• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA KULETA TEKNOLOJIA YA KILIMO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 27, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA KULETA TEKNOLOJIA YA KILIMO

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Mtwara

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema miaka mitano ijayo serikali yake itajikita kuleta mapinduzi katika matumizi ya teknolojia sekta ya kilimo.

Amesema mkakati huo, utajikita katika kuongeza uzalishaji mazao, upatikanaji masoko, maabara za utafiti, kuimarisha mawasiliano na taarifa za hali ya hewa.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa Nanenane mjini Mtwara, Dk. Samia amesema miaka mitano ijayo, itakuwa miaka ya kupiga hatua kubwa katika matumizi ya teknolojia ya kisasa.

“Vilevile miaka mitano ijayo, tunataka kuchukua hatua za makusudi kudumisha mila, tamaduni na desturi zetu siyo zile zenye madhara.

“Tutaongeza matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo akili unde (AI) kuimarisha ufanisi katika uzalishaji na utoaji huduma ikiwemo kilimo.

“Katika kilimo tumeanza kwa kufanya tafiti kwa njia za kisasa ambazo ni tafiti za mbegu, udongo na tafiti mbalimbali katika kilimo ambazo tunazifanya kwa kutumia teknolojia ya kisasa,”amesema.

Dk. Samia amesema Julai, mwaka huu alipata fursa kufungua maabara kubwa ya kitaalamu mkoani Dodoma ambayo inakwenda kufanyakazi za tafiti katika kilimo.

Pia, amesema mwaka jana alifungua maabara katika Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) itakayotumika kuwafundisha vijana namna ya kuzalisha mazao kitaalamu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

“Katika masuala ya vipimo, tumeanza kuona katika uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambapo wale wanaokwenda kuuza mazao NFRA (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula) wakifika pale ni teknolojia inayotumika kutoa unyevu wa mahindi na mizani za kisasa kujua uzito.

“Hapo hapo mkulima anapata risiti yake kwa mashine na anapokea meseji katika simu yake kwamba, umeleta mzigo fulani, unyevu upo kiasi fulani na gredi ya mazao yako kiasi fulani hivyo fedha zako kwa bei ni kiasi fulani,” amewaeleza wananchi.

Pia, amesema matumizi ya teknolojia yatatumika kuimarisha mawasiliano na ufuatiliaji hali ya hewa.

Amebainisha teknolojia hiyo itakwenda kufundishwa kwa wanafunzi kuanzia ngazi za vyuo.

“Hapa ndipo tunakwenda kuunganisha teknolojia, mila na tamaduni zetu. Tutakwenda kufundisha teknolojia ambayo haitafuta, haitaharibu na haitawapotosha vijana wetu.

“Kadri inavyowezekana teknolojia tunayokwenda kuitumia tunataka tuirithishe na tuipe hadhi kujenga kizazi kijacho chenye maadili,”amesema.

BILIONI 726/- KUTOA RUZUKU KWA WAKULIMA

Katika hatua nyingine, Dk. Samia alisema mwaka 2021/22, serikali iliamua kuanza mfumo wa ruzuku za pembejeo katika zao la korosho.

Alisema tangu kipindi hicho, hadi hivi sasa pembejeo zimetolewa bure huku kiwango kikiongezeka kila mwaka.

“Serikali imefanya uamuzi huo na miaka minne iliyopita, tumeshatumia sh. bilioni 726 kugawa mbolea na pembejeo za ruzuku kote nchini.

“Tunatumia sh. bilioni 192 kila mwaka, fedha ambayo ingekuwa inatoka mfukoni kwa wakulima, lakini tumezibakisha mifukoni mwao.

“Mbolea, salpha, dawa za kuua wadudu tunatoa bure. Kwa hiyo ndugu zangu serikali inafanya hivyo kwa sababu tumedhamiria kukuza kilimo na uzalishaji wa korosho,”alisema.

Dk. Samia alisema uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani 118,000 mwaka 2021 ambazo zilikuwa na thamani ya sh. bilioni 265, ambapo hivi sasa uzalishaji umekua kufikia tani 330,505 zilizouzwa katika msimu uliopita zikiwa na thamani ya sh. trilioni 1.9 ambazo zimeingia kwa wakulima.

Alieleza hayo ni manufaa makubwa kwa wakulima, kwani bila ruzuku uzalishaji ungeshuka na mapato kwa wakulima yangeporomoka.

Alibainisha serikali itaendelea kutoa huduma hizo kwa wakulima lengo likiwa kuongeza uzalishaji.

“Kama mnavyofahamu nchi yetu ni ya pili kwa Afrika katika uzalishaji korosho, wanaotupita ni Ivory Coast wa pili ni sisi. Tutaendelea kuweka jitihada twende sanjari na nchi hiyo ambayo inaongoza.

“Jitihada hizi zimechangia kuongeza uzalishaji siyo tu katika korosho bali pia kwenye mbaazi na ufuta. Uwekezaji mwingine ni kuongezeka kwa skimu za umwagiliaji,”alisema.

Dk. Samia alisema skimu hizo katika mkoa huo, zipo 66 ambapo kuna miradi miwili mikubwa yenye thamani ya sh. bilioni 38.6 inayojengwa Ndanda (Masasi) na Arusha chini (Newala).

Alieleza endapo CCM ikipewa ridhaa ya kuliongoza taifa, itaendelea kutafuta masoko yenye uhakika siyo tu kwa zao la korosho bali mazao yote.

Vilevile, alisema serikali itaendelea kuvutia uwekezaji katika ujenzi wa kongani ya viwanda iliyopo kijiji cha Maranje wilayani Mtwara.

Pia, alisema serikali itaendelea kusimamia kwa karibu vyama vya ushirika uondoa ubadhilifu wa fedha za wanaushirika na pia ucheleweshaji malipo kwa wakulima.

Alibainisha lengo la serikali ni kuvifanya vyama hivyo kuwa vyenye uwezo wa kujitegemea.

Katika hatua nyingine, alisema serikali imeanzisha benki ya ushirika iweze kutoa huduma bora kwa vyama vya ushirika.

Vilevile, alisema katika upande wa huduma za kijamii uwekezaji mkubwa umefanyika katika maeneo mbalimbali.

“Kimkoa nakumbuka Septemba 15, 2023 nilikuja kuzindua hospitali ya rufaa kanda ya kusini ambayo imesogeza huduma za kibingwa karibu zaidi na wakazi wa Mtwara, Lindi na Ruvuma.

“Mbali na hospitali hiyo, Mkoa wa Mtwara sasa una hospitali mbili za rufaa ambayo ya Ligula na Ndanda. Pia kuna hospitali tatu za halmashauri (Manispaa ya Mtwara, Nanyamba na Wilaya ya Mtwara) haya ni maendeleo ndugu zangu,” alisisitiza.

Aliwaahidi wananchi wa mkoa huo kwamba, serikali yake itaboresha zaidi huduma zinazotolewa kwa kupeleka vifaa tiba zaidi na kuongeza watumishi wa afya.

Katika hatua nyingine, alisema serikali ilileta sh. bilioni 87 za miradi ya maji ambapo endapo akipewa ridhaa ya kuliongoza taifa atakwenda kukamilisha mradi uliobaki wa Makonde kutoa maji kutoka Mto Ruvuma.

Alisema mradi huo, utamaliza changamoto ya uhaba wa maji Nanyamba, Mtwara Mjini na vijijini.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Saidi Njegendi, alieleza kuwa katika kipindi cha miaka minne mafanikio makubwa yameshuhudiwa katika majimbo yote ya uchaguzi.

Alibainisha wakati Dk. Samia alipoingia madarakani mkoa huo ulikuwa ukizalisha tani 100,000 za korosho lakini hadi mwaka jana zaidi ya tani 300,000 zimezalishwa.

“Hayo yamewezekana mbali na kugawa pembejeo, ameajiri maofisa ugani 535 ambao walitoa elimu kwa wakulima kuhusu kilimo bora cha korosho.

“Wakati unaingia madarakani mbaazi ilikuwa mboga lakini ukapandisha bei ya mbaazi kutoka sh. 200 kwa kilo hadi zaidi ya sh. 2,000 kwa kilo. Sasa mbaazi siyo mboga bali ni zao la biashara,” alisisitiza.

Pia, alisema Dk. Samia ametoa zaidi ya sh. bilioni 38 kutoa maji Mto Ruvuma kwenda Nanganka pamoja na vijiji vinavyopitiwa na mradi huo.

Alimpongeza Dk. Samia ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa huo wa mpakani.

WAGOMBEA UBUNGE

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Tandahimba, Katani Katani, alieleza kuwa Mkoa wa Mtwara umenufaika kupata barabara zaidi ya kilometa 160 za lami huku Jimbo la Tandahimba likipata kilometa 60.

Pia, alisema Dk. Samia ametoa sh. bilioni 84.7 kuanza utekelezaji mradi wa maji Makonde ambao kwa muda mrefu utekelezaji wake ulisuasua.

Kadhalika, alisema Dk. Samia ni kiongozi wa kwanza nchini kutoa pembejeo kwa wakulima zenye thamani zaidi ya sh. bilioni 600.

“Kwa niaba ya Wanatandaimba nikuhakikishie Jimbo la Tandahimba litakuwa la kwanza kukupa kura za kutosha katika uchaguzi huu,” alisisitiza.

Naye, mgombea ubunge Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota, alisema Dk. Samia ametoa pembejeo za kutosha na kuchagia ongezeko la uzalishaji korosho zaidi ya tani 30,000 kutoka tani 16,000 kwa mwaka.

Alisema Dk. Samia amejenga kongani ya viwanda vya korosho katika jimbo hilo hivyo kuongeza ajira zaidi ya 10,000 kwa wananchi wa eneo hilo.

“Ukaja na mkakati mwingine badala ya kutegemea korosho umeanzisha mradi mkubwa wa umwagiliaji wenye kujumuisha ekari zaidi 1,000. Pia umetuingiza katika mradi wa TACTIC ambao utajenga kituo cha mabasi, soko jipya na barabara za lami.

“Hakuna haja ya kuyumbayumba Oktoba 29, mwaka huu. Kwa ajili ya korosho yetu, kwa ajili ya ujenzi wa kongani za viwanda, twendeni tukampigie kura Dk. Samia,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Newala Vijijini, Yahya Nawanda, alisema mwaka huu zaidi ya sh. bilioni 15 zimepelekwa katika jimbo hilo za ununuzi wa pembejeo za korosho.

Alisema wananchi wa Newala vijijini wamenufaika baada ya kujengewa hospitali ya wilaya ambapo sasa hawalazimiki kwenda Ndanda kupata huduma za afya.

Kuhusu maji, alisema jimbo hilo limepewa sh. bilioni 84.7 kugharamia mradi huo ambao utawezesha wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa zaidi ya asilimia 50.

Mgombea ubunge Jimbo la Mtwara Mjini, Joel Nanauka, alisema Septemba 23 mwaka 2023, Dk. Samia alipofanya ziara katika mkoa huo, aliagiza korosho zisafirishwe kupitia Bandari ya Mtwara.

Alisema uamuzi huo umechangia Manispaa ya Mtwara kuongeza mapato yaliyowezesha utekelezaji miradi 43 ya maendeleo kupitia ushuru.

Nanauka alisema uamuzi huo pia umewezesha wanawake na vijana zaidi ya 3,000 kupata ajira kupitia usafirishaji korosho.

Kwa upande wa maji, alisema Dk. Samia alitoa sh. bilioni 3.1 kutekeleza mradi wa ujenzi chujio la maji hali iliyowezesha kuongeza ubora wa maji.

Aliongeza ujenzi wa hospitali ya rufaa katika mkoa huo umewezesha zaidi ya wananchi 80,000 kupatiwa matibabu mkoani hapo bila kupewa rufaa.

Previous Post

SIMBU APANDISHWA CHEO

Next Post

DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

Next Post
DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KIBAIGWA IMEFUNIKA, OKTOBA WANATIKI KWA DK. SAMIA

KIBAIGWA IMEFUNIKA, OKTOBA WANATIKI KWA DK. SAMIA

2 months ago
DK. NCHIMBI ATAJA KIPAUMBELE CCM

DK. NCHIMBI ATAJA KIPAUMBELE CCM

1 day ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.