• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WALIOONGOZA KURA ZA MAONI WAPEWA JUKUMU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 11, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
WALIOONGOZA KURA ZA MAONI WAPEWA JUKUMU
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema wanachama walioongoza kura za maoni na kupewa dhamana ya kupeperusha bendera ya Chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, wana dhamana ya kuwaunganisha wana CCM na sio kuwafarakanisha.

Amesema CCM ni kama mtumbwi unaosafiriwa na wengine, hivyo, haitavumiliwa kuona watu wachache wanataka kuutoboa na kuzamisha watu wote.

Wasira, alieleza hayo, Kilombero mkoani Morogoro alipozungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya wilaya hiyo, akiwa katika ziara ya kutafuta kura za mgombea urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan na wagombea ubunge na udiwani.

Alisema anatambua kuna msuguano, katika baadhi ya kata ambapo walioshindwa, wanasema hawajashindwa vizuri, hivyo kusababisha misuguano na walioshinda.

“Sisemi hapa mna matatizo makubwa, wala si kweli, yako majimbo yana matatizo, nimepitapita huko nimekutana na matatizo makubwa, kuna mahali imenibidi nifanye maamuzi magumu, hapa ninaambiwa matatizo hayo yapo ila yanaweza kumalizwa.

“Sasa ushauri wangu au niagize kwa wale walioshinda, ninyi mna dhamana zaidi ya kuleta umoja kuliko walioshindwa, kwa sababu ukishinda na wewe tena ukawa unatamba na watu wako nao wanawatambia wengine, unatufarakanisha,” alisema.

Alisema ushindi walioupata baadhi ya wana CCM kwa kuongoza kura za maoni, unatokana na mfumo uliojiwekea Chama kupata wagombea.

“Ule ushindi wa ndani ya Chama ni mfumo wa kupata mgombea, siyo mapambano ya kufanya wengine waonekane wanafaa na wengine hawafai, siyo kweli.

“Maana kuna mahali pengine hata aliyeongoza hatukumchukua tukamchukua wa pili, kuna mahali tukamchukua wa tatu,” alisema.

Aliwasihi waliopewa nafasi kuonesha njia katika kuleta umoja kwa walioshindwa kwa kuwa, wote ni wanachama wa CCM na uongozi ni zamu kwa zamu.

“Hivyo, kama ilikuwa zamu yenu kuongoza, basi ambao hawakuongoza na wao zamu yao itakuja.

“CCM sisi ni kama watu tunasafiria katika mtumbwi, usitoboe mtumbwi ambao tunasafiria wote, maana ukiutoboa, tunazama wote, kwa hiyo ukiongoza leo, utaongoza kwa miaka mitano, mtumbwi ule utakuwa bado upo kwa wengine nao kusafiria,” alisema.

Previous Post

DK. NCHIMBI ATOA AHADI YA KONGANI

Next Post

TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

Next Post
TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

TANZANIA IMEJIPANGA – DK. MIGIRO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MTANDAO WA GESI KINYEREZI HADI CHALINZE, SASA WANUKIA

MTANDAO WA GESI KINYEREZI HADI CHALINZE, SASA WANUKIA

9 months ago
WATANZANIA WAMKUMBUKA KWA KAZI KUBWA ALIYOIFANYA ENZI ZA UHAI WAKE

WATANZANIA WAMKUMBUKA KWA KAZI KUBWA ALIYOIFANYA ENZI ZA UHAI WAKE

3 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?