• ePaper
Sunday, May 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MOGELLA, MTEMI WAMKINGIA KIFUA GAMONDI KIKOSI STARS

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 11, 2025
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
MOGELLA, MTEMI WAMKINGIA KIFUA GAMONDI KIKOSI STARS

KOCHA wa Taifa Stars Miguel Gamondi

0
SHARES
16
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ABDUL DUNIA

WACHEZAJI wa zamani wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, wamemkingia kifua kocha wa kikosi hicho, Miguel Gamondi kutokana na kile kinachodaiwa ameita wachezaji wengi wa nafasi ya ulinzi (mabeki) kuliko viungo na washambuliaji kwa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Michuano ya AFCON 2025 inatarajiwa kufanyika Desemba 21 hadi Januari 18, mwaka huu nchini Morocco ambapo Stars imepangwa kundi C na timu za Uganda, Nigeria na Tunisia.

Katika michuano hiyo, Gamondi amewaita wachezaji 28 ambapo makipa watatu, mabeki 10, viungo saba na washambuliaji wanane.

KIKOSI CHA TAIFA STARS

Wakati wakipa ni Yakoub Suleiman, Hussein Masalanga na Zuber Foba, mabeki ni Bakari Mwamnyeto, Shomari Kapombe, Lusajo Mwaikenda, Mohamed Hussein, Nickson Kibabage, Wilson Nangu, Pascal Msindo, Ibrahim Bacca, Haji Mnoga na Dickson Job.

 Viungo wanaounda timu hiyo ni Morice Abraham, Feisal Salum, Yusuph Kagoma, Habib Idd, Kelvin Nashon, Novatus Dismas na Alphonce Mabula huku washambuliaji ni Mbwana Samatta, Simon Msuva, Kelvin John, Kibu Denis, Idd Nado, Abdul Sopu, Charles M’mombwa na Tarryn Allarakhia.

MOGELLA, MTEMI WALONGA

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wachezaji wa zamani wa Taifa Stars, wamesema kwamba, hawajaona tatizo katika kikosi kilichoitwa na Gamondi kwa fainali hizo.

Aliyekuwa nyota wa Simba na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella, alisema anaamini Gamondi ana mpango madhubuti ambao utasaidia katika fainali hizo.

“Ni mpango mkakati wake, naamini kuna kitu anataka kuona, binafsi sioni tatizo katika hilo ninaamini mwalimu kuna kitu kakiona na ndiyo maana kafanya hilo chaguo,” alisema.

“Taifa Stars ya sasa ni bora na soka limebadilika, sasa mpira wa miguu ni sayansi zaidi, hivyo naamini kila kitu kitakuwa sawa,” aliongeza.

Mtemi Ramadhani ambaye pia aliwahi kukipiga Taifa Stars, alisema anaamini Gamondi ana mpango mzuri ambao utaiongoza timu hiyo kufanya vyema katika AFCON.

“Ninafikiri mwalimu anajua nini anakifanya, pengine anahitaji kuingia na mpango wa kujilinda zaidi katika mechi ngumu, lakini naamini kabisa kikosi kilichoitwa ni kizuri kwa mashindano,” alisema.

KUFUZU MARA NNE AFCON

Katika kundi hilo, Taifa Stars ndiyo timu iliyofuzu fainali hizo mara chache (4), Tunisia mara 22, Nigeria mara 21 wakati Uganda ikitinga mara nane.

Katika kundi hilo, Taifa Stars ndiyo timu pekee ambayo haijawahi kupenya hatua ya mtoano wakati Nigeria ikiwa ni bingwa mara tatu mwaka 1980, 1994 na 2013, Tunisia mara moja mwaka 2004 huku Uganda ikiwahi kushika nafasi ya pili mwaka 1978.

Katika fainali zote tatu zilizopita ambazo Stars ilishiriki, timu hiyo haijawahi kutinga hatua ya mtoano hata mara moja.

MATOKEO

Katika michuano ya mwaka 1980 iliyofanyika Nigeria, Taifa Stars ilipangwa kundi A na timu za Nigeria, Misri na Ivory Coast.

Taifa Stars iliburuta mkia kwa pointi moja baada ya kutoka sare na Ivory Coast. Awali, ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya Nigeria na mabao 2-1 ilipovaana na Misri.

Katika AFCON mwaka 2019 zilizofanyika nchini Misri, Tanzania ilipangwa kundi C na timu za Algeria, Senegal na Kenya.

Taifa Stars ilimaliza katika kundi hilo ikiwa nafasi ya nne baada ya kufungwa mechi zote tatu.

Kikosi hicho kilikuwa kikinolewa na Amunike, kilianza kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Senegal, kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Kenya na kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.

Pia, Taifa Stars iliburuta mkia katika hatua ya makundi ya AFCON mwaka 2023 zilizofanyika nchini Ivory Coast.

Ikiwa imepangwa kundi F, Stars ilivuna pointi mbili (nyingi zaidi ya AFCON ilizoshiriki awali), ikianza kwa kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Morocco, sare ya bao 1-1 kutoka kwa Zambia na suluhu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Previous Post

MKENDA AANIKA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA ELIMU

Next Post

MCHUJO MKALI  KOCHA SIMBA

Next Post
MCHUJO MKALI  KOCHA SIMBA

MCHUJO MKALI  KOCHA SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

8 months ago
KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

KOFANE ALIVYOANDIKA HISTORIA CAMEROON AFCON MSIMU HUU

4 months ago

Popular News

  • MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?