• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Makala

DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 20, 2025
in Makala, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA ANAVYOTAFSIRI ‘KAZI NA UTU’ KWA VITENDO

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MUSSA YUSUPH

KAZI ni shughuli yoyote ya kimwili au kiakili anayoifanya mtu kwa lengo la kupata matokeo fulani iwe kipato, huduma, maendeleo binafsi au ya kijamii.
Kitaaluma, kazi hufafanuliwa kama mchakato wa kutumia maarifa, ujuzi na nguvu ili kuzalisha bidhaa au huduma kwa lengo la kupata ujira fulani.
Kijamii, kazi ni wajibu unaomfanya mtu kuwa sehemu ya maendeleo ya familia, jamii na Taifa.


Lakini pia, kazi humfanya mtu awe mwenye thamani na heshima mbele ya jamii. Kwa kufanya kazi halali, mtu hujenga utu wake kama raia mwema anayechangia maendeleo ya Taifa.

Kazi yenye utu siyo kwa faida binafsi tu, bali ni huduma kwa wengine. Mfano, mwalimu anapofundisha kwa moyo au daktari anapotibu kwa huruma, anaonyesha utu wake kupitia kazi.

Kwa upande wake, Utu ni asili ya ubinadamu inayomtofautisha mtu na viumbe wengine ikijumuisha heshima, maadili, wema, huruma na usawa. Utu huoneshwa kupitia namna mwanadamu anavyoheshimu na kuthamini wenzake. Utu pia ndiyo msingi wa maadili ya kijamii unaojenga mshikamano na upendo.

Mtu anapofanya kazi kwa uadilifu, bidii na kujituma, kazi hiyo hugeuka kuwa kielelezo cha utu wake. Utu wake unaonekana katika jinsi anavyoheshimu muda, anavyowajibika na kutojipatia mali kwa njia za hila.

Utu wenye maadili (kama uaminifu, uadilifu na heshima) ndiyo unaoongoza namna kazi inavyofanyika. Bila utu, kazi inaweza kufanyika lakini kwa ubinafsi, wizi au dhuluma.

Bila utu, kazi hubaki kama biashara tupu. Bila kazi, utu unaweza kubaki dhana isiyoonekana kwa vitendo.
Mara baada ya kipyenga cha uchaguzi mkuu kupulizwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Mgombea wake wa Urais, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kinatumia kauli mbiu ya ‘Kazi na Utu, Tunasongambele.’

Kauli mbiu hiyo inaamisha kwamba kazi na utu ndiyo msingi wa maendeleo katika jamii yeyote ile. Taifa lisilothamini utu wa watu wake ni vigumu likapiga hatua za maendeleo kwa sababu matokeo ya kazi bora yanaanzia namna unavyowatendea wale uliowapa majukumu.

Katika kipindi cha miaka minne tangu Dk. Samia alipoingia madarakani uongozi wake umetafsiri kwa vitendo maana halisi ya Kazi na Utu. Kuanzia utekelezaji miradi yenye kugusa maisha ya wananchi, demokrasia, uwezeshaji wananchi kiuchumi, ushirikishwaji makundi yote katika ngazi za maamuzi na vita dhidi ya ubadhirifu.

Rais Dk. Samia amekuwa akisisitiza siasa za mshikamano, majadiliano na maridhiano badala ya mgawanyiko ili kila Mtanzania afurahie matunda ya demokrasia. Amefungua milango ya mazungumzo, uhuru kwa vyombo vya habari na taasisi za kiraia, jambo linalowapa wananchi nafasi ya kushiriki mijadala bila uwoga.

Kadhalika, serikali yake imewekeza katika elimu, afya na maji safi, kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi ya kuishi kwa kupata huduma muhimu za kijamii.

Akiwa katika mikutano yake ya kampeni, Dk. Samia amekuwa akisisitiza umuhimu wa kujenga uchumi jumuishi wenye kugusa maslahi ya kila mmoja.
Amekuwa akipinga dhana ya serikali kuwa ya kundi fulani la kijamii bali msisitizo wake ni kwamba kila mwananchi awe maskini, tajiri, mwenye ulemavu, aishiye vijijini au mijini ana haki ya kunufaika na rasilimali za nchi.

Mathalani, alipokuwa akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Nanenane Ipuli mkoani Tabora, Dk. Samia alisema CCM imedhamiria kujenga uchumi jumuishi unaozingatia ustawi wa wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.

Alisisitiza kuwa msingi mkuu wa kauli mbiu ya ‘Kazi na Utu’ ni dhamira ya kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye kujitegemea na kuneemesha watu wake.
“Leo nchi yetu inaendeleza mapambano ya uhuru wa kujitegemea kiuchumi. Tayari uhuru wa siasa tulishaupata mwaka 1961, leo tunakwenda katika mapambano ya kujitegemea uhuru wa kiuchumi.

“Uhuru wa kujenga taifa lenye uchumi jumuishi linalotegemea na linalozingatia ustawi wa watu wote. Na ndiyo maana tunasema Kazi na Utu, Tunasonga mbele,” alisisitiza.

Alibainisha kuwa CCM inataka kujenga taifa linalojitegemea na linalozingatia ustawi wa watu. Katika mapambano hayo, alibainisha kuwa CCM inaendeleza yale ambayo Baba wa Taifa aliyasisitiza kwa kusema wananchi ni sisi sote kwa pamoja.

“Maendeleo ni yetu na juu yetu wenyewe. Maendeleo tunayoyataka ni maendeleo ya watu, yaletwe na watu wenyewe, yaendelezwe na watu wenyewe na yawafuate watu kule walipo,” alisisitiza.

Alisema hiyo ndiyo maana halisi ya uchumi jumuishi ambao CCM imedhamiria kuujenga kuleta maendeleo mijini na vijijini.

Vilevile, wakati akizindua kampeni za uchaguzi mkuu katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam Agosti 28 mwaka huu, Dk. Samia alieleza kwa kina namna ambavyo serikali yake itakavyojika kuzingatia zaidi utu wa watu wake kwa kutekeleza mambo 13 ndani ya siku 100 pindi akipewa ridhaa ya kuliongoza Taifa.

Alisisitiza kuwa serikali atakayoiunda itajikita kuleta mabadiliko yenye kugusa maslahi ya wananchi moja kwa moja katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Miongoni mwa mambo ambayo ameahidi kuyatekeleza ndani ya siku 100 ni kutoa ajira 12,000 kwa walimu na wataalamu wa afya, serikali kutoa matibabu bure kwa wajawazito, wazee na Watoto kupitia mpango wa bima ya afya kwa wote.

“Kupitia Bima ya Afya kwa Wote, tutazindua mfumo wa mfumo wa taifa kwa wamu ya majaribio kuanzia wazee, wototo, wajawazito ambapo gharama za matibabu zitabebwa kupitia mfuko wa bima ya afya.

“Pia, serikali itagharamia kwa asilimia 100 wananchi wasiokuwa na uwezo kupata vipimo vya figo, moyo, sukari, mishipa ya fahamu na mifupa. Tutatoa ajira 5000 katika sekta ya afya ndani ya siku 100 wakiwemo wauguzi na wakunga.

Alisisitiza: “Tutapia marufuku hospitali kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa kwa sababu ya kudaiwa gharama za matibabu. Tutakuja na mfumo mwingine kuhakikisha jamaa wa marehemu wanalipa gharama lakini siyo kuzuia miili.”

Dk. Samia alisema ndani ya siku 100 serikali yake itaweka mkakati wa elimu kisayansi ambao kila mtoto wa darasa la tatu atakuwa na uwezo wa kusoma, kuandika bila shida, sambamba na kuajiri walimu 7,000 wa masomo ya hisabati na sayansi.

“Tutazindua mpango wa pamoja utakaohusisha waajiri, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu, kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta za kipaumbele. kuwafanya wanafunzi wa VETA kuchukuliwa viwandani kufanyakazi zao za mazoezi.

“Tutatenga sh. bilioni 200 kuwezesha upatikanaji mitaji kwa wafanyabiashara wadogo na kati, uanzishwaji kampuni changa, kurasimisha wajasiriamali wadogo wakiwemo bodaboda, mama lishe, wafanyaviashara wadogo kuingizwa katika mfumo rasmi wa serikali.

Vilevile, alisema serikali itaanzisha programu ya mitaa ya viwanda wilayani kwa lengo la kuzalisha ajira kupitia mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi madini na misitu.
Pia, alisema katika siku hizo, serikali itakayoiunda itaanza ujenzi wa gridi ya taifa ya maji kwa lengo la kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji.

Alisema gridi hiyo itahusisha vyanzo vikuu vya maji ambavyo ni Ziwa Viktoria, Tanganyika, Nyasa na mito mikubwa.

Ahadi nyingine aliyoitoa ni kuendeleza jitihada nishati safi kupikia ili kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, kuweka mifumo rafiki ya uwajibikaji kwa mawaziri na wakuu wa mikoa kutakiwa kutoa taarifa na kujibu maswali kwa wananchi kwa njia ya simu.

Kwa jumla, Dk. Samia amekuwa akisisitiza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo endapo akipewa fursa na wananchi kuendelea kuongoza nchi, serikali yake itaendelea kuimarisha heshima na thamani ya kila Mtanzania, siyo kwa maneno tu bali kwa vitendo vitakavyojielekeza kufungua fursa za kiuchumi ili kila mwananchi ashiriki ujenzi wa Taifa na kwa kujali utu.

Previous Post

DK. MIGIRO ATAJA SABABU ZITAKAZOMPA USHINDI DK. SAMIA

Next Post

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

Next Post
DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

DK. SAMIA : UTAKUWA UCHAGUZI WA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

Rais Samia atoa maelezo kuhusu maendeleo ya uchumi

2 months ago
ICHAGUENI CCM, ILANI YAKE INATEKELEZEKA – WASIRA

ICHAGUENI CCM, ILANI YAKE INATEKELEZEKA – WASIRA

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.