• ePaper
Sunday, September 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 18, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais Deogratius Ndejembi, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri zake kuhakikisha hali ya Dampo la Pugu inaboreshwa, huku akielekeza maeneo ya makazi yanayozunguka dampo hilo kupuliziwa dawa ili kuwalinda wananchi dhidi ya wadudu na kupunguza hatari ya magonjwa, hususan katika kipindi cha mvua.

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 18, 2026, alipofanya ziara katika Dampo la Pugu linalotumika kukusanya taka za Mkoa wa Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya eneo hilo na kusikiliza kero za wananchi wanaoishi maeneo ya jirani.

Aidha, ameelekeza kuandaliwa kwa mpango kazi wa pamoja utakaoainisha hatua za haraka na za muda mrefu za kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa Dampo la Pugu pamoja na kero zinazowakabili wananchi wanaoishi katika maeneo yanayolizunguka, ikiwemo kutopuliziwa dawa za kuua wadudu.


Akiwa katika dampo hilo, Ndejembi ameonesha kutoridhishwa na kutofautiana kwa takwimu kuhusu kiasi cha taka zinazokusanywa na kupelekwa katika Dampo la Pugu kila siku kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, amezitaka mamlaka zote zinazohusika kukaa pamoja, kuhakiki na kuweka takwimu sahihi zitakazokuwa msingi wa kupanga na kutekeleza hatua madhubuti za kuboresha usimamizi wa taka jijini Dar es Salaam.

“Hatuwezi kutatua changamoto za eneo hili bila kuwa na taarifa na takwimu sahihi. Hawa wananchi mnaowaona wamechoka na stori; wanataka kuona kazi,” alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema wananchi wanatarajia kuona matokeo ya moja kwa moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali, hivyo amewataka viongozi na taasisi husika kuharakisha utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha kero za wananchi zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Makamu wa Rais amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni Serikali sikivu inayojali maslahi ya Watanzania na itahakikisha changamoto za watanzania zinatatuliwa kwa wakati.

Previous Post

JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UVCCM YAWAPA POLE WALIOPATA MADHILA

UVCCM YAWAPA POLE WALIOPATA MADHILA

10 months ago
MAELFU WAFURIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM DAR

MAELFU WAFURIKA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM DAR

1 year ago

Popular News

  • NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KIFUA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?