• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

‘WALIPENI WAKULIMA, WAFANYAKAZI’

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 6, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
‘WALIPENI WAKULIMA, WAFANYAKAZI’

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Rungwe

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amewataka wawekezaji wa mashamba ya chai kulipa madeni ya wakulima na wafanyakazi wa viwanda vya zao hilo, kabla serikali haijatwaa mashamba ambayo walibinafsishiwa.

Amesema wawekezaji hao pamoja na serikali kuweka mazingira bora ya uwekezaji, wameshindwa kuyaendeleza mashamba hayo na kutolipa madeni ya wakulima na wafanyakazi.

Pia, ametangaza mpango wa serikali kujenga vituo 50 vya kuhifadhi parachichi, ukiwa mkakati wa kuhakikisha soko la uhakika kwa wakulima wa zao hilo.

Akizungumza na maelfu ya wananchi, wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Manzese wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Dk. Samia, amesema serikali itasimama bega kwa bega na wakulima nchini.

Amewataja wawekezaji hao ni WETCO na Kampuni ya Mohammed Enterprises, ambao wamelalamikiwa kutolipa madeni ya wakulima na wafanyakazi wa viwanda vyao.

“Nikianza na hoja ya chai, najua katika chai, kuna mtu anaitwa WATCO na Mohammed Enterprises, ndugu zangu, mashamba haya tuliyatoa tukiamini kwamba, sekta binafsi tutafanya nayo kazi kwa maendeleo ya watu.

“Hivyo ndivyo inavyotokea maeneo mengi, serikali tumeamua kufanya kazi na sekta binafsi, tunasaidiana kuleta maendeleo ya watu. “Kwa maana hiyo, serikali tuliweka mazingira mazuri ya uwekezaji kuanzia sheria, sera na mambo mengine,” ameeleza.

Amesema katika kuweka mazingira bora kwa wawekezaji, serikali imeendelea kusambaza umeme vijijini, kujenga miundombinu ya barabara na maji.

Dk. Samia, amesema lengo la hatua hiyo ni kusaidia wananchi na kuwawezesha wawekezaji kufanya shughuli zao katika mazingira bora.

“Tulikubaliana na wenzetu hawa WETCO na Mohammed Enterprises kuwapa mashamba, waweke viwanda, chai iongezwe thamani kabla ya kusafi rishwa, lakini inavyoonekana, hii kazi sasa imewashinda.

Ameongeza: “Kinachofanyika sasa, serikali imeunda timu ambayo inafanya tathmini ya mashamba na viwanda, lengo letu ni kuyachukua pamoja na viwanda, kisha kumilikisha kwa vyama vya ushirika chini ya uongozi wa serikali.”

“Pia, tunajua kwamba watu hawa wanamadeni kwa wafanyakazi wao wa viwanda lakini pia kwa wakulima. Nataka niwaambie tumewaelekeza waanze kulipa madeni ya watu,” amesisitiza.

Mgombea huyo wa Urais kupitia CCM, alisema serikali imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hao kupata mikopo katika taasisi za kifedha ili kulipa madeni.

“Lazima madeni yalipwe, madeni ya wakulima, lakini pia madeni ya wafanyakazi wa viwanda. Lazima yalipwe kabla ya serikali haijachukua mashamba na kuwamilikisha wanaushirika. Nataka niwaahidi siyo muda mrefu madeni yatalipwa,” amesisitiza.

Kauli hiyo ya Dk. Samia aliibua shangwe kutoka kwa wananchi wa wilaya hiyo ambayo wanategemea kilimo cha zao hilo na parachichi kuwainua kiuchumi.

ATANGAZA MKAKATI ZAO LA PARACHICHI

Kwa upande wa parachichi, Dk. Samia, aliwapongeza wakulima wa zao hilo kwa kuongeza uzalishaji na kuifanya Tanzania kushika nafasi ya tatu duniani.

Amesema parachichi kutoka Tanzania yamepata soko katika mataifa mbalimbali duniani.

“Lakini kama mnavyojua biashara bei inapanda na kushuka, kwenye chai hivyo hivyo soko la dunia limepanda halafu likashuka na ndiyo maana wawekezaji wakashindwa kuendeleza, lakini serikali kama soko ni zuri kama soko ni baya wajibu wetu ni kuwashika wakulima wetu na hicho ndicho tunachokwenda kufanya.

“Duniani wanazalisha parachichi kwa bahati mbaya zinazalishwa wakati mmoja na ndiyo maana bei inashuka kwa sababu wanunuaji wanakuwa na uwanja mpana wa kuchagua,” ameeleza.

Amesema mkakati wa serikali ni kujenga vituo 50 vya kuhifadhi zao hilo na viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya parachichi.

“Tunachokwenda kufanya tunakuja kujenga vituo 50 vya kuhifadhia parachichi, viwili vitakuwa hapa Rungwe ambavyo vitakuwa na baridi ya kuhifadhia parachichi na mazao mengine ya mbogamboga.

Amesisitiza: “Tuvute muda wakati mataifa mengine yamezalisha parachichi na zina nunuliwa duniani, za kwetu zivute muda na tunatarajia vituo vitakavyojengwa vitaweza kuhifadhi parachichi zetu kwa miezi mitatu ili soko lipande.”

Amesema wakulima na wanaushirika watauza katika vituo ambavyo vitakusanya, kuhifadhi kusubiri soko lipande bei.

Vilevile, alisema serikali ina lengo la kujenga kongani ya viwanda katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilayani Rungwe.

“Kwa upande wa Rungwe tutakuja kuweka viwanda chini ya vijana kupitia mpango wa BBT, tutawajengea vijana viwanda vidogo vya kuongeza thamani zao la parachichi.

“Kwa zile zinazoharibika zenye dosari ambazo hatutaweza kuziweka, tutazalisha vitu vingine kama mafuta na vyakula vya wanyama, tutakuja kuweka viwanda ili vijana wetu waweze kuziongezea thamani parachichi,” amebainisha.

Dk. Samia alisema serikali imetoa bure miche 1,000 ya zao hilo kwa wakulima pamoja na kuajiri maofi sa ugani.

“Tumeamua kuajiri maofi sa ugani maalum kwa zao la parachichi na hao watawekwa kwenye maeneo ambayo yanalimwa parachichi.

Alibainisha: “Watapima udogo, kutoa huduma za ugani kama pembejeo na mbolea. Tutaendelea kutoa ruzuku kwenye zao la parachichi.”

Kwa upande wa dawa, alisema tayari serikali imeshanunua dawa hizo zenye thamani ya sh. bilioni mbili.

AKATA MZIZI WA FITNA

Akizungumzia kuhusu wanachama wa CCM kubebwa katika magari kuhudhuria mikutano hiyo, alisema hakuna sababu ya mwanachama kutembea kilometa 90 kuhudhuria mikutano hiyo, wakati Chama kina uwezo wa kuwaleta mikutanoni.

“Jana nilimuona mwenezi wa chama chetu, Kenani Kihongosi akihojiwa na waandishi wa habari, wakimwambia kuwa, Chama Cha Mapinduzi, mnasafirisha watu ndiyo maana mikutano yenu inajaa.

“Huwezi kutegemea mtu anatoka kilometa nyingi huko zaidi ya 90 ndani ya Rungwe atembee kwa miguu. Lazima tuwasaidie usafiri wafike, lakini hatutoi watu wilaya nyingine kwenda wilaya nyingine.

Amesisitiza: “Kama wana imani ya kuja kusikiliza lazima tuwape imani ya kuwasogeza kuja kutusikiliza, kwa hiyo siyo shida wala siyo aibu kwa chama kuwasafirisha wanachama wake kuja kusikiliza Ilani ya chama inasemaje lakini yale ambayo tumewatendea pia.”

Rais Samia amesema lengo la CCM ni kuhakikisha inamaliza changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini

MAOMBI YA WABUNGE

Awali, wagombea ubunge katika majimbo ya Rungwe na Busokelo, walimwomba Dk. Samia kushughulikia changamoto katika mazao ya chai na parachichi.

Mgombea ubunge Jimbo la Rungwe, Anthony Mwantona, alisema kiwanda cha chai kilichopo eneo hilo, kimefungwa huku wakulima na wafanyakazi wakidai malipo yao.

Previous Post

RC MAKALLA AKAGUA UJENZI UWANJA WA AFCON ARUSHA

Next Post

DK. NCHIMBI AWAAHIDI FURSA WACHIMBAJI WADOGO

Next Post
DK. NCHIMBI AWAAHIDI FURSA WACHIMBAJI WADOGO

DK. NCHIMBI AWAAHIDI FURSA WACHIMBAJI WADOGO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI : CCM INAJIVUNIA MTAJI MKUBWA WA WANACHAMA

DK. NCHIMBI : CCM INAJIVUNIA MTAJI MKUBWA WA WANACHAMA

1 month ago
DK. SAMIA NI KIONGOZI MWENYE NGUVU KUIVUSHA TANZANIA – CHONGOLO

DK. SAMIA NI KIONGOZI MWENYE NGUVU KUIVUSHA TANZANIA – CHONGOLO

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.