Na MWANDISHI WETU,
DODOMA
MKUTANO wa kwanza wa Bunge la 13 unatarajiwa kuanza rasmi kesho, Novemba 11, 2025, jijini Dodoma.
Mkutano huo unafanyika baada ya kukamilika kwa shughuli za Uchaguzi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Bunge hilo kupitia tangazo lililotolewa katika Gazeti la Serikali.
Kupitia tangazo hilo, wabunge wateule walipewa nafasi ya kujisajili kuanzia Novemba 8 hadi 10, 2025, ambapo zoezi hilo linakamilika leo, Novemba 11, 2025.
Pamoja na mambo mengine, kuanza kwa mkutano huo kutaambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo kuapishwa kwa wabunge wateule, uchaguzi wa Spika na Naibu Spika wa Bunge, kuthibitishwa kwa jina la Waziri Mkuu, pamoja na uzinduzi rasmi wa Bunge hilo jipya.




