• ePaper
Friday, October 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 17, 2026
in Burudani, Michezo
0
FUNZO JIPYA KADI NYEKUNDU YANGA
0
SHARES
14
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

BAADA ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi amejifunza kuwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa kiungo wa timu hiyo, Stephane Aziz KI imewapa uzoefu wa kucheza muda mrefu wakiwa pungufu.

Pia, alisema tukio hilo, limeisaidia timu kujenga tabia ya kujiandaa kwa changamoto zinazoweza kutokea katika  msimu mzima.

Yanga juzi iliitandika bao 1-0  timu ya Geita Gold katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Dar es Salaam.

Bao la ushindi lilipachikwa wavuni na beki wa timu hiyo, Farouk Koumara katika dakika ya 54 ya mchezo.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Mngqithi alisema hakuridhishwa na uamuzi wa mwamuzi kumpa kadi nyekundu  Aziz KI kwa vile hakuona nia ya kumdhuru mpinzani.

Hata hivyo, kocha huyo alifurahishwa na namna wachezaji wake walivyopambana licha ya kumkosa Aziz Ki.

Alisema changamoto kubwa ilikuwa kupoteza uwezo wa kufanya presha ya juu kusaka mabao zaidi.

Hata hivyo, kocha huyo alisema waliamua kubadilisha baadhi ya mipango yao kipindi cha pili na wachezaji wake kufanikiwa kupambana kupata matokeo mazuri.

Mngqithi aliwashukuru wachezaji wake  kwa kuipambania timu mwanzo mwisho kuhakikisha wanafanya vizuri na kufikia malengo waliojiwekea.

“Ukweli kadi nyekundu alionyeshwa Aziz Ki imewaongezea wachezaji wangu ubora na uzoefu wa kucheza muda mrefu wakiwa pungufu,” alisema Mngqithi.

Kocha huyo alifafanua kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanapata alama tatu katika kila mchezo.

Mngqithi amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Clement Mzize kuwa kizuri na ana imani, atafanya vizuri licha ya kukaa nje kwa takribani miezi saba bada ya kupata majeraha.

Kocha huyo alisema Mzize ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika mipango yake na anatamani aendelee kuwa fiti msimu huu ili aisaidie timu kushinda mabao mengi zaidi.

Aidha, Mngqithi alisema anasubiri kwa hamu kurejea kwa beki Dickson Job, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na kikosi kamili na wachezaji wote wakiwa katika afya njema.

Mngqithi alisema kuwa kuhusu baadhi ya wachezaji aliowapumzisha katika mchezo wa dhidi ya Geita Gold, hawakuwa na majeraha, bali aliamua kuwapa mapumziko kutokana na kucheza michezo kadhaa mfululizo.

Kocha wa Geita Gold, Zuberi Katwila, alisema  kadi nyekundu aliyoonyeshwa  Aziz KI dakika ya 18, haikufanya timu hiyo kuwa dhaifu.

“Kiukweli pamoja na  mchezaji wa Yanga kupewa kadi nyekundu, timu yao haikuwa dhaifu na wao kushindwa kutumia vyema nafasi waliokuwa nayo ya kupata ushindi, hivyo wanaenda kurekebisha kasoro zilizojitokeza,” alisemaila.

Katwila alisema ana imani kubwa na wachezaji wake kwani wamefanya makosa na wapinzani wake wameyatumia vyema  kupata ushindi.

Previous Post

WALIOTELEKEZA NIDA KUBANWA

Next Post

KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

Next Post
KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

KASI MAANDALIZI AFCON 2027 YAIKUNA CAF

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TRA YANG’ARA ROBO YA TATU:MAKUSANYO YAVUKA MALENGO KWA KASI YA AJABU

TRA YANG’ARA ROBO YA TATU:MAKUSANYO YAVUKA MALENGO KWA KASI YA AJABU

7 months ago
DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

1 year ago

Popular News

  • WAZIRI ULEGA AAGIZA UKAGUZI WA MAHABUSU NCHINI

    WAZIRI ULEGA AAGIZA UKAGUZI WA MAHABUSU NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYERERE ANAISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MA-RC WABEBESHWA BIMA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AMPA TANO JIHAN DIMACK

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HATIMAYE IMELIPA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?