• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BALOZI KUSILUKA ATAKA TAARIFA POTOFU ZIJIBIWE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 18, 2025
in Habari, Kitaifa
0
BALOZI KUSILUKA ATAKA TAARIFA POTOFU ZIJIBIWE

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na IRENE MWASOMOLA

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, amewata Maofisa Habari wa Serikali, kutumia vizuri teknolojia ya habari  na kutoa ufafanuzi   kwa wakati pindi zinapotokea taarifa za upotoshaji.

Amesema teknolojia ya habari imebadilika kwa kasi kubwa, hivyo inaweza kutumiwa na maadui kuhatarisha usalama wa nchi kama haitatumiwa vizuri.

Balozi Dk. Kusiluka aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, alipofungua mkutano wa kikao kazi cha Kitaifa cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Maofisa Habari wa Serikali.

“Nilazima Maofisa Habari kuhakikisha mnajipanga vizuri kuitumia teknolojia ya habari, ili kuleta maendeleo ya nchi,” alifafanua na kuhoji:

“Sisi ni jeshi la Serikali,  inakuwaje  wakati mwingine tushambuliwa wakati sisi (Maofisa Habari) tumekaa?”

Alisema ni matarajio ya serikali kuona Maofisa Habari watajipanga vizuri katika kukabiliana na matumizi hasi ya teknolojia ya habari.

Aidha Balozi Dk. Kusiluka aliwaagiza Maofisa Habari kuhakikisha wanakua na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia utekelezaji wake ndani ya taasisi zao na kutoa taarifa kwa umma.

Vilevile aliwataka wahakikishe wanakuwa washauri wazuri kwa viongozi wao katika utekelezaji wa mikakati ya taasisi zao.

Pia, Balozi Dk. Kusiluka aliwataka Maofisa Habari kuendelea kuzingatia miiko na maadili ya taaluma katika utekelezaji wa majukumu yao.

MSIGWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa alisema, kikao kazi hicho kinafanyika kwa siku mbili kuanzia jana hadi leo kitasaidia kukumbushana na kuongeza maarifa kwa Maofisa Habari.

Alisema kikao kazi hicho kimehudhuliwa na Maofisa Habari wa Serikali, Taasisi za Umma na vyombo vya usalama zaidi ya 500.

TIDO

Mshauri wa Rais Habari na Mawasiliano, Tido Mhando, alisema ni dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuona Maofisa Habari wanatoa taarifa sahihi na kwa uzalendo.

Alisema Serikali katika kuhakikisha inaboresha sekta ya habari, Rais Dk. Samia   alianzisha Tume ya Kuangalia maslahi ya Vyombo vya Habari, Bodi ya Ithibati na kufanya uteuzi wa Mshauri wa Rais  Habari na Mawasiliano.

Aidha Mhando alisema ni matarajio yake kwamba, Maofisa Habari wataendelea kuwa daraja zuri kati ya serikali na wananchi na kumsaidia Rais Dk. Samia.

MACHUMU

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, alisema Maofisa Habari wa Serikali na taasisi za umma ni daraja la heshima kati ya Serikali na wananchi, wakiongozwa na utu na 4R. Alisema kikao kazi hicho kinachoendelea kufanyika leo kinatumika kuwakumbusha Maofisa Habari wa Serikali wajibu wao wa kujifunza na kutumia wingi wao kama mtaji wa taifa katika kutoa taarifa sahihi na kwa wakati.

Previous Post

WAZIRI KOMBO NA PROF. KABUDI WAITEMBELEA KAMBI YA TAIFA STARS

Next Post

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

Next Post
MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAPOMBE AFUNGUKA STARS

KAPOMBE AFUNGUKA STARS

3 months ago
DK. NCHIMBI : KUMBUKIZI ZA MAJIMAJI ZIWE CHACHU YA UZALENDO NA UWAJIBIKAJI

DK. NCHIMBI : KUMBUKIZI ZA MAJIMAJI ZIWE CHACHU YA UZALENDO NA UWAJIBIKAJI

3 weeks ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?