• ePaper
Sunday, September 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 18, 2026
in Habari, Kitaifa
0
JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

RAIS mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, amewataka wanaume kupima afya ya tezi dume mara kwa mara, akisema uchunguzi wa mapema huwezesha kupatikana matibabu kwa wakati kabla saratani haijasambaa.

Dk. Kikwete ametoa wito huo jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Mwezi wa Uelewa wa Saratani ya Tezi Dume, yaliyofanyika katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni.

Katika maadhimisho hayo, Dk. Kikwete alitembelea mtambo wa kisasa wa High Intensity Focused Ultrasound (HIFU), unaotumika kutibu baadhi ya uvimbe, ikiwemo saratani ya tezi dume kwa wagonjwa wanaostahili, bila kufanyiwa upasuaji wa kawaida. Teknolojia hiyo hutumia mawimbi ya sauti yenye nguvu kuelekeza joto katika sehemu iliyovimba.

Akielezea uzoefu wake, Dk. Kikwete alisema alipogundulika mapema kuwa na dalili za saratani ya tezi dume mwaka 2014, aliamua kufanyiwa uchunguzi wa kina Marekani.

Amesema vipimo vilichukuliwa na kuthibitisha kuwa saratani ilikuwa katika hatua za awali, hali iliyomwezesha kuchukua hatua za matibabu mapema.

“Walichukua sampuli 14 na katika sampuli mbili wakaona dalili za saratani. Madaktari wakaniambia kuwa ilikuwa inaanza na kwamba ingeweza kutibika,” alisema.

Amesema alikubali kufanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume kuzuia saratani isisambae katika sehemu nyingine za mwili, na kwamba tangu wakati huo ameendelea kuwa na afya njema.

“Baada ya kufanyiwa upasuaji nilijenga utaratibu wa kupima afya yangu mara kwa mara. Kwa sasa afya yangu ni njema kabisa; ndiyo maana mtu akisema ninaumwa, nacheka tu, kwa sababu ninaifahamu afya yangu,” amesema.

Previous Post

KOCHA SIMBA KIFUA MBELE

Next Post

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

Next Post
NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI KUENZI MEMA YA LUKUVI

SERIKALI KUENZI MEMA YA LUKUVI

6 months ago
NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

NITASHIRIKIANA NAYE KULETA MAENDELEO

1 year ago

Popular News

  • NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JK ATOA USHUHUDA DALILI SARATANI TEZI DUME

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA KIFUA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?