• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

SERIKALI ITAIMARISHA TIBA ZA KITALII – DK. MPANGO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 4, 2025
in Habari, Kitaifa
0
SERIKALI ITAIMARISHA TIBA ZA KITALII – DK. MPANGO

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango

0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na SELINA MATHEW,

Dodoma

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango, amesema serikali imedhamiria kuimarisha huduma za tiba za kitalii, kama sehemu ya mikakati ya kuboresha na kuimarisha sekta ya afya nchini na kuchangia pato la taifa.


Hayo aliyasema Dodoma, katika halfa ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha mafunzo, matibabu ya saratani na uzinduzi wa kituo cha upandikizaji figo katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, wenye thamani ya sh. bilioni 30.4.

Alisema mchango wa Utalii wa Tiba katika pato la taifa, hivi sasa, unakadiriwa kuwa sh. bilioni 166.5 na idadi ya wagonjwa wanaokuja kutibiwa nchini, imeongezeka kutoka 5,700 mwaka 2021 hadi 12,180 mwaka huu.

Alisema eneo la Utalii Tiba, anautambua mchango wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, unaotokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali katika miundombinu, vifaatiba, vyenye teknolojia ya kisasa na wataalamu waliobobea.


“Hatua hii, inatoa fursa ya kuendelea kupanua huduma za Utalii Tiba, zitakazowezesha wagonjwa kutoka nchi mbalimbali, hususan zinazotuzunguka kuja kwa wingi kutibiwa nchini.

“Huduma hizi zitachangia kuinua viwango vya utoaji huduma na vilevile, zitaendeleza ushirikiano kati ya nchi yetu na jirani na kutuongezea fedha za kigeni,”alisema.


Aliishauri hospitali hiyo, kuwa na ubia na Sekta Binafsi au Halmashauri ya Jiji, iangalie uwezekano wa kujenga jengo maalumu la huduma za malazi na nyinginezo kama chakula na fedha, kwa ndugu na wagonjwa wanaotoka nchi jirani au mikoani, hasa wanaposubiri matibabu au kuruhusiwa kurejea makwao baada ya matibabu.


Kuhusu elimu ya afya, Dk. Mpango alisema ili kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, ni lazima jitihada za makusudi zifanyike.


Alieleza kuwa, miongoni mwa mikakati iliyopo ni  kupunguza vihatarishi vya magonjwa hayo kwa kuelimisha jamii kuchukua hatua stahiki za kujikinga na maradhi, ikiwemo kuboresha mtindo wa maisha kwa kuzingatia ulaji unaofaa, kupunguza matumizi ya pombe, kuacha matumizi ya tumbaku, kufanya mazoezi na kuepuka tabia bwete.


“Mtindo wa maisha usiofaa ni miongoni mwa vihatarishi vikubwa vya magonjwa mengi yasiyoambukiza ikiwemo saratani,”alisema.

Pia, alishauri kuwa elimu-kinga inayotolewa izingatie kwa kadri inavyowezekana, elimu, aina ya kazi, kipato na mazingira ya mgonjwa kwa ujumla.


Aliwataka madaktari na wahudumu wote wa afya, kuhakikisha kuwa, elimu kwa umma kuhusu kujikinga na magonjwa, inahusisha makundi mbalimbali kuepuka gharama kubwa za matibabu.

Dk. Mpango, aliwataka wawe wabunifu katika kutoa elimu ikiwa ni pamoja na kutumia njia mbalimbali hasa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na mifumo ya kidijitali kuwafikishia wananchi elimu hiyo muhimu.


“Natoa rai kwa Watanzania wote kuzingatia ushauri na elimu tunayopewa na wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na Maofisa Maendeleo ya Jamii, kwa faida yetu wenyewe na Taifa,”alisema Dk. Mpango.

Pia, aliigiza Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kuweka utaratibu wa kuwasomesha na kuwaendeleza madaktari hadi kufikia ngazi ya ubingwa na ubobevu katika kutibu magonjwa ya saratani, upandikizaji wa figo na upandikizaji wa uboho.


Aidha, aliitaka Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuangalia uwezekano wa kuanzisha ushirikiano na wataalamu wengine kutoka nje ya nchi kama vile Japan, Korea na mataifa mengine kuwajengea uwezo wataalamu.

Pia, alifafanua kuwa, Serikali imeendelea kutoa kipaumbele katika utoaji wa huduma za afya zenye ubora na zinazowafikia wananchi wote kuboresha afya zao.


Alisema Serikali inatambua umuhimu wa afya bora kwa wananchi wake kwani ni raslimali muhimu kwa maendeleo.


“Ninawasihi madaktari na wahudumu wote wa afya katika Hospitali hii kuzingatia kiapo cha maadili ya taaluma yenu, kujituma na kutoa huduma zenye viwango na zinazomjali mteja/mgonjwa,”alisema.


Pia, aliielekeza Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao kuhakikisha mifumo ya matibabu katika Hospitali za kitaifa na zile maalum za kikanda (Muhimbili, Bugando, KCMC, Mbeya Zonal Referral Hospital, Ocean Road Cancer Institute, na Benjamin Mkapa) inasomana.


Awali, alifafanua kuwa takwimu zinaonesha kuwa, ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani za aina mbalimbali, kama saratani ya shingo ya mlango wa kizazi, tezi dume, matiti, umio na nyinginezo, zinasababisha vifo vingi zinapochelewa kugundulika au kukosa tiba sahihi.


Alisema kwa sasa, matibabu ya uhakika ya Saratani yanapatikana katika Hospitali za Ocean Road, Dar es salaam na Bugando, Mwanza.


Hivyo, mradi wa ujenzi wa kituo cha umahiri cha matibabu ya magonjwa ya Saratani ambao Jiwe lake la Msingi ameliweka, utaongeza upatikanaji wa matibabu ya uhakika kwa Wananchi wa Kanda ya Kati na Mikoa ya jirani.


Alitoa wito kwa Wizara ya Afya kusimamia kwa karibu mradi huo, kuhakikisha ujenzi na usimikaji wa vifaa tiba unakamilika kwa wakati na wataalamu wa kutosha wanakuwepo.


Kuhusu magonjwa ya figo, alisema ni changamoto nyingine kubwa inayowakabili wananchi na katika kukabiliana na tatizo hilo, Hospitali ya Benjamin Mkapa ilianza kutoa huduma za upandikizaji figo mwaka 2018 kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na shirika la TOKUSHIKAI la Japan.


“Hadi sasa, idadi kubwa ya wagonjwa wamepandikizwa figo na wengine wanaendelea na huduma za usafishaji damu. Kwa Bahati mbaya, asilimia kubwa ya wananchi wenye changamoto hii na wenye vigezo vya kupandikizwa figo, hawana uwezo wakugharamia matibabu hayo.
“Kwa wasiofahamu, gharama za huduma za kusafisha damu mara tatu kwa wiki, kwa mgonjwa ni sh. 900,000, mbali na gharama za usafiri, vipimo vya damu na dawa,”alisema.


Alisema gharama za kupandikiza figo ni sh. milioni 35 kwa mgonjwa, ukiacha zinazolipwa na Bima ya Afya na maandalizi ya anayetoa figo.


Alibainisha kwa kulitambua hilo, Serikali katika kipindi cha mwaka 2023/24 hadi 2024/25 ilitoa ufadhili wa zaidi ya sh. milioni 700 kwa Hospitali hiyo kwa wagonjwa ambao hawana uwezo wa kugharamia matibabu hayo huku wagonjwa 20 wakinufaika.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Abel Makubi, alisema kituo hicho kikikamilika kitahudumia wananchi milioni 14 waliokuwa wakienda kupata matibabu Dar es Salaam, kuongeza wagonjwa watakaohudumiwa kwa mwaka kutoka 5000 hadi 8500 kwa mwaka na kupunguza rufaa kwenda nje.

Previous Post

WASIRA ATABIRI RUNDO LA KURA KWA DK. SAMIA

Next Post

TCU YAFUNGUA DIRISHA UDAHILI AWAMU YA PILI

Next Post
TCU YAFUNGUA DIRISHA UDAHILI AWAMU YA PILI

TCU YAFUNGUA DIRISHA UDAHILI AWAMU YA PILI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRI : CCM INAFANYA KAZI KUBWA YA KULETA MAENDELEO

WASIRI : CCM INAFANYA KAZI KUBWA YA KULETA MAENDELEO

4 weeks ago
KIKWETE AWATOLEA UVIVU WAZUSHI, ASEMA UTEUZI WA DK. SAMIA ULIFUATA KATIBA YA CCM

KIKWETE AWATOLEA UVIVU WAZUSHI, ASEMA UTEUZI WA DK. SAMIA ULIFUATA KATIBA YA CCM

2 months ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.