• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

TANZANIA KAMILI AFCON 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
May 5, 2026
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
TANZANIA KAMILI AFCON 2027
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Dodoma

SERIKALI imetangaza kuwa miundombinu yote vikiwemo viwanja vya michezo vitakavyotumika katika michuano ya soka kwa Mataifa ya Afrika (AFCON 2027), vitakamilika mwezi Agosti, mwaka huu.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa  AFCON 2027 katika mashindano yatakayofanyika pia nchini Kenya na Uganda.

Hayo yalisemwa bungeni jijini Dodoma, jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara hiyo katika Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Makonda alisema wizara yake inaendelea na maandalizi ya mashindano hayo kwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo katika miji ya Dar es Salaam na Arusha.

Alisema tayari Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa sh. bilioni 76.1 ambayo ni ada ya uandaaji mashindano hayo yenye mvuto zaidi Afrika.

 UKARABATI VIWANJA

Makonda alisema hadi sasa ukarabati uwanja wa Benjamin Mkapa umefikia asilimia 95, ukarabati wa viwanja vitatu vya mazoezi vya Gymkhana, Meja Jenerali Isamuhyo na Shule ya Sheria umekamilika huku ujenzi wa viwanja vitatu vingine vya mazoezi vya Farasi, Leaders Club na Gymkhana II vipo katika hatua za awali.

“Ujenzi uwanja wa Arusha wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 32,000 umefikia asilimia 77.5 na ujenzi kiwanja kimoja cha mazoezi kinachojengwa katika eneo la uwanja wa Arusha umefikia asilimia 60. Ni matarajio yetu kuwa kufikia Agosti 2026, serikali itakuwa imekamilisha miundombinu yote kwa ajili ya AFCON 2027”.

Aliongeza: “Katika kudhihirisha dhamira ya dhati ya serikali kuhakikisha tunafanikisha mashindano ya AFCON 2027, tayari Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameridhia na kutoa dola 30,000,000 sawa na sh. bilioni 76.1 kama ada ya uandaaji mashindano husika. Hii ndiyo tafsiri halisi ya Dk. Samia kama mwanamichezo namba moja nchini.”

VITUO VYA MICHEZO

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), alisema serikali imeendelea kuwekeza katika maendeleo ya miundombinu mingine ya michezo nchini kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati yenye lengo la kukuza vipaji, kuboresha huduma za michezo kwa wananchi.

Alisema miradi mingine ambayo inatekelezwa ni ujenzi wa vituo vya kukuza vipaji, kikiwemo cha  Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 49.

Alisema ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Dodoma wenye uwezo wa kuchukua watizamaji 32,500 umefikia asilimia tano.

“Ujenzi Kituo cha Mazoezi na Kupumzikia Wananchi jijini Dodoma ambao umefikia asilimia 73.5, ujenzi wa Kituo cha Mazoezi na Kupumzikia Wananchi jijini Dar es Salaam kilichofikia asilimia 49 na ukarabati uwanja wa Uhuru  umefikia asilimia 70,” alisisitiza.

Previous Post

HAIJAPATA KUTOKEA

Next Post

RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

Next Post
RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM YAAHIDI UJEZI WA VITUO VITANO VYA AFYA, ZAHANATI20 WILAYA YA KWIMBA

CCM YAAHIDI UJEZI WA VITUO VITANO VYA AFYA, ZAHANATI20 WILAYA YA KWIMBA

8 months ago
YANGA YATAMBIA REKODI LIGI KUU

YANGA YATAMBIA REKODI LIGI KUU

1 month ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KAMILI AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?