• ePaper
Sunday, July 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. SAMIA AAHIDI UWANJA WA SOKA DODOMA KUKAMILIKA MWAKA 2027

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 1, 2025
in Habari, Kitaifa, Michezo, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AAHIDI UWANJA WA SOKA DODOMA KUKAMILIKA MWAKA 2027
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

VICTOR MKUMBO Na

AMINA KASHEBA

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan ameahidi kwamba hadi kufikia mwaka 2027 ujenzi wa Uwanja wa soka wa kisasa wa Dodoma utakuwa umekamilika.

Aliyasema hayo jana katika kampeni yake iliyofanyika v iwanja vya Tambukareli  jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wananchi.

“Tunakwenda kumaliza uwanja wa soka wa kimataifa, ni matumaini yetu ifikapo mwaka 2027 utakuwa umeshakamilika ili utumike katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027),” alisema Dk. Samia.

Alisitiza tayari mkandarasi alishapatikana ambapo anatarajia kuanza kazi ya ujenzi hivi karibuni.

“Tumejipanga kukamilisha ujenzi wa uwanja mkubwa wa soka wa Dodoma na mkandarasi tayari alishapatikana na ataanza kufanya kazi ya ujenzi hivi karibuni,” alisema.

Dk. Samia alisema Uwanja wa Dodoma ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 32,500 ambapo utajengwa na Kampuni ya Limonte Group ya Italia.

Katika kampeni hizo zilipambwa na burudani za wasanii mbalimbali wakiwemo Rajabu Kahali ‘Haromize’, Kontawa, Barobaro, Abdallah Sultan ‘Dullah Makabila’ na kikundi cha ngoma ya asili.

Mbali ya wasanii hao kutoa burudani katika kampeni hizo, nyota wa muziki wa bongo fleva, Harmonize alikuwa mwimbaji wa kwanza kuwanyenyua vitini viongozi baada ya kutoa burudani ya wimbo wake wa ‘Mama Anashindwaje’.

Wakati Harmonize anaimba viongozi wakiongozwa na Dk. Samia walionekana wamesimama na wengine kucheza kwa dakika 10 huku msanii huyo akitoa burudani ya aina yake na kuibua shangwe kwa wananchi waliojitokeza.

Previous Post

KIBU DENIS, MANULA WATEMWA STARS

Next Post

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

Next Post
ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TOTTENHAM YAHAMIA KWA AKANJI

TOTTENHAM YAHAMIA KWA AKANJI

11 months ago
DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA

DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA

4 months ago

Popular News

  • KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA AIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWALIMU, GUEYE WAPO SIMBA SANA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI ASHTUKIA ‘USANII’ WA WACHIMBAJI MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?