soka nchini kujaa kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri katika msimu mpya utakaoanza hivi karibuni.

Amesema kuwa mashabiki wa Simba wanatakiwa kuujaza uwanja lengo likiwa ni kuwasapoti wachezaji wao na kuona viwango bora vya wachezaji waliosajiliwa kwa msimu mpya.

“Tunawaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuhakikisha wanaujaza uwanja siku hiyo ikiwemo kupata burudani nzuri kutoka kwa wachezaji wa timu yao.

“Simba Day ni tamasha la kipekee kwetu, na litatoa mwanga wa ubora na uwezo wa wachezaji tulionao kwa msimu mpya, tunaamini litafanyika kwa ukubwa wake kama ilivyozoeleka,” amesema.

Simba itaadhimisha tamasha lao la 17, tangu lilipoanzishwa mara ya kwanza 2009, chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo wakati huo, Hassan Dalali.

Katika tamasha hilo, burudani hutawala, pamoja na mechi mbalimbali za bonanza, kabla ya mashabiki kupata fursa ya kuwaona wachezaji wapya na wale wote wanaunda kikosi cha msimu, hatimaye kucheza mechi rasmi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Previous Post

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FUSRA AFCON

Next Post

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

Next Post
CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SUMAYE: DK. SAMIA NDIYE KIONGOZI MWENYE UPEO

SUMAYE: DK. SAMIA NDIYE KIONGOZI MWENYE UPEO

1 week ago
TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.