• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Burudani

RC MAKALLA AKAGUA UJENZI UWANJA WA AFCON ARUSHA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 5, 2025
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
RC MAKALLA  AKAGUA UJENZI UWANJA WA  AFCON ARUSHA

KUU wa Mkoa wa Arusha, CPA. Amos Makalla

0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU,

Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA. Amos Makalla, ametembea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu utakaotumika kwenye mashindano ya  Mataifa ya Afrika ya AFCON mwaka 2027 unaojengwa na serikali kwa gharama ya Shilingi bilioni 340, kwenye Kata ya Olmot Jijini Arusha.

Ukaguzi huo umefanyika baada ya kikao kazi kilichofanyika kikihusisha wakuu wa idara na mamlaka zinazohusika na miundombinu ya huduma za Maji, nishati, barabara na mawasiliano katika uwanja huo, wakiazimia kuteua Kikosi kazi cha wataalamu wa sekta hizo chini ya mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambao watakuwa uwanjani hapo muda wote kushughulikia uwekaji wa miundombinu hiyo chini ya Mpango mkakati wa dharura.

“Kama Mkoa wa Arusha tunajivunia utalii, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mawili Royal Tour, ametangaza utalii na anatuletea Utalii wa michezo (sport tourism) na uwepo wa uwanja huu utaongeza mzunguko wa pesa utakaochochea ukuaji wa biashara na uchumi wa mtu mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.

Hivyo tunamuhakikisha Mhe. Rais kwamba tutamuwakilisha vyema, tutasimamia ukamilishaji wa uwanja huu ili kuhakikisha malengo aliyotarajia yanatimia na mkandarasi ametuhakikishia kwamba utakamilika kama ilivyopangwa Julai 2026.” Amesema Mhe. Makalla.

Aidha Makalla amesisitiza kuwa uwanja ni mkubwa na wa kisasa wenye kukidhi viwango vya Shirikisho la soka barani Afrika CAF, akisema maamuzi haya ya Rais Dk. .Samia ya kutumia mapato ya serikali kuujenga uwanja huo yanakwenda kuipa heshima Tanzania na kuwapa fursa wananchi wa Arusha na watanzania kwa ujumla kuweza  kushuhudia mashindano hayo nchini mwao, yakifanyika kwa ushirikiano wa Mataifa ya Tanzania, Kenya na Uganda.

Hata hivyo Mwakilishi wa mkandarasi anayetekeleza mradi huo China Railway Construction ya nchini China Mhandisi Denice  Benito Mtemi amesema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 60 ukitarajiwa kujumuisha nyasi asili kwenye sehemu ya kuchezea na kwenye uwanja wa mazoezi, Vyumba vinne vya kubadilishia Mavazi, yote haya yakiwa yamezingatia Vigezo vya kimataifa, huku akimshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa wakati na hivyo kutosababisha kikwazo katika ujenzi huo.

Previous Post

CCM YATAJA SABABU MBILI KUOMBA KURA SONGWE

Next Post

‘WALIPENI WAKULIMA, WAFANYAKAZI’

Next Post
‘WALIPENI WAKULIMA, WAFANYAKAZI’

‘WALIPENI WAKULIMA, WAFANYAKAZI’

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

2 days ago
DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

5 days ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.