• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KWA GAMONDI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 17, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
MAAGIZO YA RAIS DK. SAMIA KWA GAMONDI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na AMINA KASHEBA

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa Kocha wa Taifa ‘Taifa Stars’Miguel Gamondi kama kuna kijana  Mtanzania ana kipaji na anafanya vizuri kule alipo, amuite kuja kuchezea timu hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda  katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, alipozungumza maelekezo aliyopewa na Rais Dk. Samia, baada ya tukio la kutia saini mkataba wa kocha huyo.

“Maelekezo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mwambie Gamondi kama kuna kijana wa Kitanzania kokote duniani amlete hapa  katika taifa lake kwa lengo la kujiunga na kikosi, ili timu ifanye vizuri na kombe la AFCON 2027 libaki nchini.

“Kocha  Gamondi amepewa uwanja mpana zaidi pale anapoona kijana yupo Hispania, Uarabuni, Marekani ama nchi yoyote,  lakini ni Mtanzania ana kipaji na anafanya vizuri kule alipo, Rais ametupa kibali cha kuwaita wote kuja kuchezea timu yao ya taifa,”amesema.

Katika hafla hiyo, Makonda alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji  Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa pamoja na Rais wa Shirikisho la Miguu wa Miguu  Tanzanía (TFF) Walace Karia alisema kocha huyo anatakiwa kuanza kuandaa programu za kuwanoa wachezaji kuelekea mashindano ya AFCON 2027.

Waziri huyo alifafanua kwamba Gamondi alifanya vizuri katika mashindano ya AFCON yaliyofanyika nchini Morocco na timu kumaliza hatua ya 16 na kuonesha kiwango kikubwa, ndiyo maana wamempatia fursa ya kukinoa kikosi cha Stars kuelekea AFCON 2027.

“Wote tumeshuhudia Gamondi alipewa timu ndani ya muda mchache, lakini mabadiliko yalionekana na wachezaji walifika hatua ya 16 na kuacha historia kubwa pale nchini Morocco, hivyo serikali imeona ipo haja ya kumpatia mkataba wa kuinoa Stars atahudumu ndani ya miaka miwili.

“Gamondi anapaswa kufahamu serikali imewekeza fedha kwake, hivyo anatakiwa kukinoa vyema kikosi ili kifanye vizuri na kubakisha kombe nyumbani, pia kupanda viwango sio CAF hadi FIFA,” alisema.

Makonda alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwapa furaha Watanzania wote na kusisitiza  haiwezekani mashindano ya AFCON 2027 yaandaliwe nchini halafu Tanzania iwe ya kwanza kutoka.

Waziri huyo alisema fedha za malipo za mishahara ya  kocha huyo, zitalipwa na serikali chini ya Rais Dk. Samia hivyo anahitaji kikosi hicho kinolewe vizuri na kufanya vizuri katika mashindano yanayokuja.

Rais wa TFF, Walace Karia alishukuru serikali kwa uwekezaji mzuri wa miundombinu na sapoti kubwa katika michezo hasa mpira wa miguu.

“Tunashukuru serikali kwa sapoti kubwa katika michezo hasa soka, kama shirikisho tutafanya kazi kwa bidii na kufanya mchezo huu kuwapa watu furaha na kupeperusha vyema bendera ya taifa,” alisema.

Kocha, Gamondi alisema anajisikia fahari kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na kuahidi kushirikiana na taasisi mbalimbali kuhakikisha Stars inapanda viwango katika mpira wa miguu duniani.

“Nashukuru kwa kuwa kocha mkuu wa Stars, nimefurahi naipenda Tanzania nitahakikisha nashirikiana vizuri na taasisi za soka nchini ili timu ifanye vizuri na kuonesha soka bora na kupanda viwango Afrika na duniani nzima,” alisema kocha huyo.

Wakati huo huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kufanya kikao na vyama vya michezo mbalimbali kujadili namna ya kufanya vizuri kimataifa.

Akizungumza Dar es Salaam, Waziri huyo alisema wanahitaji kuona vyama na mashirikisho hayo ya michezo mingine kuhakikisha yanafanya vizuri kama ilivyo TFF.

Alisema Tanzania kuna michezo mingi ambayo inapaswa kufanya vizuri na kupeperusha bendera ya taifa katika mashindano ya kimataifa.

“Natoa maagizo kwa BMT kukaa na kufanya kikao na vyama na mashirikisho ya michezo kujadili namna gani wanaweza kufanya vizuri katika ngazi ya kimataifa.

“Tunahitaji kushinda medali na makombe kwani kuna michezo mingi ambayo inapaswa kufanya vizuri na kuwapa furaha Watanzania,” alisema.

Waziri huyo alisema kuna vijana wengi mtaani wana vipaji hivyo viongozi wa vyama na mashirikisho wanatakiwa kuliangalia jambo hilo.

“Kama kuna kiongozi wa chama au shirikisho ambaye anagombea uongozi kila wakati ukifika halafu mchezo huo haufanyi vizuri, mnatakiwa kutompa fomu ya kugombea maana haleti faida,” alisema.

Previous Post

RONALDO  AWASHA MOTO

Next Post

MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

Next Post
MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AMLILIA KARDINALI PENGO

RAIS DK. SAMIA AMLILIA KARDINALI PENGO

4 weeks ago
JUKWAA LA WANAWAKE LAIBUKA  NA MAAZIMIO 10 KUHUSU AMANI

JUKWAA LA WANAWAKE LAIBUKA  NA MAAZIMIO 10 KUHUSU AMANI

3 months ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?