• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MKENDA AANIKA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA ELIMU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 11, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MKENDA AANIKA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA ELIMU

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetangaza kuwa mtaala mpya wa elimu utaanza kutumika rasmi mwaka 2028, hatua inayolenga kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza sekondari kuajiriwa au kujiajiri moja kwa moja.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema mageuzi hayo ni sehemu ya maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyesisitiza umuhimu wa mfumo wa elimu kuendana na mahitaji halisi ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Profesa Mkenda amesema mtaala huo mpya utatoa nafasi kwa wanafunzi kuchagua mkondo wa elimu ya jumla au elimu ya amali, wanapoanza sekondari, tofauti na mfumo wa sasa unaowalazimu wote kusoma muundo mmoja wa masomo.

Amefafanua lengo ni kumjengea mwanafunzi ujuzi wa moja kwa moja unaomwezesha kufanya kazi au kuanzisha shughuli za uzalishaji mali anapohitimu elimu ya sekondari bila kusubiri elimu ya juu.

“Mfumo wa sasa wa 7+4+2+3 umeanza kutumika miaka ya 60, baada ya maelekezo ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere kati ya 1965 na 1968 yaliyolenga kubadili mfumo wa miaka minne, minane au 12. Mageuzi yale yalifanikiwa, na sasa tunafanya mageuzi makubwa tena chini ya uongozi wa Rais Samia,” amesema.

Amesema mfumo mpya utakuwa 6+4+2(3)+3, ambapo elimu ya msingi itakuwa miaka sita pekee, na mwanafunzi atakapohitimu darasa la sita atalazimika kuendelea na elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kwa mujibu wa sheria.

“Hawa walioko darasa la tatu, mwaka 2027 watakapofika darasa la sita ndiyo watakaoanza mfumo huu mpya. Lengo ni kujenga taifa lenye vijana wenye ujuzi, uwezo wa kubuni miradi na kukabiliana na ushindani wa ajira hata katika ngazi za kimataifa,” ameeleza.

MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Waziri huyo akizungumzia mikopo ya elimu ya juu, alisema imeongezeka asilimia 40, kutoka sh. bilioni 464 mwaka wa masomo 2021/2022 hadi sh. bilioni 916.7 kwa sasa.

Profesa Mkenda alisema ongozeko hilo limetokana na baadhi ya mikopo kuingizwa kwa vijana wanaosoma vyuo vya kati, pia kuongozeka kwa uboreshaji wa miundombinu ya Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA).

“Wakati Rais Dk. Samia anaingia madarakani, tulikuwa na mikoa mitano haina vyuo vya VETA vyenye hadhi ya mkoa, sasa tumejenga katika mikoa ya Geita, Simiyu, Njombe, Rukwa na Mkoa wa Songwe ujenzi unaendelea.

“Tulikuwa na Wilaya 64 ambazo hazina vyuo vya VETA, sasa tunajenga. Niwaambie tu vijana sasa hivi ukichukuliwa na serikali katika chuo cha VETA, unakula na kulala hapo, ada yake ni sh. 120,000, ukiwa unatokea nyumbani ada yake ni sh. 60,000,” alisema.

MASOMO YA SAYANSI

Prefesa Mkenda, alisema ili nchi iendelee lazima uwekezaji mkubwa ufanyike katika maeneo muhimu husan Sayansi, Teknolojia na ubunifu, kwa kulitambua hilo serikali imeweka msisitizo zaidi kwa wanafunzi katika kusoma masomo hayo ya sayansi.‎

‎Alisema chini ya maelekezo ya Rais Dk. Samia, kila mkoa umejengewa shule ya sekondari ya wasichana ya sayansi huku mkakati ukiwa kujengwa nyingine za wanaume.‎

‎Aliongeza kuwa, maagizo ya Rais yanataka vijana wote wenye uwezo wa kusoma masomo ya sayansi wasomeshwe kwa gharama za serikali.

WATAALAMU WA AI

Prefesa Mkenda alisema kwa kutambua kasi ya matumizi ya akili unde (Artificial intelligence) katika maeneo mbalimbali, ukiwemo usalama wa nchi, kilimo na sekta nyingine za uchumi, serikali imeamua kuanza kufundisha masomo yanayohusiana na eneo hilo.

“Eneo jingine kubwa ambalo kwa hakika dunia inaenda kwa kasi sana wanaita akili unde, yaani akili iliyoundwa, Artificial intelligence, mambo ya data sayansi, na maeneo kama hayo, dunia inaenda kwa kasi sana hata maswala ya usalama wa nchi, uchumi ‘banking’ (benki), kilimo, kinaenda kutegemea sana masuala ya akili unde” alifafanua.

Waziri huyo alisema hadi sasa vijana 50 wamechukuliwa kupelekwa katika kambi ya mafunzo, inayowaanda kwa kujifunza mambo mbalimbali, baadaye wapelekwe wakasome nje ya nchi kwa uratibu wa serikali.

Previous Post

MSAMAHA WA RAIS DK. SAMIA WAGUSA WAFUNGWA WAZEE, WENYE UJAUZITO

Next Post

MOGELLA, MTEMI WAMKINGIA KIFUA GAMONDI KIKOSI STARS

Next Post
MOGELLA, MTEMI WAMKINGIA KIFUA GAMONDI KIKOSI STARS

MOGELLA, MTEMI WAMKINGIA KIFUA GAMONDI KIKOSI STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

DK. SAMIA ASEMA MIAKA MITANO IJAYO, SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YAO

6 months ago
RAIS DK. SAMIA AIPAISHA TANZANIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

RAIS DK. SAMIA AIPAISHA TANZANIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

1 week ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?