• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NONDO ZA RAIS SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 9, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NONDO ZA RAIS SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema mabadiliko ya viongozi wa serikali, yanalenga kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu ya taifa, kuimarisha uwajibikaji, kuhakikisha mipango ya maendeleo inaendana na matarajio na mahitaji ya wananchi.

Aidha, aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uwajibikaji, akisisitiza dhamira ya serikali ni kutekeleza Dira ya Maendeleo ya miaka 25 ijayo, kuelekea Tanzania ya mwaka 2050.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua jijini Dar es Salaam, Rais Samia, aliwapongeza kwa kuaminiwa kutokana na uwezo, uzoefu na uadilifu wao.

Aliwataka waishi na kuzingatia viapo walivyoapa, kikiwemo cha uadilifu na maadili ya uongozi wa umma.

“Nawataka mkaishi na viapo hivi, siyo vya leo tu, bali viwe sehemu ya maisha yenu ya utumishi. Kiapo cha maadili mlichosaini, mtakirudia mara kwa mara kujikumbusha wajibu wenu kwa taifa.

“Kazi yetu ni kuweka msingi imara wa taifa letu. Tanzania itaendelea, serikali itaendelea, na kila mmoja wetu, anatakiwa kucheza nafasi yake.

“Hatutaki mtu ambaye hatua zake haziendani na mwelekeo wa maendeleo tunayopiga,” alisema Rais Dk. Samia.

Rais Samia aliwahakikishia Watanzania mabadiliko ya uongozi hayamaanishi kuyumba kwa serikali, bali ni sehemu ya kuboresha utendaji kazi, huku akiwataka wananchi, kupuuza upotoshaji na kuendelea kuiunga mkono serikali katika safari ya maendeleo.

“Mabadiliko haya ni jitihada za kuongeza nguvu ya utekelezaji, kuimarisha uwajibikaji kulinganisha majukumu ya viongozi na vipaumbele vya taifa letu.

“Lengo letu ni kuhakikisha shughuli za serikali zinaendana na kasi na matarajio ya wananchi,” alisema Rais Dk. Samia.

Katika maelekezo yake, Rais Samia aliwataka viongozi aliowateua, kushirikiana kwa karibu na waliowakuta, akisisitiza mshikamano wa utendaji kazi, hasa mikoa ya kimkakati kwa usalama na uchumi wa nchi.

DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Akizungumzia utekelezaji wa mipango ya taifa na Dira ya Maendeleo 2050, Rais Samia, alisema serikali itachangia asilimia 22 ya utekelezaji wa shughuli za uchumi, sekta binafsi asilimia 70, huku mashirika ya umma, yakichangia asilimia nane, akasisitiza umuhimu wa kufungua milango kwa wawekezaji.

Alisema Dk. Tausi Mbaga, amempa ‘kofia’ mbili ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, hatua inayolenga kuhakikisha upangaji mipango na utekelezaji wake, vinaenda pamoja.

Rais Samia, alisema uamuzi huo, umetokana na umuhimu wa kuwa na mwelekeo mmoja wa kitaasisi, ili kinachopangwa kama sera na mkakati ndani ya wizara, kilingane moja kwa moja na utekelezaji wake kupitia Tume ya Mipango.

Alisema kwa kuwa mhusika ni mmoja katika upangaji na utekelezaji, hakutakuwa na mianya ya kuchelewesha au kupishanisha majukumu, hatua itakayosaidia serikali kwenda kwa kasi inayolingana na matarajio ya wananchi na malengo ya taifa.

“Sekta binafsi ndiyo injini ya uchumi wetu. Nataka mfungue milango kwa wawekezaji waje wawekeze. Wasiwahi kuja halafu tukawafungia mlango. Tukiwawezesha, tutafikia malengo yetu ya ukuaji uchumi,” alisema.

Rais Samia, alisisitiza viongozi waliopo wamekuwa sehemu ya maandalizi ya Dira ya Taifa, hivyo wana wajibu mkubwa wa kusimamia utekelezaji wake kwa ufanisi, kwa kuwa, wanafahamu kwa undani malengo na mikakati yake.

Pia, Rais Samia, alimtaka Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Emmanuel Tayari, kusimamia kwa karibu shughuli zote za ujenzi na uendelezaji wa viwanda vya dawa nchini na wawekezaji wake, ili ifikapo mwaka 2030, Tanzania ijitegemee angalau asilimia 80 katika uzalishaji wa dawa na vifaatiba.

 “Najua unaweza kusimamia viwanda vya dawa na wawekezaji. Nenda kasimamie, nenda ukaelewe wanaowekeza ni kina nani. Watu wengi wana hamu ya kuja kuwekeza, lakini wanakwazwa na masuala ya ardhi na ukiritimba wetu.

“Nataka ukasimame, kuhakikisha viwanda vya dawa vinajengwa ndani ya nchi yetu, ifikapo mwaka 2030, tujitegemee kwa si chini ya asilimia 80,” alisema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia, alimtaka Tayari kusimamia kikamilifu mchakato wa ujenzi wa viwanda vya dawa, kuondoa vikwazo vinavyokwamisha uwekezaji na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.

Vilevile, Rais Samia, aliainisha sekta za kimkakati zikiwemo za viwanda, uwekezaji, maji, mazingira, mifugo, uvuvi na kilimo, akisema ndizo zitakazobeba ajira za vijana na kuongeza mapato ya taifa endapo zitasimamiwa kisayansi na weledi.

“Mifugo, uvuvi na kilimo ni sekta zenye uwezo mkubwa wa kuchukua vijana wengi na kuleta mapato ya haraka.

“Lazima tubadilike, tusimamie vizuri rasilimali zetu na kuhakikisha tunafaidika kikamilifu na masoko ya kimataifa,” alisisitiza.

Pia, Rais Samia, alisisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya mazao na rasilimali kabla ya kuuza nje, hususan katika sekta ya mifugo na uvuvi, akibainisha kuwa mabadiliko ya sera na sheria yatafanyika kulinda maslahi ya taifa.

Akizungumzia uamuzi wa kuwateua wasaidizi wake kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, Rais Samia, alisema unalenga kuwapa nafasi ya kuonesha vipaji vyao vya uongozi.

Alisema baada ya kufanya vizuri wakiwa Ikulu, amekuwa na utaratibu wa kuwapa nafasi kuonesha vipaji vyao na kusaidia shughuli za maendeleo serikalini.

Rais Samia, alidokeza waliokuwa wasaidizi wake Ikulu, wameendelea kufanya vizuri, baada ya kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali.

“Waziri umefanya kazi nzuri sana, lakini kazi yangu ni kulea na kukuza, si kulea na kudumaza, ndiyo maana wengi niliowalea nawatoa nawapa posti nendeni kafanyeni, nasukuma vipaji mbele,”alisema Rais Dk. Samia.

Hivi karibuni, Rais Samia alifanya mabadiliko ya muundo wa Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Nishati kwa wizara hizo kuwa na makatibu wakuu wawili kwa kila wizara.

Pia, aliteua na kufanya uhamisho wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni wakuu wa mikoa, Kanali Yahya Kido, aliyeteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, akichukua nafasi ya Fatma Mwassa.

Pia, Kanali Donald Msengi, aliteuliwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akichukua nafasi ya Kanali Patrick Sawala, ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Vilevile, Rais Samia, alimteua Dk. Tausi Kida kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango na Dk. Fred Msemwa kuwa, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Uwekezaji.

Taarifa hiyo, ilisema Balozi Waziri Rajab Salum, aliteuliwa kuwa, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Balozi Salum anachukua nafasi ya Dk. Hashil Twaib Abdallah, ambaye atapangiwa majukumu mengine,” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. James Mataragio, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme na nishati jadidifu.

MAKATIBU TAWALA MIKOA

Pia, Rais Samia, alimteua Dk. Toba Nguvila kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha. 
“Dk. Nguvila anachukua nafasi ya Missaile Musa ambaye

amestaafu,” alisema.

Wengine walioteuliwa ni Dk. Stephen Nindi kuwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe na atachukua nafasi ya Judica Omary ambaye amestaafu.

NAIBU MAKATIBU WAKUU

Vilevile, Nsubili Akomeligwe Kajela Joshua, aliteuliwa kuwa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia huduma za Hazina na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenifa Omolo ambaye aliteuliwa kuwa, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana.

Pia, Aristides Mbwasi, aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara na anachukua nafasi ya Dk. Suleiman Hassan Serera, atakayepangiwa majukumu mengine.

“Rais Samia, alimteua Profesa Mohammed Sheikh kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya uvuvi. Aidha, Dk. Edwin Mhede aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo atapangiwa majukumu mengine,” ilisema.

Taarifa hiyo, ilisema Rose Ambrose, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji huku Emmanuel Tayari, akiteuliwa kuwa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, anayeshughulikia masuala ya dawa na vifaatiba.

“Profesa Peter Msoffe amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda kuwa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya maendeleo ya mazao na usalama wa chakula, akichukua nafasi ya Dk. Stephen Nindi, ambaye ameteuliwa kuwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema Dk. Fabian Madele, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayeshughulikia mifugo, huku Balozi Baraka Luvanda, akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira.

“Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Sosthenes Kewe, ameteuliwa kuwa, Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Taifa ya Mipango anayeshughulikia masuala ya ufuatiliaji na tathmini. Kewe anachukua nafasi ya Dk. Linda Ezekiel ambaye atapangiwa majukumu mengine,” ilifafanua taarifa hiyo.

Aidha, Balozi Meja Jenerali Marco Gaguti, aliteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo.

MWENYEKITI WA BODI

Pia, Rais Samia, alimteua Dk. Hassan Mahmoud Mshinda, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Previous Post

UKWASI MIFUKO HIFADHI YA JAMII NCHINI, WAPAA

Next Post

DK. NCHIMBI AGUSIA UJIO WA FURSA ZA AJIRA

Next Post
DK. NCHIMBI AGUSIA UJIO WA FURSA ZA AJIRA

DK. NCHIMBI AGUSIA UJIO WA FURSA ZA AJIRA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

2 weeks ago
NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

1 month ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?