• ePaper
Friday, August 28, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KUNENGE: JNHPP KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 21, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KUNENGE: JNHPP KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME NCHINI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Pwani

Na Mwamvua Mwinyi

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amesema uzinduzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), utakaofanyika kesho wilayani Rufiji mkoani hapa, ni atua kubwa ya kihistoria katika kuimarisha upatikanaji nishati ya uhakika nchini.

Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme unaotekelezwa kwa asilimia 60 katika Mkoa wa Pwani na asilimia 40 katika Mkoa wa Morogoro, unaonyesha dhamira ya serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya kuchochea shughuli za uzalishaji.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kunenge alisema mkoa wa Pwani unajivunia kuwa mwenyeji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.

“Mradi huu ulianza kutekelezwa kuanzia Serikali ya Awamu ya Tano. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliupokea ukiwa umefikia asilimia 30 ya utekelezaji, lakini sasa ameukamilisha hatua aliyofanikisha kutimizwa ndoto ya mwasisi wa mradi huo, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Alisisitiza: “JNHPP ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati ya nishati nchini, ukitarajiwa kusafirisha umeme kupitia njia mbalimbali za Gridi ya Taifa na vituo vya kupozea umeme vya Chalinze–Kinyerezi, Kwala–Zegereni–Zinga na Dundani–Msufini Mkuranga.”

Katika hatua nyingine, Kunenge alisema sekta ya viwanda na uwekezaji imeendelea kukua kwa kasi mkoani Pwani, ambapo kuna jumla ya viwanda vikubwa na vya kati 495.

Kuhusu uhifadhi wa vyanzo vya maji, Kunenge aliwataka wananchi kutunza vyanzo hivyo na kulinda mazingira yanayozunguka bwawa hilo.

Sanjari na matumizi ya maji kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, alibainisha kwamba serikali inapanga kujenga bwawa la maji safi litakalotumika kwa matumizi ya wananchi wa Pwani na Morogoro, huku mpango huo ukitarajiwa kunufaisha hadi Mkoa wa Lindi.

Previous Post

CCM YATAKA VIONGOZI WASIOYUMBA -WASIRA

Next Post

TUNDU LISSU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Next Post
TUNDU LISSU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

TUNDU LISSU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NEEMA YA MAJI KILA KIJIJI 2030

NEEMA YA MAJI KILA KIJIJI 2030

7 months ago
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA KUKABILI UKAME

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA KUKABILI UKAME

4 days ago

Popular News

  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI KUMRITHI BALOZI DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME YA MADINI YATOA SIKU 30 KWA WALIOKIUKA MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ARIDHIA DK. NCHIMBI KUJIUZURU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?