• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

TOTTENHAM YAHAMIA KWA AKANJI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 1, 2025
in Burudani, Michezo
0
TOTTENHAM YAHAMIA KWA AKANJI
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

LONDON,

England

TOTTENHAM  Hotspur inaendelea na kazi kubwa ya kutaka kumsajili beki wa Manchester City, Manuel Akanji.

 Imeeleza kuwa timu hiyo ya England, imepania kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.

Hata hivyo, Tottenham inaweza kukutana na upinzani kutoka kwa klabu za AC Milan na Crystal Palace kupata sahihi yake.

Timu zote zinawania saini ya mchezaji huyo kwa ajili ya kumsajili aweze kuichezea timu moja wapo kati ya hizo.

Manuel Akanji hivi  karibuni alikataa ofa ya kujiunga na timu ya Galatasaray.

Alikanusha taarifa hizo zilizokuwa zimeenea kuwa yupo mbioni kutua nchini Uturuki.

Hata hivyo, nyota huyo ameweka wazi kwamba bado anatafakari mustakabali wake na Manchester City.

Manuel Obafemi Akanji ni mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Uswisi ana mkataba na klabu ya Man City.

Mlinzi huyo alizaliwa Neftenbach nchini Uswisi,Julai 19, mwaka 1995 amefikisha miaka 30.

Alijiunga na Manchester City, mwaka 2022  amewahi kuichezea timu ya Borussia Dortmund.

Akanji alitua katika kikosi cha B orussia mwaka 2018 akitokea Uswisi.

(Gazetta Dello Sport)

CHELSEA KUIBOMOA BARCA

CHELSEA ipo tayari kutoa ofa nono kunasa saini ya Fermin Lopez.

 Timu hiyo ya England inamtaka nyota huyo  mwenye umri wa miaka 22 mwenye thamani pauni milioni 78 ndani ya klabu ya Barcelona FC.

(Mundo Deportivo)

WEST HAM YAINGIA VITANI

KLABU ya West Ham imeingia  vita ya kusaka saini ya Fabio Vieira kutoka Arsenal.

Hata hivyo, West Ham itakutana na upinzani kutoka kwa timu ya Stuttgart  na klabu nyingine zinazoshiriki Bundesliga  kumnasa kiungo huyo Mreno mwenye miaka 25.

(Sky Sports Germany)

RB LEIPZIG YAVAMIA LIVERPOOL

TIMU ya RB Leipzig  imevamia klabu ya Liverpool kutaka kumsajili kiungo na England, Harvey Elliott.

Mchezaji huyo anaichezea timu ya Taifa ya England U21, huenda akaziba nfasi ya Xavi Simons, hata hivyo RB Leipzig bado inasita kutoa uamuzi juu ya dau linalotakiwa na Liverpool.

(ESPN)

BOYOMO HUYOO ASTON VILLA

ASTON Villa inatarajiwa kukamilisha uhamisho wa beki wa Osasuna,Enzo Boyomo.

Mlinzi huyo ana miaka 23 ni raia wa Cameroon huenda akanunuliwa na Aston Villa kwa pauni milioni 21.25. (The Telegraph)

Previous Post

ZANZIBAR MPYA YA DK. MWINYI YAVUTIA WANANCHI

Next Post

MBETO : HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM ZANZIBAR 2025-2030

Next Post
MBETO : HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM ZANZIBAR 2025-2030

MBETO : HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM ZANZIBAR 2025-2030

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWINYI ACHUKUA FOMU ZANZIBAR, AHADHARISHA CHUKI

DK. MWINYI ACHUKUA FOMU ZANZIBAR, AHADHARISHA CHUKI

8 months ago
DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

6 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?