• ePaper
Saturday, June 27, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home AFYA

BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 13, 2026
in AFYA, Habari, Kitaifa
0
BEHEWA LA AFYA LAIBUA WADAU
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

BAADHI ya wadau wa sekta ya afya, wamepongeza hatua ya serikali ya kutaka kuanzisha behewa maalumu la afya katika treni ya kisasa (SGR), hatua ambayo itaboresha huduma za dharura na kuimarisha usafirishaji salama wa wagonjwa nchini.

Pia, wamesema uwepo wa behewa hilo, utakuwa suluhisho muhimu kwa changamoto za kiafya zitakazojitokeza ghafla wakati wa safari, kutoa fursa kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wakati wa kusafirishwa katika mazingira salama zaidi.

Wamesema hayo kwa nyakati tofauto, juzi, walipozungumza na gazeti hili kuhusu kuanzishwa kwa behewa hilo katika SGR.

DK. TULIZO SHEMU

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Tulizo Shemu, alisema hatua ya serikali ya kuanzisha behewa maalumu la afya katika treni ni jambo muhimu litakalosaidia kuimarisha huduma za dharura kwa wasafiri.

Dk. Shemu, ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group, alisema usafiri wa treni, hubeba idadi kubwa ya abiria, hivyo uwepo wa huduma za afya ndani ya treni ni muhimu kwani siyo kila msafiri anaweza kufahamu hali yake ya afya kabla ya kuanza safari.

Alisema baadhi ya wasafiri hupata changamoto za afya wakiwa safarini, ikiwemo maumivu ya ghafla ya tumbo, kuharisha na matatizo mengine yanayohitaji msaada wa haraka, hivyo behewa hilo litasaidia kutoa huduma za awali bila kulazimika kusubiri hadi safari iishe.

Mkurugenzi huyo, alisema kwa safari ndefu zinazotarajiwa kufanyika kwenda maeneo mbalimbali nchini, huduma hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa abiria watakaohitaji uchunguzi na matibabu ya haraka wakiwa safarini.

Aliongeza kuwa, behewa hilo litasaidia kusafirisha wagonjwa kwa usalama zaidi, hususan wale wanaopelekwa kupata matibabu katika hospitali mbalimbali, kutokana na uwepo wa wataalamu wa afya ndani ya treni.

“Kuanzishwa kwa behewa maalumu la afya ndani ya treni ya SGR ni hatua muhimu itakayosaidia kutoa huduma za dharura kwa wakati, siyo kila mgonjwa anaweza kufahamu au kuripoti changamoto yake ya afya kabla ya safari. Hii itasaidia kuokoa maisha na kuhakikisha usafiri unakuwa salama zaidi kwa abiria wote,”alisema.

DK. ERICK KIMARO

Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Erick Kimaro,  alisema wagonjwa wengi hupata changamoto wanapotumia usafiri wa kawaida kutokana na mazingira yasiyo rafiki kwa hali zao za afya, hivyo huduma hiyo mpya, itawawezesha kupata uangalizi wa karibu kutoka kwa wataalamu wakati wa safari.

Alisema baadhi ya wagonjwa hushindwa kukaa muda mrefu safarini katika mabasi au magari ya kawaida, jambo linaloweza kuhatarisha afya zao kabla ya kufika hospitali.

“Hatua hii ni muhimu kwani wagonjwa watakuwa katika uangalizi mzuri zaidi na kupata huduma maalumu kwa ajili yao.

“Njia zote za usafiri ni muhimu, hivyo ni vyema kuendelea kuboresha mifumo mbalimbali wagonjwa wafike kwa wakati na kupata huduma kwa urahisi zaidi,” alisema.

DK. DANIEL MAGOMERE

Mbobezi wa Afya ya Umma na Mkurugenzi wa taasisi ya Health Status, Dk. Daniel Magomere, alisema hatua hiyo, maendeleo na itasaidia kuboresha mfumo wa rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya juu kutoka mikoa mbalimbali kwenda hospitali za rufaa.

Alisema ipo haja ya kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuanzisha huduma za ‘ambulance za anga’ na helikopta, kuongeza uwezo wa kuwahudumia wagonjwa wa dharura kwa haraka zaidi.

“Naipongeza serikali kwa jitihada hii kwa sababu haina vikwazo wala foleni, inaongeza nafasi ya kuokoa maisha ya watu.

“Ninaiomba serikali isiishie katika ‘ambulance za treni’ pekee, bali ifike hatua ya kuwa na ‘air ambulance’ na helikopta kwa  wananchi wanaohitaji msaada wa dharura,” alisema.

Hivi karibuni, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, alisema wizara hiyo ipo katika hatua za majadiliano na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhusu mpango wa kuanzisha behewa maalumu la ‘ambulance’ ndani ya treni ya SGR, kutoa huduma za afya kwa abiria wanapokuwa safarini.

Previous Post

IDADI WAGONJWA AFYA YA AKILI TISHIO

Next Post

POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI

Next Post
POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI

POLISI WAPATA SEHEMU YA KICHWA CHA JAMES TEMBA, MGANGA WA KIENYEJI MBARONI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

HISTORIA ELIMU MSINGI YAANDIKWA

HISTORIA ELIMU MSINGI YAANDIKWA

5 months ago
KOCHA SERENGETI BOYS AKOSHWA NA KIWANGO

KOCHA SERENGETI BOYS AKOSHWA NA KIWANGO

7 months ago

Popular News

  • HAKUNA MJADALA AMANI, USALAMA WA NCHI-MWIGULU

    HAKUNA MJADALA AMANI, USALAMA WA NCHI-MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA SIKU YA KILIO,KICHEKO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VIJANA 400  WAAGWA KWENDA KUFANYA KAZI NJE YA NCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‘NAFUU YA MAFUTA KUANZA KUONEKANA JULAI’ NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZOTE KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL-NINO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?