• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA AWEKA REKODI KABAMBE MWANZA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 9, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AWEKA REKODI KABAMBE MWANZA

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Mwanza

NI zaidi ya mafuriko. Ndivyo ilivyoshuhudiwa baada ya maelfu ya wananchi kufurika katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, kumsikiliza Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

Wananchi hao, wameufanya Mkoa wa Mwanza wenye idadi kubwa ya wapiga kura katika Kanda ya Ziwa, kuingia katika rekodi ya mkutano huo, kuhudhuriwa na idadi kubwa zaidi ya wananchi.

Hali hiyo ni uthibitisho, Dk. Samia, anaendelea kuwa mgombea mwenye ushawishi mkubwa kwa wananchi kipindi hiki, ambacho Oktoba 29, mwaka huu, Watanzania watatimiza haki yao, kidemokrasia kuchagua viongozi.

Katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika, Dk. Samia alisema amedhamiria kuufungua mkoa huo, kiuchumi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema serikali imetoa sh. trilioni 5.6, ambazo zimetumika katika mkoa huo, kuleta maendeleo kupitia miradi mbalimbali

Alisema katika sekta ya afya, serikali katika mkoa huo, imeboresha hospitali mbili kubwa za rufaa, ambazo ni Sekou Toure ambako kumejengwa jengo la ghorofa tano la mama na mtoto kwa sh. bilioni 10.1.

Alisema jengo hilo, lina uwezo wa kubeba vitanda 261, hivyo kuchangia kupunguza vifo vya kinamama na watoto kwa kiasi kikubwa.

Vilevile, alisema vimewekwa vifaa vya kisasa, zikiwemo mashine za CT Scan, Endoscope na mtambo wa uzalishaji hewa safi.

“Zamani tulikuwa tunasafirisha mitungi kusambaza katika hospitali, sasa hivi hospitali zetu za rufaa na mikoa, zote zinazalisha oksijeni.

“Mgonjwa anayezidiwa pumzi hapati huduma, ipo palepale, kwani mashine za kisasa zinapatikana,” alisisitiza.

Kwa upande wa Hospitali ya Bugando, alisema zaidi ya sh. bilioni tisa, zimepelekwa kuboresha huduma, vifaatiba na ujenzi wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).

Pia, alisema serikali imejenga jengo la matibabu ya saratani, ikiwa ni pamoja na kununua mashine za uchunguzi wa saratani za matiti, kinamama wameanza kupata huduma za uchunguzi.

Alieleza kuwa, mashine za mionzi ya saratani, zimenunuliwa Bugando, hivyo wagonjwa wa saratani kutoka Kanda ya Ziwa, haiwalazimu kwenda Ocean Road kupata matibabu.

Kadhalika, alisema uwezo wa hospitali kuhudumia wagonjwa, umeongezeka kutoka 1,200 hadi 1,500.

“Tunataka huduma za kibingwa zote zipatikane hapa Mwanza, tupunguze rufaa kwenda Dar es Salaam. “Mkitupa ridhaa ya kuongoza nchi hii, kipekee katika kisiwa cha Ukerewe, tutaboresha Hospitali ya Nansio, kuweka majengo ya wagonjwa wa dharura,” alisisitiza.

Alisema uboreshaji huo, utahusisha ujenzi wa hospitali moja ya kibingwa wilayani humo.

“Yale ya mgonjwa kazidiwa kivuko kimeondoka, atapata huduma zote Ukerewe,” alisisitiza.

UJENZI WA SGR

Dk. Samia, alisema ujenzi wa SGR kati ya Mwanza na Isaka, utakuwa na stesheni tano, ambazo zitainua shughuli za kiuchumi za mkoa huo.

“Vilevile tutajenga maghala ya kuhifadhia bidhaa za kusafirisha mizigo. Ni muhimu kwa fursa za ajira. Ikumbukwe pia, pale Fela kuna Bandari Kavu, itakayotumika kupakia na kupakua mizigo. 

“Kwa sasa, SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma mambo safi, kuna watu wanasafiri kwa sababu ya vikao, wanarejea siku hiyo hiyo, reli hii ina manufaa makubwa sana,” alisema. 

Pia, alieleza kuwa, baada ya kukamilika, reli hiyo kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kutapunguza umbali wa safari kutoka saa 20 hadi saa nane pekee.

“SGR itarahisisha biashara. Mtu aliyekuwa akisubiri mzigo wake kwa siku mbili, ataupata siku hiyo hiyo. “Ukipakia mzigo asubuhi, jioni unaupokea. Tuchagueni tukamilishe hii kazi. Gharama za usafiri na bidhaa, zitashuka, kwa sababu bei ya bidhaa hupanda kwa usafiri kuwa juu,” alisema.

KILIMO CHA PAMBA

Pia, Dk. Samia, aliahidi kufufua viwanda vya kuchakata Pamba (Ginery) kuongezea thamani zao hilo na kupunguza kuagiza vifaa vya hospitali ikiwemo pamba na shuka.

“Tunasambaza mbegu za pamba na dawa, bure bila malipo. Vilevile tutasambaza vijana 700 wa huduma za ugani kuongeza uzalishaji. 

“Tumeagiza trekta 700 kati ya hizo, 350 zimefika, tutazisambaza kwa kulima kwa nusu bei. Tutayasambaza katika vituo vya zana za kilimo. 

“Tutafufua viwanda vya Ginery vya Sengerema, Buchosa na Manawa. Ili tuzalishe bidhaa za Pamba kwa wingi, kuna vitu vingi tunaagiza nje, hasa sekta ya afya kama pamba za kusafisha vidonda, bendeji na vitu vingine kama shuka, tunatumia fedha za kigeni kuagiza wakati pamba tunazalisha nchini,” alisema.

Aliongeza kuwa, katika Mkoa wa Simiyu, Itilima kutakuwa na kiwanda kimoja kutengeneza kamba za kufungia Tumbaku.

“Tumekifufua kiwanda cha pamba, Itilima kupata kamba za kufungia tumbaku. Kamba za tumbaku, zinatakiwa kuwa za pamba,” alisema.

MAPINDUZI ELIMU

Kwa sekta ya elimu, alieleza kuwa, mbali ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari, serikali imeendelea kutekeleza sera ya elimu bila ada.

Alisema serikali imejenga vyuo vitatu vya VETA Magu, Misungwi na Buchosa kuhakikisha kila wilaya inapata chuo cha kutoa mafunzo ya ufundi stadi kuwawezesha kumudu maisha yao.

Pia, alisema kwa upande wa elimu ya juu katika mkoa huo, imejengwa kampasi ya Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika Wilaya ya Ilemela.

Aliongeza kuwa, kampasi ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imejengwa wilayani Misungwi.

MAFANIKIO NISHATI

Dk. Samia alisema awamu ya kwanza, serikali ilitoa mitungi ya gesi kwa ruzuku kwa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Alisema mitungi hiyo, ilitolewa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama ukombozi kwa afya ya kinamama.

Alibainisha kuwa, katika maeneo ambayo bado mwitikio ni mdogo, serikali itaendelea kutoa mitungi hiyo kwa njia ya ruzuku.

MATUMIZI YA MAJI KATIKA KILIMO

Kuhusu kilimo, alisema serikali ina mpango kutumia miundombinu ya maji katika kilimo cha umwagiliaji.

Alisema fedha zaidi zitaongezwa katika mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ili kuwepo matoleo ya maji kwa umwagiliaji kama ambavyo baadhi ya nchi zinavyofanya.

Alisema kwa kipindi kirefu maji ya ziwa hayatumiki ipasavyo kuleta manufaa makubwa, hivyo serikali imeamua kutumia maji hayo kujenga gridi ya maji kitaifa na umwagiliaji.

“Lengo letu kuyaleta maji hayo hadi Dodoma ni safari ndefu ni mradi mkubwa sana kwa hiyo tunafanya hivyo kwa sababu tuna ajenda kufanya sekta ya kilimo ikuwe zaidi.

“Sasa hivi inakuwa kwa asilimia tano, tuifanye ikue kwa asilimia 10 ifikapo 2030,” alisisitiza.

MAKONDA, NYALANDU WATIKISA

Naye, Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Paul Makonda, alisema Dk. Samia alipoingia madarakani, alikuta mradi ujenzi bwawa la Mwalimu Nyerere ukiwa chini ya asilimia 30.

Alisema baada ya kuingia madarakani, ameliwezesha taifa kukamilisha mradi huo uliowezesha ongezeko la nishati ya umeme hatua ambayo serikali imeanza mchakato kuuza umeme nje ya nchi.

“Kwa sasa mipango hiyo itaifanya Tanzania kuwa nchi inayouza umeme, badala ya kuwa na mgao wa umeme. Umeme tunao wa kutosha.

“Wakati Magufuli alipokuwa Rais, alifanyakazi ya heshima sana, kiliibuka kikundi kilichotoa kila aina ya lugha chafu. Leo hii Mungu ametupa Dk. Samia, kikundi kile kile kimeibuka kumtolea kauli chafu, vijana mko wapi kumlinda Dk. Samia?” alihoji.

Makonda aliuliza swali hilo, ambalo maelfu ya wananchi waliitika wapo tayari kumlinda Dk. Samia kwa msisitizo.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema Dk. Samia, amelihakikishia Taifa kuwa na uwezo wa kuwatibu wananchi wake kupitia uboreshaji uliofanyika wa sekta ya afya.

Alisema katika kipindi cha miaka minne, serikali imejenga hospitali za wilaya zaidi ya 100 huku hospitali 113 zikiwa na uwezo wa kutibu wagonjwa wa dharura kama ajali kutoka hospitali saba.

Pia, alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi chache zenye ongezeko kubwa la madaktari bingwa.

WAGOMBEA UBUNGE

Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Kafiti William, alisema Januari 30 mwaka jana, Dk. Samia alifika katika jimbo hilo kuzindua programu za mikopo kwa wavuvi yenye thamani ya sh. bilioni mbili.

Alieleza kuwa, katika ilani ya uchaguzi 2025 – 2030, imeahidi kujenga vizimba 200 vya kufugia samaki na boti mbili za doria.

Naye, Mgombea Ubunge Viti Maalumu kundi la vijana, Ngwasi Kamani, alisema kundi la vijana limepewa kipaumbele kikubwa na Serikali ya Dk. Samia.

Kwa upande wa Mgombea Ubunge Viti Maalumu, Marry Masanja, alizitaja sababu za kumchagua Dk. Samia katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu ni namna alivyotekeleza miradi ya maji ambayo ni ajenda iliyoleta matokeo mazuri ikiwemo uanzishaji mradi wa maji chanzo cha Butimba.

Previous Post

NEEMA YAJA WAKULIMA WA MIKARAFUU ZANZIBAR

Next Post

DK. SAMIA, MWINYI WAMELETA MAENDELEO NCHINI – DK. NCHIMBI

Next Post
DK. SAMIA, MWINYI WAMELETA MAENDELEO NCHINI – DK. NCHIMBI

DK. SAMIA, MWINYI WAMELETA MAENDELEO NCHINI – DK. NCHIMBI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

16 hours ago
DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

DK. NCHIMBI : DK. SAMIA KIONGOZI WA MAJAWABU

5 days ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.