• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA : WANAWAKE TUNA UWEZO KUONGOZA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 11, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA : WANAWAKE TUNA UWEZO KUONGOZA

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Serengeti

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amevunja ukimya dhidi ya watu wenye mtizamo hasi kuhusu wanawake kushika nyadhifa za uongozi nchini.

Amesema wanawake wana uwezo mkubwa kushika nafasi za uongozi na kuleta mafanikio makubwa nchini, kwani katika miaka minne ya uongozi wake amefanya makubwa ya maendeleo ambayo hayakutarajiwa.

Dk. Samia amelazimika kutoa msimamo huo baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya watu wanaohoji uwezo wa wanawake waliopewa nafasi kugombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za uchaguzi uliofanyika wilayani Serengeti mkoani Mara, Dk. Samia alisema licha ya uwepo wa mila na desturi, umoja wa Watanzania ni suala muhimu.

“Mungu alivyotuumba hakutuumba mwenye kichwa fulani alichozaliwa nacho ana akili kuliko mwenzake. Pia hatukuambiwa mwanamke ana akili zaidi ya mwanaume au mwanaume ana akili kuliko mwanamke.

“Mwenyezi Mungu alitutofautisha katika kazi ambazo alitwambia wanawake tutabeba ujauzito na kuzaa kwa uchungu na akatuumba kwa maumbile hayo.

Amesisitiza: “Wanaume mkaambiwa nyinyi ni wasimamizi wa wanawake na mtafanya kazi kutunza familia zenu. Lakini jinsi tunavyokwenda, wanawake wanafanya kazi na kutunza familia zao.”

Dk. Samia ameyasema hayo baada ya kusikia maneno mgombea ubunge wa jimbo hilo (Marry Daniel), ambaye ni mwanamke ni kinyume cha mila na desturi za eneo hilo.

“Katika maendeleo ndugu zangu hakuna mwanamke, hakuna mwanaume. Mimi ninayesema hapa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya miaka minne nimefanya makubwa sana.

Ameongeza: “Ingekuwa mwanamke hawezi nisingeweza kuyafanya yote niliyofanya. Mungu ametuumba wote kwa akili sawa, uwezo wa kufikiri, ukiwa mwanaume unafikiri ukiwa mwanamke unafikiri.”

“Tena mwanamke ni mwaminifu zaidi na mtendaji zaidi kwa sababu ya uoga kuliko mwanaume. Nimeanza kusikia maneno mara hii CCM wametupa wagombea wanawake, kwani wanawake wana nini?,” amehoji Dk. Samia huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi.

Amesema wanawake wana uwezo mkubwa katika kuongoza taifa kwa sababu ya uaminifu.

“Nataka niwaambie, wanawake wanachapa kazi kama wengine wanavyochapa kazi. Mkoa huu (Mara) utaendelezwa na wanawake na wanaume kwa mshikamano.

“Tanzania hii itaendeshwa na kuendelezwa mambo yake na wanaume na wanawake kwa umoja wetu. Cha muhimu hapa sote ni Watanzania, sote wa taifa moja,” amefafanua.

Dk. Samia ameeleza maendeleo ya dunia hivi sasa yanachagizwa na makundi yote kushirikiana katika taaluma mbalimbali.

“Ulimwengu unajengwa na wanawake na wanaume. Kuna wanasayansi wanawake na wanaume, kuna madaktari wanawake na wanaume na unapokwenda hospitali husemi huyo daktari mwanamke asinitibu. Unatibiwa na mwanamke na mwanaume.

“Unapolindwa na askari wetu unalindwa na wanawake na wanaume au tumesema askari wetu wanawake hawafai kulinda? Wanapangwa malindo na Tanzania yetu ipo salama.

Amesisitiza: “Hata mimi (Dk. Samia) nilipoingia kuna waliobeza sitoweza, leo tunazungumza mengine.”

CCM HAITOKUBALI NCHI IYUMBE

Akiwa katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika wilayani Butiama, Dk. Samia alisisitiza CCM haitokubali nchi kuyumba kwa kisingizio chochote.

Alisema CCM inatambua umuhimu wa kuendelea kuimarisha mshikamano wa Watanzania ikiwemo kukamilisha mchakato wa katiba mpya kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi (2025-2030).

“Haya ni matakwa ya makundi ya Watanzania kwa nyakati tofauti. Tulijaribu wakati wa awamu ya nne mchakato haukukamilika, awamu ya sita tunakwenda kuendeleza mchakato huo.

“Kama walivyofanya waasisi wa taifa na chama chetu, nasi tutaendelea kulinda Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia yote hayo kwa maslahi mapana ya Watanzania.

Alisisitiza: “Baba wa Taifa letu alisema bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba. Hatukubali nchi yetu iyumbe kwa kisingizio chochote kile.”

Awali, mgombea ubunge Jimbo la Serengeti, Marry Daniel, alisema uongozi wa Dk. Samia umewezesha kuchochea uchumi wa eneo hilo unaotegemea sekta ya utalii kupitia filamu ya Tanzania Royal Tour.

Alisema Dk. Samia ameongeza fedha za kununua dawa na vifaatiba katika zahanati 58, vituo vya afya nane na hospitali mbili zilizopo wilayani hapo.

ATIMIZA NDOTO ZA MWALIMU NYERERE

Dk. Samia alisema Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere ni vigumu kumtenganisha na misingi ya falsafa aliyoijenga nchini.

Alisema misingi na falsafa hizo zilibebwa kwa dhana ya uhuru na umoja, uhuru na kujitegemea, uhuru na kazi, uhuru na wajibu na dhana nyingine muhimu za kiitikadi.

Alieleza dhana hizo alizianzisha kuleta umoja na mshikamano nchini kujenga taifa imara lenye kutegemea na kujali maendeleo ya watu.

“Maendeleo yote yenye maana hayana budi kuwalenga watu ndiyo maana dira, mipango yetu ya maendeleo pamoja na ilani za Chama Cha Mapinduzi zinajielekeza kujenga taifa linalojitegemea lenye uchumi jumuishi na ustawi wa watu,” alieleza.

Dk. Samia alisema serikali imetekeleza miradi mikubwa ya utawala bora inayotoa msukumo katika sekta za uzalishaji ambazo ni sehemu ya ndoto ya Mwalimu Nyerere.

Aliitaja miongoni mwa miradi hiyo ni utekelezaji mpango wa kuhamisha makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.

“Tuliamua miaka ile makao makuu ya nchi yetu yatakuwa Dodoma. Tumechelewa kidogo, lakini kuanzia awamu ya tano na hii ya sita tumekamilisha uhamiaji wa serikali, mihimili yote mitatu tayari ipo Dodoma, bunge lilitangulia, serikali tukafuata na mahakama mwaka 2024 ilihamia Dodoma.”

Alisema jambo lingine ambalo lilikuwa ndoto ya Mwalimu Nyerere ni ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Julius Nyerere, ambapo alitaka bwawa hilo lijengwe kipindi chake lakini hali haikuruhusu, hata hivyo serikali imekamilisha mradi huo.

Mradi mwingine alioutaja ni wa maji Same-Mwanga ambako Mwalimu Nyerere alijenga bwawa la Nyumba ya Mungu, lakini alishindwa kuliendeleza.

Alisema serikali imeendeleza mradi huo na kuukamilisha ambapo hivi sasa wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe wanapata huduma za maji.

Alitaja mabwawa mengine ambayo Hayati Mwalimu Nyerere alitaka yajengwe ni bwawa la Mkomazi lililopo Korogwe ambalo limefikia asilimia 50 na Kidunda ambalo lingesaidia maji mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

“Zile ndoto za Mwalimu Nyerere za utawala bora, sekta za uwezeshaji wananchi kiuchumi na maendeleo ya jamii ndiyo haya ambayo tunaendelea kutekeleza.

“Baba wa Taifa alituachia misingi mizuri kifalsafa, kisera na kisiasa. Kazi yetu ni kutafsiri misingi ile na fikra zile katika mazingira ya hivi sasa,” alieleza.

Dk. Samia alisema serikali itaendelea kudumisha tunu za amani, umoja, mshikamano wa taifa na Muungano.

Previous Post

WASIRA ANYOOSHEA KIDOLE WATU WENYE CHOKOCHOKO

Next Post

DK. SAMIA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

Next Post
DK. SAMIA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

DK. SAMIA KUWAINUA WANANCHI KIUCHUMI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TUNAMWOMBEA KURA DK. SAMIA, WATANZANIA NI MASHAHIDI – WASIRA

TUNAMWOMBEA KURA DK. SAMIA, WATANZANIA NI MASHAHIDI – WASIRA

1 month ago
DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.