Na NJUMAI NGOTA,
Tanga
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa, amesema Dk. Samia Suluhu Hassan,amethibitisha uwezo mkubwa kwa kuleta mageuzi chanya katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wake.
Pia, Chama kimejidhihirisha kuwa na sera madhubuti, itikadi imara na falsafa makini, kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Mchungaji Msigwa, alisema hayo Uwanja wa Cleopa Msuya, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.
“Tumeshuhudia ujenzi wa zahanati, upatikanaji majisafina salama, barabara za lami na uboreshaji wa huduma zaafya na elimu.
“Mama Samia ameonesha weledi wa hali ya juu namapenzi ya dhati kwa nchi yetu,” alisema.
Aidha, katika kuonesha dhamira ya kuendeleza kasi yamaendeleo, Mchungaji Msigwa, alisema Dk. Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kuwa Mgombea Mwenza huku akieleza kuwa, ni kiongozi mwenye uwezomkubwa, uzoefu na uchapakazi.
“Kama zawadi kubwa kwa kazi nzuri ya Dk. Samia, nikumpa kura za ndiyo kwa wingi.
“Pia, tunamletea Dk. Nchimbi kuwa, Mgombea Mwenza. Huu ni uteuzi makini, unaoonesha nia ya kuendeleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita,” alisema.
MAFANIKIO YA SERIKALI
Msigwa aliwataka wananchi waendelee kuiamini CCM kwa sababu, mafanikio yaliyopatikana, yanazungumza yenyewe kama kuongezeka vituo vya afya, kupungua kwavifo vya watoto wachanga, ujenzi wa madarasa unaosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi, kuongezeka kwa barabara za lami na huduma za jamiivijijini na mijini.
“Mkiulizwa kwa nini CCM tena? Waambieni tunaona maendeleo kwa macho yetu.
“Tunaona shule zikijengwa, tunapunguza ujinga, tunalima kwa weledi, tunafanya kazi kwa ujuzi kwa sababu yauongozi madhubuti wa Dk. Samia,” alisisitiza.
MSIGWA ATAKA KURA TATU KWA CCM
Msigwa aliwaomba wakazi wa Mwanga, kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, Oktoba 29, mwaka huu nakuhakikisha wanapiga kura zote tatu kwa CCM kwa Dk. Samia, Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Dk. Ngwalu Maghembe na udiwani kwa wagombea wa CCM katika kata zote.
“Hakikisha unapiga kura ya ndiyo kwa Dk. Samia, kuraya ndiyo kwa Dk. Maghembe kuwa Mbunge na kura zakutosha kwa madiwani wa CCM. Tufanye kazi hii kwaumoja na ari mpya,” alisema.